Undugu wetu, uendelee tu kukutana kipindi cha misiba tu?

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
39,320
Reaction score
60,506
Ni wachache sana waliofanikiwa kushikamana kwenye biashara kwa wanandugu, hasa sisi kizazi cha kiafrika aka ‘black mamba’.

Kumekuwa na dhana, mmoja au zaidi katika familia anaweza kuona fursa na kuifanyia kazi na baadaye kuwashirikisha ndugu na jamaa, ili wajumuike naye katika hiyo biashara ili wote kwa pamoja waweze kukua kiuchumi.

Changamoto zimekuwa ni nyingi, badala ya kutimiza ndoto ya mafanikio kumekuwa na maporomoko.

Tatizo litakuwa ni nini?

Au undugu wetu, uendelee tu kukutana kipindi cha misiba tu?​
 
Kunaepusha mambo mengi sana, ndugu wakizidiana mafanikio ni maneno maneno tu, fitina, uchonganisha na uchawi! Kwahiyo kuyaepuka hayo yote bora iwe hivyo!
Na hii ni kwa waafrika tu, au mpaka kwa hawa wenzetu?
 
Hapo kwenye biashara nahisi ni kutokana na kiwango kidogo cha elimu au ujuzi Miongoni mwa wanafamilia au ukoo

Hili linasababisha hata ukitaka kuwapa ndugu zako vitengo mwishoni wataharibu tu na biashara kuisha au kushuka

Na ukiwapa vitengo vinavyoendana na level zao watabaki kulalamika kuwa unawatesa na. Mengine mengi
 
Wenzetu wana maendeleo makubwa, hawakutani hovyo bila mialiko hata misiba ina mialiko, wana mipaka na wanaheshimiana sasa haya mambo yana nafasi ndogo sana kwao!
Umeeleweka, tuendelee kukutana kwenye misiba tu.
 
Wenzetu wana maendeleo makubwa, hawakutani hovyo bila mialiko hata misiba ina mialiko, wana mipaka na wanaheshimiana sasa haya mambo yana nafasi ndogo sana kwao!
Kwenye misiba pia ni eneo la watu kujua nani kajipata na nani bado ni mnywa maji ya kandoro.

Wengine ndo huanza kupiga simu wapi watampa mtaalamu ili kushughulikia wewe mwenye maendeleo kuliko wao.
 
Hapo kwenye biashara nahisi ni kutokana na kiwango kidogo cha elimu au ujuzi Miongoni mwa wanafamilia au ukoo

Hili linasababisha hata ukitaka kuwapa ndugu zako vitengo mwishoni wataharibu tu na biashara kuisha au kushuka

Na ukiwapa vitengo vinavyoendana na level zao watabaki kulalamika kuwa unawatesa na. Mengine mengi
Tatizo linaweza kuwa ni elimu zetu au ni asili tu tulio zaliwa nayo?
 
Kwenye misiba pia ni eneo la watu kujua nani kajipata na nani bado ni mnywa maji ya kandoro.

Wengine ndo huanza kupiga simu wapi watampa mtaalamu ili kushughulikia wewe mwenye maendeleo kuliko wao.
Ndio maana kuna watu wanasafiri kuwahi mazishi tu wakishazika wanageuza ukilala msibani ni kuwa kama upo au haupo ukijifanya unapenda engagement sana na wanandugu yatakukuta uendako!
 
Kwenye misiba pia ni eneo la watu kujua nani kajipata na nani bado ni mnywa maji ya kandoro.

Wengine ndo huanza kupiga simu wapi watampa mtaalamu ili kushughulikia wewe mwenye maendeleo kuliko wao.
Inasikitisha sana, tatizo linakuwa ni nini?
 
Tatizo linaweza kuwa ni elimu zetu au ni asili tu tulio zaliwa nayo?
Yote yanaweza kuchangia mkuu ila kukosa elimu au ujuzi Unaweza kusababisha hili suala la kushindwa kuleta maendeleo ya pamoja kama familia

Ila Hilo la asili pia ni tatizo bado tuna roho za kwanini
 
Back
Top Bottom