markbusega
JF-Expert Member
- Oct 12, 2015
- 826
- 847
Ni mwezi huu nilipoamua kuwaokoa wadogo zangu wawili na ndoa za utotoni. Iko hivi:
Wakati nikifanya utaratibu wa kumwendeleza kielimu mdogo wangu wa miaka 14 wa kike aliyefeli la 7,kumbe baba alikuwa tayari ameamua aolewe ila anaunga mkono nia yangu kinafiki .akaja akinidanganya mama amekataa ati aolewe tu kuona hivyo
Ndipo niliamua kuwaokoa hawa wengine wawili miaka 10 na 12 wote wa kike kwa kuwahamishia nnakoishi kikazi
alikataa kugharamia hata mchakato wa nauli kwa ajili ya kufuatilia uhamisho wao maana mimi niko mbali kwa madai hana hela jambo ambalo sikweli nikagharamia mchakato wote wa uhamisho na nauli ya kuwaleta na kumrudisha aliyewaleta ukawa umegharimu laki tatu kuna dogo naye anasoma sec day gvt naye nikamrushia elfu 50 uniform n.k nilikuwa na akiba ya laki tano ikawa ndo hivyo tena.
Kinacho nifanye niandike ni leo asubuhi ananiomba laki mbili nimesema sina, anasema mshahara si umetoka? Nimemwambia bado haamini anataka nikakope hata kama haujatoka kwa kweli sina mpango wa kumpa maana nimemwambia mshahara huu unabajeti ya kodi ya nyumba mwezi huu analalamika eti nikioa ndio itakuwa zaidi ya hapa duh nimechoka sina hamu naye.
wadogo hawa watatu wananitegemea kwa kila kitu shule mavazi, malazi hadi matibabu lakini mzee haoni mchango wangu naombeni msaada wenu wadau jinsi ya kuishi na mzee wangu maana yeye anaamini mimi ni suluhisho la matatizo yake yote na changu chote ni chake nasipaswi kujipanga. kupiga simu naomba fedha ninunulie kiwanja chake shamba au nadaiawa kwake ni kawaida hajachoka kivile anang'ombe 20 mbuzi mashamba ekari 30 n.k nisiwachoshe nawasilisha.