Ananipima au hanitaki?

Kwa hiyo akitangulia mtoto then ndoa ndio itadumu milele?

Suala siyo kutangulia mtoto, jamaa anaonekana hajajipanganga kwa hizo sherehe zenu za mashela. Wakae chini wakubaliane, wakatambulishane kwa wazazi, mahali itolewe waendelee na maisha. Hayo mengine watajipanga baadaye. Ndoa ni makubaliano ya watu wawili wakipewa na baraka za wazazi! Kuna ndoa ya kidini, kiserikali na kimila. Kidini ni ile inayohusisha wachungaji,mashehe na mapadri, ya kimila mnamaliza kila kitu nyumbani na ya kiserikali mnaenda kwa mtu wa viapo bomani. Mara nyingi ya kidini huwa inaunganishwa na ya kiserikali ndo maana vinatolewa vyeti vitatu. Sasa kama jamaa hiyo sherehe ya mashela haiwezi na we una hamu ya mume, chagua kitu ambacho ni simple. Ndio maana kukawa na kubariki ndoa na siku hizi wamerahisisha kuna ndoa za jumuia aafu zinagharamiwa na kanisa. Tatizo lenu mnataka sherehe na sio ndoa.
 
Yaani unataka hadi akutamkie kabisa kuwa HAKUTAKI?
 
A lot lies untold in this episode...cant comment!
 

Dah! Sister hapo ni kama hakuna mwoaji! Na kama ni mwoaji kweli,basi bado anamatatizo kdg ktk mtazamo wake wa kuwa na uhakika na wewe km unauwezo wa kuzaa! Kaa naye umshauri kuwa suala la kuzaa ni Mungu ndio anahusika.Asipoeleweka achana naye na umwombe Mungu akupe mume wako,huyo atakuwa si wako!
 

Kama kweli tatizo ni kujipanga kwa sherehe,hapaswi kuwa mkali na ku demand mtoto badala yake aongee na mwenzi wake watakubaliana. Katika aina zote za ndoa ulizotaja hakuna hata moja ambayo jamaa ame opt,yeye kaja na yake mapyaa ya kutaka mtoto kwanza ndoa itakuja tu!
Aseme kama tatizo ukata ataeleweka watafunga wanayo afford.
 
haya ni yale ya kuku na yai kipi kinatangulia,yai ama kifaranga mtoto au ndoa,mie mwenzako nina mareserve nikiona huyu hafai naenda plan B :shocked::shocked::shocked::shocked:,hawakosekani hawa kama umekamilika lol kuwa na amani utampata wako na uombe mungu akuonyeshe njia kwa hili
 

Ukweli unaufahamu, wadada wa siku hizi wanatafuta sherehe ya harusi kuliko ndoa. Yawezekana jamaa amekerwa na kila siku kuôngelewa mambo ya mashela!! Seriously, hata mimi nikiona maongezi yako yametawaliwa na sherehe za harusi kuliko maendeleo nasepa. Mara sijui x alipendeza hivi, y sherehe yake siku fulani! Yananihusu? Na wengine wanatuomba na hela kabisa wakachangie harusi! Nikutoe out, hela ya kusuka, pads, nguo, viatu mpaka mchango wa harusi!!
 

inaelkea mbahili ukute hutoi ht hio hela mmmnh:shocked::shocked::shocked:
 
inaelkea mbahili ukute hutoi ht hio hela mmmnh:shocked::shocked::shocked:

Material things sounds more than môney. Nakununulia nakuletea mechi inapokaribia na wekundu wa msimbazi. Usiniulize nilizijuaje anazozipendelea.
 
kimbiaaaaaaaaa

Atakimbiaje na yeye anajiona ameshazeeka? Yewezekana hakuna wengine wa kuingia kwenye nyavu zake ni huyo tu! Wengine wote wameshaoa. Chezea wadada wanaoringa wakiwa chuo wewe! Wakishakuja kazini ndio wanaanza kujutia zile nafasi.
 
huyo hajajitambua bado anatakiwa apewe elimu kuhusu nn maana ya ndoa
 
pole bidada kama vipi tangaza nia humu jamvin waoaji kibao mwenzio debora kashajipatia wake humu humu
 
Hadithi za namna hii zinaniuma aisee, miaka 30 akiondoka huyo itakuwa ngumu kumpata mwenye nia hasa ya kukuoa.

Najua unapenda ndoa, shela na harusi.. tena inawezekana unataka harusi ya kifahari, je unaijua hali ya kifedha ya mchumba wako? Kama ana uwezo wa kulipa mahari mkatambulika na wazazi, mimi naona mnaweza kuendelea, sherehe zitakuja baadae... ukimzalia ukiwa kwenu hatakuoa huyo!
 

Uhusiano wetu una miezi sita. Sitaki sherehe kubwa.
 
May b anahis wewe ni mgumba so anataka atest kama vipuri viko vizuri. mdanganye mwambie umeconsiv uone atasema nin
 
ndoa si kitu cha kulazimisha wala kuwekea dhamana maana waweza lazimisha ndoa na bado isidumu sasa sijui hapo utashangilia kuvaa shela au kuolewa.. cha msingi angalia umeweza kudumu kimahusiano muda gani na je nini moyo wako unataka na ongea nae taratibu kwa kupanga vitu vya mbele kuliko kuweka ndoa kama amana
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…