Anaomba ushauri, Je amuache?

Candela

Member
Aug 12, 2021
77
150
Habari wadau. Kuna mtu wangu wa karibu amenifuata akitaka ushauri juu ya mahusiano yake. Anajiuliza kama anaweza kumuacha mpenzi wake au aendelee nae.

Anasema alikutana na huyu binti miaka miwili iliyopita, wakati akimtongoza binti alisema anataka mtu siriaz amechoka kuchezewa ndio maana ameamua kukaa singo. Jamaa akakomaa mpaka akampata huyu binti lakini ndani ya miezi miwili ya mahusiano yao akabaini binti ana mahusiano na wanaume wengine wawili kwa takribani miaka 3 na mwingine miaka 5.

Anasema aliamua kukaa kimya kwa kuamini kama binti ameamua kuwa nae basi huenda hana mpango na hao jamaa labda hakupata tu mtu ataekuwa karibu.( hao jamaa wote ni waume za watu). Kwa imani hiyo jamaa akavumilia kuwa nae karibu huyu binti mpaka siku 1 alipomuaga anaenda kusalimia ndugu lakini kumbe alienda kwa mwanaume mwingine. akalala huko siku 2 kisha akarudi kwa jamaa.

Licha ya jamaa kugundua ukweli na mpaka aliongea na jamaa kwa simu alipoipokea simu ya binti wakati alipompigia saa 8 za usiku, bado hakuweza kumuacha, aliendelea nae. Kwa sasa anadai binti amesafiri tena kaenda kwa jamaa wa mwingine na amejaribu kumuuliza anaenda wapi anasema majibu hayamridhishi kabisa, binti anadai akifika anakoenda atamwambia lakini tangu amesafiri simu haipatikani tena.

Anasema anavumilia sana ameshindwa aamue nini kwani binti amwemwambia ana ujauzito wake hivyo anajikuta njia panda kumkataa asije sema kaikataa mimba.

Binafsi nimekosa cha kumshauri nimeona niwadondoshee wadau hapa tupate mitazamo tofauti.

Nawasilisha.
 

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
20,197
2,000
Jamaa kapenda kweli.. haya ndo mapenzi uchizi sasa!

Mkuu we kwa kuangalia tu jamaa kapigwa hayo matukio yote lakini hajaacha unafikiri wewe kumshauri aache ataacha kweli..?

Nikupe jibu la hekima kabisa kamwambie hivi muda utakapofika sahihi na hisia zake zikipunguka kwa huyo binti kutokana na matukio yake,na akawa radhi kumuacha kutoka ktk akili yake na hisia zake basi huo ndo utakuwa muda sahihi kumuacha maana atakuwa ameamua ndani yake bila kuhitaji ushauri.

Kwa kipindi ambacho atakuwa anaendelea nae mwambie ajihadhari na magonjwa.
 

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
5,894
2,000
Mimi hata sijasoma chochote ulichoandika ila nashauri ampige chini aachane naye, ukianza kuona unawaza sijui nimuache we muache tu msipotezeane muda!
 

Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
48,541
2,000
Habari wadau. Kuna mtu wangu wa karibu amenifuata akitaka ushauri juu ya mahusiano yake. Anajiuliza kama anaweza kumuacha mpenzi wake au aendelee nae.

Anasema alikutana na huyu binti miaka miwili iliyopita, wakati akimtongoza binti alisema anataka mtu siriaz amechoka kuchezewa ndio maana

Nawasilisha.
Kikubwa ni rafiki yako kwenda kupima afya ya akili yake kwanza kabla hatujaelekea kwenye mashauri
 

Lihove2

JF-Expert Member
Mar 23, 2018
2,628
2,000
Habari wadau. Kuna mtu wangu wa karibu amenifuata akitaka ushauri juu ya mahusiano yake. Anajiuliza kama anaweza kumuacha mpenzi wake au aendelee nae.

Anasema alikutana na huyu binti miaka miwili iliyopita, wakati akimtongoza binti alisema anataka mtu siriaz amechoka kuchezewa ndio maana
Mwanamke alitaka mtu serious, so mwambie jamaa anazo sifa hizo, aendelee kuwa serious tu mpaka kifo kimkute. Upumbavu mtupu! Mungu asaidie kufungua fahamu za wanaume wenzangu wa aina hii
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom