Ananipenda lakini chamoto nakiona

Ananipenda lakini chamoto nakiona

Sir Sule

Member
Joined
Jul 13, 2015
Posts
27
Reaction score
13
Mpenzi wangu ambae siku zote namuamini sana kwa zaidi ya miaka minne sasa lakini cha ajabu anapenda sana kuninunia haswa ikitokea tumepishana kiswahili nimejaribu kumkataza tabia yake hii lakini hukaa kwa mda anarudia tena yaani anaweza kukaa hata wiki moja hanipigii simu na simu yangu hapokei.

Nimejaribu kumchunguza kwa mbinu zote ili niweze kujua anamwengne au vipi lakini sijagundua nikaenda hadi kwa wanaoona kwa maono yasiyo ya kawaida lakini wameniambia ni tabia yake tu.

Lakini hana mwanaume mwingine na anakupenda sana, sasa nabaki kijiuliza ni kitu gani kinachomfanya apate ujasiri wa kunipigia kimya wiki nzima wakati tupo mikoa tofauti hua tunakutana mara chache tu.
 
Una kazi wewe kumchungaza mwanamke haaaaaa pole yako muombe mungu tu akupatie mke mwema maana unajiumiza bure
 
Mmmh hua namchunguza ili nipate pa kuanzia coz nachishwa na haka katabia kake ...
 
...nkaenda hadi kwa wanaoona kwa maono yasiyo ya kawaida lakin wamenambia ni tabia yake tu lakin hana mwanaume mwngne na anakupnda sana..sasa nabaki kijiuliza ni kitu gani kinachomfanya apate ujasiri wa kunipigia kimya wiki nzma wakati tupo mikoa tofaut hua tunakutana mara chache tu....

Hahahahaha!

Sema ukaenda kwa wachawi maana na we ni mchawi!!
 
Watu wengine wanavyopenda kutapeliwa fedha zao na waganga, sasa huyo wichidokta anamfahamu vipi huyo gf wako au ulikwenda nae?

Nilidhani elimu imetukomboa kumbe bado kabisa.
 
Baada ya hiyo wiki nani ndo anaanza kumtafuta mwenzake??
 
sasa nabaki kijiuliza ni kitu gani kinachomfanya apate ujasiri wa kunipigia kimya wiki nzma wakati tupo mikoa tofaut hua tunakutana mara chache tu....


labda huwa humfikishi 'awamu ya 4' brother, ndio sasa anakuonyesha frustrations zake. Chunguza na hilo pia.
 
Uhusiano mrefu hivo mnatafuta nini hasa kama sio kutokana lawama tu!!? Mnasoma? Duuuuh!
Anakupenda ila anatongozwa pia ukumbuke hilo!

Halafu unasema unamchunguza ili upate pa kuanzia! !!!?

Kama umechoka mwambie tu! Miaka 4 halafu uje umpatie sababu umuache! ! ? Loh
 
Miaka minne bado unapuga mark time tu, siku ya siku utasikia mwenzio kachukuliwa jumla
 
Kama unaona kununa kwake ni kikwazo kwako basi hiyo ni sababu ya kuwa hakufai.
Tafuta ambaye atakufanya uwe comfotable.
 
Huyu jamaa ni mshirikina ase.unaonekana unawaamini sana wachawi.sasa kwanini hujamloga asiwe anakununia?
 
Miaka minne!,atakuwa kidato cha nne huyu anafanya mtihani,mpe cheti chake
 
Huyu jamaa ni mshirikina ase.unaonekana unawaamini sana wachawi.sasa kwanini hujamloga asiwe anakununia?


kuna watu akipata msichana mpya anaenda kwa mganga kumuuliza je atanifaa?
mshahara ukiisha kabla ya mda anaenda kwa mganga
 
Back
Top Bottom