Anaomba second chance

Anaomba second chance

dudu linalouma hilo ..waruhusu vipi kulipa kidole..huyo mambo yke yamemchachia bab..ndio maana karejesha majeshi kwake ..ila akipata mwingine wakumzuzua tarajia kuumizwa tena..

ijapokuwa mimi mwenyew niweke wazi ..huwaga sinaga desturi yakuwavimbia ma ex wangu ..akileta papuchi nakula mzigo but namla huku akitambua kuwa hatuna future yoyote between us..yaani ni for sex only..
 
MZUMBE BINTI ANAWEZA KWENDA NA TABIA NZURI, ATAMUDU MWAKA WA KWANZA ILA MWAKA WA PILI WACHACHE SANA WATAVUKA NA TABIA ZAO, NADHANI HII NI VYUO VYOTE.

NI WAZI ALIPATA KIHANDSOME BOY HUKO MU, LAKN PIA KUHUSU KUOMBA VITU VIKUBWA ILITOKANA NA KUNDI LA MARAFK ALIOKUWA NAO.

SWALI: JE, AMEPATA KAZ? ISJE KUWA ANAKUJA KUPATA UNAFUU WA MAISHA KWAKO HALAFU BAADAYE AKPATA KIBARUA AANZE JEURI TENA.

KUHUSU KUMRUDIA MKUU KAMA NINGEKUWA MIMI NINGEMRUDIA KWA LENGO LA KUPOTEZA NAYE MUDA TU NA SYO KUOA, ILA CHANGANYA ZAKO.

KILA LA HERI..
 
Mkuu kwanza pole kubwa sana kwako kwani najua machungu ya namna hiyo yapoje. Nilishawahi kuwa na hali kama yako kwa mrembo niliyekuwa naye kwa miaka minne na alinipiga nondo ya kichwa tulivyokuwa vyuo tofauti.

Mkuu utasikia maneno yenye chuki kali kwa huyo binti kutoka kwa wachangiaji mbalimbali lakini lisikushtue hilo kwani kwangu wanafamilia walimchukia mrembo tuliyeachana kuliko hata mimi nilivyomchukulia.

Nakushauri kuwa kabla ya yote msamehe. Msamaha ni agizo la Mungu kwani hakuna yeyote asiye na kosa. Pili tambua kuwa MSAMAHA NI TOFAUTI NA KURUDIANA. Ni lazima kumsamehe ila si lazima kurudiana. Ili kurudiana hapo ndipo wahitaji kujitafakari na mtafakari pamoja.

Nakushauri zaidi umsikilize na umuambie aeleze bayana je, yale yaliyomfanya akuache ni yapi na anayaonaje kwa sasa? Na zaidi ana tathmini vipi tabia aliyokutendea na anajua ni madhara gani amekuacha nayo muda wote huo. Je tabia aliyokuonyesha mpaka mkaachana kafanya juhudi gani kuirekebisha na ni nini kimemsukuma kutaka mrudiane?

Mheshimiwa kila mtu katika utetezi ni rahisi kuweka maneno kama 'shetani alinipitia', 'ulikuwa utoto' na hata mara nyingine kutoa machozi. Hizi ni sababu nyepesi mno kwa watu kurudiana akupe sababu zenye maana na zinazoendana na malengo yako.

Furthermore, epuka kurudiana naye kama una mpenzi mwingine uliyemchagua na kumpa maneno matamu akakubali kuwa nawe. Usifikirie hata wazo la kumuacha. Pia, usirudiane naye ili tu ulipize kisasi utakuwa umeharibu mema yote mliyojitengenezea na utajishusha mno thamani yako mbele ya Mungu na wanadamu. Usiingie naye kwenye kurasa mpya bila kusamehe na kumuamini na kuchukulia yaliyopita kama darasa.

Mwisho, mpe muda ajifikirie na kama ana nia utamjua. Ni rahisi sana kwa aliyetendwa kumkumbuka yule yeye aliyemtenda kwa kudhani alimlaani na kutaka kurudi kufarijiwa. Usiharakishe mrudiane kama unataka hivyo. Muache apoe na umuambie ukweli kuwa unampa muda wa miezi kadhaa ama utakavyopenda wewe. Akisahau yaliyompata utaona huo muda ukipita dalili kuwa anamaanisha. Usiruhusu kutaka kufanya naye mapenzi haraka haraka kwani utapofushwa na hutatumia tena kichwa kikubwa kutoa maamuzi. Kuwa muwazi na msimamo wako kama ni YES au NO ukijifanya mwanadiplomasia mtapotezeana muda na anguko la pili litakuwa baya kuliko la kwanza.

ONYO! Nimeandika uzi mrefu tofauti na kawaida yangu nikiamini uzoefu wangu katika hilo utakusaidia. Soma kwa makini na usiyapoteze haya madini. Kila la kheri.
 
Claret ameandika vyema sana. Nami nimalizie kwa mifano;

Mfano 1: Kaka yangu kabla hajaoa alikuwa na rafiki wa kike waliyependana sana kwa takribani mwaka mmoja. Aliamini binti alikuwa akimpenda lakini kuna jambo moyoni mwake lilimnyima amani juu ya huyo binti na hata alipoliwasilisha kwake walishindwa kukubaliana. Baada ya tafakuri na maumivu mengi alifanya maamuzi magumu ya kumaliza uhusiano ule kwa kuamini kila mmoja alistahili kuwa na amani kwenye uhusiano. Hakuwa binti mbaya, hakumkosea chochote.
alijisemea moyoni, atajipa muda akae peke yake na binti akae peke yake kila mmoja ajitafakari. Ikitokea akampata binti mwingine vyema, ataendelea na maisha. Ikitokea baada ya mwaka mmoja atakuwa peke yake, basi atamtafuta yule dada. Miezi tisa baadaye walikutana na katika kuongea hakuna hata mmoja wao aliyekuwa amedate mwingine (at least kwa kaka yangu ilikuwa hivyo). Wakazungumza na kugundua kumbe binti alishabadili kile walichokuwa wameshindwana mwanzoni. akaomba msamaha, akatangaza nia na juzi December walijaliwa mtoto wao wa pili.

