Anataka Kutoa Mimba -Nimemkatalia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anataka Kutoa Mimba -Nimemkatalia

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Regia Mtema, Mar 31, 2010.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #1
  Mar 31, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Nikiwa nimekaa nyumbani kwangu jana usiku nikifuatilia tamthlia ya Ruby mara nikapata mgeni.Mgeni huyu ni jirani yangu.Akaniomba nitoke nje ili tukaongelee huko.Akanileleza habari yake kwa kirefu.Kifupi ni kwamba yeye ni binti wa miaka 33 ana mtoto aliyemaliza darasa la saba mwaka jana na mtoto huyo amechaguliwa kuendelea na kidato cha kwanza hapa jijini Dar es salaam.Anasema kwamba mtoto huyu baba yake alimkataa tangu akiwa mimba hovyo kwa kipindi cha miaka yote hii amekuwa akimtunza yeye mwenyewe.Yeye anafanya kazi za kubahatisha.Baada ya mtoto wake huyu kufaulu anahitaji mahitaji mbalimbali ya kumfanya aweze kwenda shule na yeye uwezo hana.Baada ya kutafakari kwa kina akaona bora amtafute mwanaume fulani aliyekuwa akimtongoza siku za nyuma kwa lengo la kuomba msaada wa fedha ili mwanae aende shule.Jamaa akampa masharti huyu dada kwamba kama anataka kumsadia ni lazima akubali afanye naye mapenzi.Mdada hakuwa na jinsi zaidi ya kukubali..Anasema baada ya kufanya mapenzi na bwana huyu,bwana huyu akaingia mitini bila kumpa dada huyu ujira wake..Hivi sasa dada huyu ni mjamzito na jamaa hapokei kabisa simu za huyu dada..Dada huyu kanifuata jana na kutaka nimpe hela ili aende akatoe mimba kwani anadai hawezi kuzaa mtoto mwingine asiye na baba.Imani yangu ya dini hairuhusu kutoa mimba wala mimi mwenyewe kama mwanaharakati siungi mkono suala la kutoa mimba..Nimemkatalia kabisa,najua ujirani wetu uko mashakani..Niko njia panda.
   
 2. bht

  bht JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  Good manners are of more importance than Laws

  GS ni hivyo tu kwa sasa
   
 3. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #3
  Mar 31, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  kwakweli upo sahihi na simamia msimamo wako na jaribu kumshauri vizuri na kumpa madhara ya kutoa mimba kwani ukimpa msaada ni kwamba na ww umeshiriki dhambi ya kuua asilimia mia
   
 4. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #4
  Mar 31, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  bht bana..Haya nashukuru.
   
 5. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #5
  Mar 31, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,745
  Likes Received: 3,182
  Trophy Points: 280
  Kama utapata nafasi tena ya kuweza kuzungumza naye fanya hivyo. Mweleze nini hasara ya kutoa mimba si kwamba ni kinyume tu na mapenzi ya mungu bali pia kwa afya yake na umuhimu wa uhai kwa kiumbe alichobeba. Awe mvumilivu ataweza kama ameweza kwa huyo aliye naye sasa na huyu naye mungu atamjalia ataweza. Azikatae nguvu za shetani na mambo yake katika hili. Mungu ni mwema kwetu sote ndio maana alituumba kwa mfano wake.
   
 6. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #6
  Mar 31, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  according to your story wewe ni mchango mkubwa wa hiyo zahma na nasikitika kwamba wewe kama mgombea ubunge bado uko kimnya wakati kuna vyombo husika vya sheria vinaweza kufanya hii kazi
   
 7. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #7
  Mar 31, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,710
  Trophy Points: 280
  Umefanya vizuri sana mama endelea kushauri asitoe kabisa!
   
 8. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #8
  Mar 31, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  weee braza genekai si umeaga wee na tukakwambia tutakumiss,april fool nini?
   
 9. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #9
  Mar 31, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  na wewe si ulisema uunabadili avata wewe,............. ama nayo ilikuwa april fool in advance?................
   
 10. PJ

  PJ JF-Expert Member

  #10
  Apr 1, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 297
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kama una uwezo jitolee kumsaidia huyo mtoto wake aliye shuleni ili kumuondolea frustration huyu dada na Mungu kwa njia zake za ajabu atakurudishia na kukuongezea pale utakapopungukiwa
   
 11. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #11
  Apr 1, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  usimpe chochote

  usije ukatenda dhambi kwa mawazo, kwa maneno, kwa vitendo na kwa kutimiza wajibu wa kumpa huyu mama pesa.

  kuna zaid ya hilo, wakati hajampata huyo jamaa maisha yake alikuwa anayaendesha vip?
   
 12. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #12
  Apr 1, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  mwambie azae kisha na amgawe mtoto....................nafikiri kuna watu kadhaa wa kadhaa waliokuwa wanatafuta watoto hawana.
   
 13. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #13
  Apr 1, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Sawa kabisa.
   
 14. K

  Kindimbajuu JF-Expert Member

  #14
  Apr 1, 2010
  Joined: Jul 8, 2009
  Messages: 711
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  hii habari imekosa nguvu ya ushawishi. tena sioni kama mleta habari alihitaji kuileta jamnvini. nadhani huyo dada kama kweli alitaka kutoa mimba asingekwenda kuomba pesa ya kutolea mimba- angeweza hata kudanganya shida nyingine kwa mtoa maada, apate pesa, ili mimba itoke. pili huyu dada wakati anatafuta ada ya mtoto hakuwai kumfuata mtoa maada na kuomba pesa ya ada? au kama si ada basi hata kutaka ushauri wa nani wa kumkopa???. miaka 33, unamfuata mwanaume ambaye unasemaanakutongoza humtaki- kwanini umfuate ukiwa na shida?? ktk mazingira haya, kipi raisi kuomba ada kwa mtoa maada au kuombapesa ya kutoa mimba???.tena dada ana shughuli zake ndogondogo ktk hizo shughuli hakuna watu wengine anawajua isipokuwa huyo mwanamme?? nadhani kwanza kabisa dada asingekwenda kukopa kwa mtu ambae walitofautiana ki-msimamo. kama ni kweli basi kuna cha kujifunza kuoka kwa huyo mama.
   
 15. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #15
  Apr 1, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Aroo GS, swala sio tu kutoa mimba ni hatari kwa afya yake, bali ni uvunjifu wa sheria ya Tanzania.
  Mwambie hata asipojali afya yake kwa kuitoa hiyo mimba lakini mkono wa sheria upo pale pale, atawajibishwa.
  Nipe details zake ili nihakikishe sheria ya nchi inafuatwa.
   
 16. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #16
  Apr 1, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 546
  Trophy Points: 280
  Usiue - Amri kuu ya mungu
  Mwambie huyu mpendwa kuua ni dhambi na pia ni hatari kwa maisha ya huyo Binti.sio kwanba ndio mwisho wa maisha ya binti anaweza kujifungua na kuendelea na masomo yake
  All the best
   
 17. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #17
  Apr 1, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 546
  Trophy Points: 280
  Kweli Gaijin
  hata mie naweza kupewa huyo mtoto nikamtunza kama mwanangu ..GS mwambie huyo binti ajifungue anigawie mtoto..ruksa kuja kumsalimia
   
 18. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #18
  Apr 1, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  hivi watu wanafanyaje mapenzi jamani bila kufikiria mara mbili mbili? li mtu umekutana nalo tu hata kinga hamtumii?jamani matatizo mengine ni ya kujitakia kabisaaaa.
   
 19. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #19
  Apr 1, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  huyu dada hakwenda kumkopa mkaka, bali alienda kufanya na wamalizane kifedha lakini mkaka akamwacha solemba, ndivyo nilivyoelewa.
   
 20. m

  mnyakyusa JF-Expert Member

  #20
  Apr 1, 2010
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 248
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Msaidie tu huyo dada kwa kumsomeshea mtoto wake na mshauri madhara ya kutoa mimba pia
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...