Anataka Kutoa Mimba -Nimemkatalia

Status
Not open for further replies.
Huna sababu ya kuwa njia panda. Msimamo ndio huo na usidhubutu kufanya hivyo. Vinginevyo, ukimkubalia huenda ikaja onekana mimba yako. Keep it up.
 
hivi watu wanafanyaje mapenzi jamani bila kufikiria mara mbili mbili? li mtu umekutana nalo tu hata kinga hamtumii?jamani matatizo mengine ni ya kujitakia kabisaaaa.
hata mie sielewi dear!kuna watu wanajilipua mabomu wazima wazima!hapo kajua ana mimba huwezi jua kanasa kipi kingine!
 
-pole sana,lazima uwe dilemma kwa kuwa ni mtu wa karibu sana

Kwanza,mshauri huyo dada madhara ya kutoa hiyo Mimba,sidhani kama kuna watu wanaojutia kulea Mimba ukilinganisha na wanaotoa

Pia,mwambie alee tu kisha atampata mtu wa kumuasili huyo mtoto

Pili,msaidie kutafuta msaada kutoka katika wanaharakati mbalimbali wamsaidie kumtafutia msaada wa kisheria ili apate haki ya mtoto wake wa kwanza kutoka kwa baba yake.inawezekana anakimbia majukumu tu,DNA itamuumbua kama an uhakika

Tatu,mpatie au mtafutie msaada wa kumlipia ada mtoto na pia mtafutie msaada wa hela za clinic na malezi madogo madogo ya Mimba for the time being coz mtu akishafikia hali hii hakawii kujitoa uhai.Najua ni ngumu but jaribu tu kumsaidia

kwa kumalizia,naomba kuuliza,huyo dada ana kiwango gani cha elimu na au ana ujuzi wa kazi gani?

Mwisho,maisha bora kwa kila mtanzania isingekua an ideal slogan basi huyu dada angeweza kuyamudu yote hapo juu na wala asingefikiria kuua kiumbe hai kisicho na hatia na wala hilo tatizo la pili lisingekuwa kubwa kiasi hicho
 
jamani mbn hivi,wangapi wanatafuta watoto hawapati?wangapi wapiga goti bado God hasnt smiled on them?wangapi wanahangaika kwa waganga na kupoteza mijihela kibao?kwann unataka kuua?kwann ulijidhalilisha?si uende kwenye vituo husika na kueleza matatizo yako?plz give me two yrs nafungua kitu pia will help u on that,my dia uliza walotolewa,now deiz watu wanageuzwa kizazi kabisa ili wasipate mimba tena,ww ungetolewa ungekuwa wapi?ungetolewa ungejua reha ya starehe zote ulizofanya?ungetolewa ungejua utamu wa ugali na dagaa na mlenda japo ww ni maskini lkn si unakula na kushiba?plz usitoeGod will make away plz.
@gnder :take actin dnt worry about ujirani one dei she will understang,by the way
You don't get paid for the hour. You get paid for the value you bring to the hour.
 
Jamani kwani huko kwao kulikuwa hakuna condoms, mwambie hasithubutu kutoa hiyo mimba kwanza ni kosa kisheria lakini ni kumkosea haki huyo kiumbe ambaye ameanza kuonja matamu na machungu ya nchi.

Pili mwambie aache hata kuwaza kutoa mimba kwani hicho kiumbe kinasikia kila kitu na kinaogopa na kumchukia huyo Mama yake kwamaana hiyo hata akizaliwa atakuwa anamchukia Mama yake kwakuwa alishajua mbinu zake za kutaka kumuua hadi aliposhauriwa na wanaJF

By the way kwanini wewe GS husiileee hiyo mimba? Hii nakupa kama bonasi ya Pasaka
 
Nawashukuru wote mliotoa michango yenu katika mada hii.Jamani hakuna asiyefahamu kama kutoa mimba ni dhambi mbele za MUNGU na nikosa kisheria,hilo analifahamu na nimezungumza naye kwa kirefu kabisa.Kuna wengine mnamalaumu kwa kulala na mwanaume huyu,na wengine hata kulala na huyu jamaa bila kondomu kifupi ni kwamba haikuwa ridhaa yake kufanya alichokifanya ila alibanwa kwenye kona akawa hana jinsi.Ni rahisi kulaumu kosa linapokuwa kwa mwenzako lakini mkumbuke kuwa watu tunaishi katika mzaingira na life staili tofauti kabisa..Kuna wengine mmeshauri kwamba nimsadie kumtafutia gharama za shule za mtoto hikli liko ndani ya uwezo wangu ndicho kitu nilichomuahidi na nitakifanya..Kuna wengine mmesema kwamba mko tayari kulea mtoto atakayezaliwa endapo dada huyu atajifungua.,jamani this is a serious issue kama kweli mtu uko tayari tafadhali naomba uni PM ili tumsaidie dada huyu kwa pamoja...Kuna mtoto tayari anayehitaji malezi mnaweza kumsadia hata huyu,bado mdogo ndio kwanza yuko kidato cha kwanza.
 
-GS umefanya jambo la Maana sana,hongera kwa hilo.

Huyo dada vipi ana elimu kiasi gani au ujuzi gani?
 
Mungu atakuwa upande wake, amtegemee mungu zaidi, asiitoe mimba hiyo maana ni hatari kwake na kiumbe pia kumchukiza mungu. Hivyo namshauri ajifungue kwanza huku akimlocate baba mwenye mtoto, kisha kama inawezekena amfikishe ustawi wa jamii na mbele ya vyombo vya sheria na wapime vinasaba kama ataweza kupata msaada. At mean time just seat down with her as her neighbour, try to counsel her on how to handle that matter. The great fears that she has in mind is the fear of responsibilities ahead brought by fear of rejection. Fear and risks are always there but we need to manage/control it. If she could had some money she could not able to see you and she would had fulfiled her goal. God is able.