Mfano wa 2: Kuna mzee mmoja kanisani ninapoenda alikuwa ameoa mke wake. Baada ya kutokuelewana katika ndoa yao kwa muda mrefu wakaachana. Kila mmoja akaenda kwa mwingine na kila mmoja akapata mtoto huko. Baada ya miaka 30, wamerudiana na kuoana tena. Wanatuaminisha wana furaha lakini kila nikienda kwao naona misuguano hasa kutoka kwa huyu mama. Hampendi mtoto wa huyo baba. Naona kama wanavumiliana tu.

Mfano wa 3: Nilimpenda binti. Akaniacha. Baada ya miezi akarudi. Nikampokea. Akaniacha tena. Alirudi baada ya miezi sita hivi akitaka kurudi. Katika kumuuliza akaniambia alikuwa kwenye uhusiano mwingine (uliofanya aniache) ila ameona ananipenda, ni tamaa na umbali kati yetu vilichangia. Nikasema asante nashukuru ila sina nafasi tena. Na huyu alijua nilikuwa ninampenda.

Niilikumbuka wimbo wa Crystal Gayle - Why have You Left the One You Left Me For.




Kwa ufupi, hakuna sheria kwenye mahusiano. Lakini kama unaamini haukuandikiwa mtu mmoja tu, basi piga moyo konde usonge mbele. Kama unaamini anaweza kuwa exception basi ushauri wangu ni muanze moja...kama marafiki, bila ahadi zozote. Usiwe na haraka maana najua una hisia naye bado, wewe ndo utakayeumia zaidi. Hakuna rafiki mzuri kama muda!

Kila la kheri mdogo wangu..usisahau kumuuliza kwanini amemuacha aliyekuacha kwa ajili yako!
 
Sijui kwa wewe.ila Mimi uwa siwezi Niki delete naformat kabisaa.na nikishamchukia demu uwa siji kumpenda tena..
Akija kuomba msamaha nitamtesa tu.sintompenda kama mwanzo.
 
Muda wote huo wewe bado uko single? maamuzi ya mwisho unayo wewe mwenyewe.
 
Muda wote huo wewe bado uko single? maamuzi ya mwisho unayo wewe mwenyewe.
 
Mkubali tu lakini jiandae kusumbuliwa kwa mara ya pili au atakaa kwako jumla.

Ni kubet hapo.
 
Amani ya Bwana iwe nanyi enyi watu wa Mungu!
basi tukiwa bado tunatafakari kauli ya mheshimiwa Trump kuhusu bara la Africa na watu wake,ningependa kushare nanyi huu mkasa wangu.
ways back kama miaka minne iliyopita,nilikua nadate binti flani hivi ambae kwa kipindi hicho ndio alikua kamaliza form six,well naweza kukiri mwanzo alionyesha mapenzi ya hali ya juu sana kwangu mpaka nikawa nishamwekea malengo ya kumuoa..akachaguliwa kwenda chuo huko mzumbe na mapenzi yalizidi kunoga mpaka anaingia mwaka wa pili ndio mambo yakaanza kuchange..ikafikia point kila jema nililokua namfanyia kwake ilikua kero,akaanza kuniomba vitu ambavyo kwa wakati huo mimi sikuweza kuvimudu asee..baada ya kumfanyia intelijensia kwa mara ya kwanza sikugundua kitu chochote,nikabadili mbinu za kumspy sikugundua kitu pia na wakati huo huo ndio vituko vyake ndio vikawa vinazidi...so kama ilivyo ada kwangu mie sinaga muda wa kupigizana kelele na wanawake au kubembelezana na binadamu mwenzangu..nikaamua kumchunia tu yule manzi,nae bahati nzuri akaamua kuuchuna..sasa cha kushangaza leo kaanza kunitafuta kwa fujo..kanipigia tumeongea mengi ananiambia eti sababu za kipindi kile kuwa vile ulikua ni utoto unamsumbua so kaniomba msamaha na anaomba nimpe second chance katika maisha yake ili tuweze kuendeleza pale tulipoishia.
Nimemtafakari sana leo,ofcourse naelewa huko alikokua atakua katendwa so kaamua kuja kujificha kwa boya wake(mimi) lakini pia nimefanya cost benefit analysis nimeangalia mazuri yake aliyonitendea ni mengi kuliko mabaya hivyo uwezekanao wa kupewa hiyo second chance upo,but kabla sijatoa go ahead ya mawazo yangu nikaamua niwashirikishe na nyie watu Mungu ili nisikie mnatoa mawazo gani hapa.
Asanteni
NB; ukijisikia kutukana wewe tukana tu maana Tnzania ni nchi huru but nakuonya you are not free to that extent,Mods wako kazini muda wote.
Ni vizuri ukimsamehe kama mistkake imefanyika mara moja, lakin lazma ujihakik mwenyewe kuwa huna mtu mwingine kwa sasa na endapo muda wako unaruhusu,,,, maana unaweza poteza muda mara ya pili tena, and time can't be paid back.. good wish
 
uzur wa wanaume hatuna expire date hata ukitaka ucheze uje kuoa na miaka 60 ni ww tu co kama wao wakifika 25 tu wanaanza kuhofia maisha
 
Back
Top Bottom