Analazimisha kunioa

Analazimisha kunioa

Huyo ikibidi ntamdedisha tu. Sio kikwazo kwangu kabisa kwenye ndoa yetu changa. Nakupenda sana mume wangu mtarajiwa. Mahari ntajitolea
😂😂😂😂🙌
 
Miaka 28 bado hujazaa? Unasubiri yale mabonge (mayai) yaote kwenye mirija ya uzazi ndio uamke kuhangaika kwamba hautozaa? Zaa nae huyo jamaa alafu endelea kumfikiria kuhusu ndoa, akisumbua achana nae baki single mama, ukijimix ukataka vyote utatuletea uzi mwingine humu
 
Miaka inaenda inarudi wanawake mpogo vile vile tu sijui kwanini, sijui akili zenu zinafanyaje kazi

Three years bado mtu unamtafakari tu, three years? it means since you was 25 up to 28 years old now? Bado unamtafakari tu? Hiyo ni bachelor in tafakaring au?

Ningekuwa mimi huyo mwanaume ningekuwa nishaoa au nishazaa na mwanamke mwingine afu nakusikilizia tu nakuchora

Anyway, swali likihitaji ujibu "YES" au "NO" afu ukawa hujui ujibu nini, basi jibu ni "NO" a big NOO
 
Utajuaje kama atakuwa baba bora wa familia ikiwa humpi nafasi ya kuwa mumeo.

Majukumu hubadili mtindo wa maisha, akishakuwa mume itamlazimu kubadili muenendo wa maisha yake. Sasa hivi anafanya starehe sababu bado ni bachelor.
Kama unampenda muweke chini umueleze hofu yako juu ya mwenendo wa maisha yake.

Katika swala la mapenzi ni bora kumpata anaekupenda na wewe unampenda kuliko kudengua sasa hivi uje kuangukia kwa baradhuli moja litakalokukoleza ulipende halafu likupiga matukio mpaka uwe chizi.

Bora ya huyo anaependa starehe unaemjua tayari kwa miaka 3 kuliko kuachana nae upate actor anaejifanya mlokole ukubali akuoe halafu uje kugundua ni mchepukaji.
Nakazia mkuu
 
Dalili ya mvua ni mawingu,kama unaona huelewi tabia zake sasa hivi mkimbie huyo akikuoa utasanda!
 
Utajuaje kama atakuwa baba bora wa familia ikiwa humpi nafasi ya kuwa mume kwanza?

Majukumu hubadili mtindo wa maisha, akishakuwa mume itamlazimu kubadili mwenendo wa maisha yake. Sasa hivi anafanya starehe sababu bado ni bachelor.
Kama unampenda muweke chini umueleze hofu yako juu ya mwenendo wa maisha yake uone kama hatobadilika.

Katika swala la mapenzi ni bora kumpata anaekupenda na wewe unampenda kuliko kudengua sasa hivi uje kuangukia kwa baradhuli moja litakalokukoleza ulipende halafu likupiga matukio mpaka uwe chizi.

Bora ya huyo anaependa starehe unaemjua tayari kwa miaka 3 kuliko kuachana nae upate actor anaejifanya mlokole ukubali akuoe halafu uje kugundua ni mchepukaji.
Fact
 
Habari za wakati huu wakuu

Niende moja kwa moja kwenye point, mimi ni binti wa miaka 28 nipo kitengo flan na mpenz wangu ana miaka 35 naye hivyo hivyo yupo kitengo flan. Sasa huyu mpenzi wangu nipo nae miaka mitatu sasa yeye alishanitambulisha kwao i mean ndugu zake wananifahamu. Mimi kwetu anamfahamu dada yangu tu,

Kiufupi nimeshindwa kumtambulisha kwani bado namtafakari tabia zake. Kwani ni mtu anayependa starehe sana (Hii labda inatokana na nature ya kazi yake) kiukweli ninavyomwangalia sioni kama ni mtu anayeweza kubeba majukumu kama baba wa familia, hii imepelekea mimi kusita sana kuolewa naye japo nampenda.

Wakubwa imefikia sehemu migogoro imekuwa mikubwa anataka anioe, nikamtambulishe nyumbani au nimzalie mtoto au tuachane. Nipo njia panda nina wiki sasa hatuongei nashindwa niamue nini nipeni ushauri wenu juu ya hili.

Ahsanteni
Moja,weye siyo binti.Mbili,kama hautaki kuolewa,acha kuutangazia umma upunyufu wako.
 
Uzuri hajajificha tabia zake hivyo maamuzi ni yako. Usidhan kuna binadamu asie na kasoro hayupo na hatokaa atokee. Mruhusu aje ajitambulishe akuoe au kama hutaki bado unasita muache usimpotezee huyo kaka muda.
 
Ni bora ukaamua moja,pia kama unaona hakufai we mteme tu.
Pia usiolewe ilimradi badae ukaanza majuto, maana ya uchumba ni kuangalia je huyu mtu ananifaa au hanifai.Ni heri ukae kwenye uchumba hata miaka tano lakini ujiridhishe kama huyu ananifaa na ntakuwa tayari kuishi naye kwenye maisha yaliyobaki.
Ndoa za siku hizi hazidumu kwa sababu ndogondogo tunazozipuuzia
Kama mtu at 35 hajitambui usitegemee jipya ukiamua kuolewa ujue huko tyari kwa lolote
 
Back
Top Bottom