Man proposes, God disposes. Poverty is the mother of crime
 
Sio mimba tu naomba pia acheki afya yake pia maana ninachoona hapa mchezo haukuwa salama, umefanya makosa dada kwa kumpa live huku ukijua lengo lake si zuri. Kama utakuwa salama umshukuru mungu na ujipange upya. Take care

It is easy to be wise after the event. Hasty climbers have sudden falls.
 
1.Mweleze kuwa kutoa mimba kunaweza kusabaisha nae akafa.
2.Mweleze pia kuwa siku zote asifanye mapenzi bila condom,labda kwa mumewe tu na hata huyo mume pia akimwona ana macho miamia amvalie condom.
3.Mweleze pia aende akapime ajue kama kaambukizwa au la.
4.Mweleze asikate tamaa,matapeli wa mapenzi wako kibao.Apange na ajiandae ataishije na mwanae mpya.
5.Mwisho afanye juu chini atafute ndugu zake/wazazi wa huyo jamaa,wanawezakusaidia kulea.
 
Nikiwa nimekaa nyumbani kwangu jana usiku nikifuatilia tamthlia ya Ruby mara nikapata mgeni.Mgeni huyu ni jirani yangu.Akaniomba nitoke nje ili tukaongelee huko.Akanileleza habari yake kwa kirefu.Kifupi ni kwamba yeye ni binti wa miaka 33 ana mtoto aliyemaliza darasa la saba mwaka jana na mtoto huyo amechaguliwa kuendelea na kidato cha kwanza hapa jijini Dar es salaam.Anasema kwamba mtoto huyu baba yake alimkataa tangu akiwa mimba hovyo kwa kipindi cha miaka yote hii amekuwa akimtunza yeye mwenyewe.Yeye anafanya kazi za kubahatisha.Baada ya mtoto wake huyu kufaulu anahitaji mahitaji mbalimbali ya kumfanya aweze kwenda shule na yeye uwezo hana.Baada ya kutafakari kwa kina akaona bora amtafute mwanaume fulani aliyekuwa akimtongoza siku za nyuma kwa lengo la kuomba msaada wa fedha ili mwanae aende shule.Jamaa akampa masharti huyu dada kwamba kama anataka kumsadia ni lazima akubali afanye naye mapenzi.Mdada hakuwa na jinsi zaidi ya kukubali..Anasema baada ya kufanya mapenzi na bwana huyu,bwana huyu akaingia mitini bila kumpa dada huyu ujira wake..Hivi sasa dada huyu ni mjamzito na jamaa hapokei kabisa simu za huyu dada..Dada huyu kanifuata jana na kutaka nimpe hela ili aende akatoe mimba kwani anadai hawezi kuzaa mtoto mwingine asiye na baba.Imani yangu ya dini hairuhusu kutoa mimba wala mimi mwenyewe kama mwanaharakati siungi mkono suala la kutoa mimba..Nimemkatalia kabisa,najua ujirani wetu uko mashakani..Niko njia panda.

Hapo kwenye kikolezo. Ina mana alikuwa anatarajia ujira wa pesa..... hakujua kuna kinga dhidi ya mimba zisizotarajiwa na magonjwa y akuambukiza kama UKIMWI na magonjwa mengine ya zinaa?..Mianamike mingine bana!
 
Nikiwa nimekaa nyumbani kwangu jana usiku nikifuatilia tamthlia ya Ruby mara nikapata mgeni.Mgeni huyu ni jirani yangu.Akaniomba nitoke nje ili tukaongelee huko.Akanileleza habari yake kwa kirefu.Kifupi ni kwamba yeye ni binti wa miaka 33 ana mtoto aliyemaliza darasa la saba mwaka jana na mtoto huyo amechaguliwa kuendelea na kidato cha kwanza hapa jijini Dar es salaam.Anasema kwamba mtoto huyu baba yake alimkataa tangu akiwa mimba hovyo kwa kipindi cha miaka yote hii amekuwa akimtunza yeye mwenyewe.Yeye anafanya kazi za kubahatisha.Baada ya mtoto wake huyu kufaulu anahitaji mahitaji mbalimbali ya kumfanya aweze kwenda shule na yeye uwezo hana.Baada ya kutafakari kwa kina akaona bora amtafute mwanaume fulani aliyekuwa akimtongoza siku za nyuma kwa lengo la kuomba msaada wa fedha ili mwanae aende shule.Jamaa akampa masharti huyu dada kwamba kama anataka kumsadia ni lazima akubali afanye naye mapenzi.Mdada hakuwa na jinsi zaidi ya kukubali..Anasema baada ya kufanya mapenzi na bwana huyu,bwana huyu akaingia mitini bila kumpa dada huyu ujira wake..Hivi sasa dada huyu ni mjamzito na jamaa hapokei kabisa simu za huyu dada..Dada huyu kanifuata jana na kutaka nimpe hela ili aende akatoe mimba kwani anadai hawezi kuzaa mtoto mwingine asiye na baba.Imani yangu ya dini hairuhusu kutoa mimba wala mimi mwenyewe kama mwanaharakati siungi mkono suala la kutoa mimba..Nimemkatalia kabisa,najua ujirani wetu uko mashakani..Niko njia panda.
Yaani nimefika hapo kwenye red ikabidi nikomment kabla kuendelea. Unamuita mama wa miaka 33 binti duh!
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom