Anapenda kujichanganya na wanaume.... Ushauri plz!

Mwana JF

Member
Jul 27, 2012
26
1
Habari zenu jamani?
Mimi nina mpenzi wangu ambaye nampenda sana na yeye ananipenda sana (kwa mujibu wa mdomo wake)
Sasa tatizo ni kwamba anapenda sana kukaa na kupiga story na wanaume.
Niliwahi kumwambia kuwa sipendi tabia hiyo na akaniahidi ataiacha.
Sasa juzi nilimkuta kwa macho yangu akiwa amekaa na wanaume watano huku mtoto wa kike akiwa peke yake wakipiga story. Hivi jamani mi nimuelewaje mtu huyu? Kweli ni sawa kwa mtoto wa kike kupenda kujichanganya na wanaume kiasi hiko. Hebu nishaurini maana hapa nilipo nafikiria kumuacha japo ameniahidi hatorudia tena.
 
mfanyie 'background check'; it is possible katika makuzi yake ametokea ku-interact zaidi na wavulana kuliko wasichana wenzake, which might not necessarily be a bad thing
 
Si tatizo sana! Lakini kama hakuna jambo baya! Wanawake wa namna hiyo siku hizi ni wengi na ukijaribu kuwa uliza wana sababu za msingi za kufanya hivyo!

Ila kwa sababu ali kuahidi kuacha ni vizuri ukajaribu kuongea nae tena kuhusu ahadi yake.
Pia jaribu kupunguza wivu!
 
Mi sioni kama kuna tatizo lolote hapo.. Angekuwa anapenda kukaa na mwanaume mmoja hapo ungehisi vibaya.. Huwezi jua anaona ni afadhali apige stori na ma men kuliko kukaa na wadada ambao muda mwingi ni umbea tuu.. Usimuache, nenda nae taratibu nahakika mwisho wa siku atakuelewa tuu..
 
jenga urafiki wa muda mfupi kati ya wale alio kuwa nao ili upate habari kama kuna anae mchukua utajua fasta tun :A S 465:
 
Una bahati sana, mwanamke anayekaa sana na wanaume huwa anawafahamu zaidi wanaume. Atajua mahitaji yako, furaha yako na hata kero zako kiurahisi. Binafsi na enjoy sana mtu wa namna hii.
 
na wewe hakikisha unajichanganya nae
wadada wa hivyo wanapenda mwanaume ambae
ana 'heshimiwa' na hao marafiki zake vidume

ukizubaa tu inakula kwako
 
Huyo anayekaa kwenye vijiwe vya wanaume ni Tom Boy...angalia tu asije kuwa lesbian. Kuna dada tulisoma nae primary. Ukimuangalia naweza sema she was the most beautiful...lakini company yake ilikuwa wanaume tu hata anavyoongea ni kibabe babe...kucheza anacheza fotball...lakini wale wanaume walikuja kumchukia baada ya kugundua anatoka na wasichana wao...alikuwa lesbiana miaka hiyo ya late 80s. Hakuwahi kuwa na boyfriend mpaka tunapotezana. Sijuhi kama alikuja olewa au alioa au yupo yupo.

Kama ni Tom Boy na si lesbian basi huna haja ya kuwa na pressure hawanaga tabia ya kuchukuliwa na guy friends wao. Ila Tom boys wana mambo ya kiume sana hivyo duuu, ngumu kweli kuwa nao. Kama si Tom Boy, mwanawane utakuwa unasaidiwa kwani lazima kuna usumaku kati ya jinsia hizi mbili.
 
Na hao wanaume anawakusanyia wapi...I mean wanakutana wapi? Kwenye bar au bado ni mwanafunzi?

Naelewa ni fahari kwa kila mwanaume kuwa na private girlfriend...hakuna cha wivu wala nini she should stop or else....
 
Wasichana wa dizani hiyo ni wazuri sana katika mahusiano kwa sababu wanakuwa wanazijua tabia za wanaume na hivyo haiwapi shida kufanya maamuzi pale mwanaume anapojipendekeza/kumtongoza wakati anajua ana bf. Kwa kuwa hawajichanganyi na wadada kihivyo wanakuwa hanana muda wa kumaindi vt vidogodogo ambavyo huwa mwiba ktk mahusiano.
Usimkataze kuwa katika company ya wanaume bali angalia aina ya wanaume ukiona c wema mwambie kwani ni bora kuwa nacompany ya wanaume kuliko wanawake.
 
  • Thanks
Reactions: LD
Huyo anayekaa kwenye vijiwe vya wanaume ni Tom Boy...angalia tu asije kuwa lesbian. Kuna dada tulisoma nae primary. Ukimuangalia naweza sema she was the most beautiful...lakini company yake ilikuwa wanaume tu hata anavyoongea ni kibabe babe...kucheza anacheza fotball...lakini wale wanaume walikuja kumchukia baada ya kugundua anatoka na wasichana wao...alikuwa lesbiana miaka hiyo ya late 80s. Hakuwahi kuwa na boyfriend mpaka tunapotezana. Sijuhi kama alikuja olewa au alioa au yupo yupo.

Kama ni Tom Boy na si lesbian basi huna haja ya kuwa na pressure hawanaga tabia ya kuchukuliwa na guy friends wao. Ila Tom boys wana mambo ya kiume sana hivyo duuu, ngumu kweli kuwa nao. Kama si Tom Boy, mwanawane utakuwa unasaidiwa kwani lazima kuna usumaku kati ya jinsia hizi mbili.

we hukuwahi kuwa Tom boy?
 
Sioni sababu ndio akae nao, mimi kwetu tumezaliwa 10 na 9 wote ni wanaume wakike peke yangu na kwetu kulikua hakwishi wanaume rafiki wa kaka zangu lakini haikua sababu ya mie kukaanao na ukikaa baribu yao utaipata habari yako.
 
The Boss, binti anayetokea BK analelewa kutambua kuwa ni mwiko kukaa na wanaume hata kama ni kaka zake. Lol. Mwanamke analelewa kuwa na tabia za kike...siyo kuweka mguu juu ya meza. Sitanii mama yetu alikuwa mkali sana kwa hilo...ingawa baada ya kukua ndio nikajua ni mfumo dume...ila imenifanya niwe na tabia za kike ambazo sioni kama ni mbaya kwani sijawahi kumkwaza nimpendaye.

Unaweza kucheka lakini mimi mfano siwezi kupiga mluzi kwani toka nikiwa mdogo niliambiwa ni mwiko...ingawa nimezaliwa na kukulia Dar.

Sina watoto wa kike ila ningekuwa nao nadhani ningewalea kama nilivyolelewa mimi, hakuna kumanua manua mtoto wa kike unajikusanya wakati wa kukaa...na mengi mengineyo.

wanawake wa Bukoba muweke miguu juu ya meza
sipati picha lol
 
Huwezi jua anaona ni afadhali apige stori na ma men kuliko kukaa na wadada ambao muda mwingi ni umbea tuu..

afadhali umesema mwenyewe neylu maana angesema mwanaume hapa kwamba watoto wa kike ni wambeya kungechimbika....
 
Last edited by a moderator:
Hiyo ingekuwa sawa nzuri...tit for tat...ila unadhani ni rahisi kuzungukwa na watoto wa kike kama si tabia yako? Je anaweza kuamua over night kuwa kuanzia leo ntakuwa nazungukwa na wadada?

Ila akiweza ndio itakuwa njia ya kunyooshana.

Na wewe hakikisha pia unajichanganya na wanawake wa kutosha.
 
Back
Top Bottom