Anahitaji ushauri

Anahitaji ushauri

Mimi naitwa Halima ni msichana wa miaka 19 Nasoma kidato cha tatu (form 3) hapa Arusha.... nimejitokeza kwenu kuomba ushauri
Mimi nina mpenzi wangu ambae yupo chuo kikuu, ana miaka 25... kutokana na upendo anaonionyesha sitamani tena kuendelea na shule... kwani nikiwa darasani muda wote namuwaza yeye tu
Nilicho penda kutoka kwa huyu BOYFRIEND wangu ni kua ananijali sana na ana pesa kwan kwao wanajiweza kifedha... ananionga sana PESA kwani nikitaka hela ya CHIPS KUKU hua ananipa, hela ya lotion, pafyumu na saloon hua ananipa kila mwezi kwahiyo sina shida na shule wala sioni umuhimu wa shule.
NAOMBENI ushauri wenu jamani.. niwaambie nini WAZAZI wangu ili wanikubalie niache SHULE ili niolewe na huyu MWANAUME nifaidi pesa zake na mali za nyumbani kwao

kwa vile umefika hapo ulipo, umechelewa kuacha we malizia tu ungejua ungeacha tangia shule ya msingi
 
We kilaza kwani unatakaje, lengo ni kufikisha ujumbe no matter habari imetoka wapi kuna wengine huko fb hawana habari napo

Sawa mimi kilaza wewe mwenye akili ushauri wako utamfikia mlengwa?? Angeleta kama habari sawa lakini kama kuomba ushauri huku yeye mwenyewe hawezi kufikisha ujumbe nahisi wewe ndo utakuwa kilaza zaidi yangu
 
kumbe nawe umeliiona hilo mkuu yanachosha mtu anashindwa kutoa kitu chako jamani?

Haya mambo yanapoteza muda na kusumbua akili za watu tu. Mtatoa ushauri na haumfikii mlengwa ni sawa na kazi bure tu sijui mtoa mada anakuwa na lengo gani hasa
 
Isee mapenzi matamu sana ikibidi ka vipi ndoa ifungwe tu dada zetu mkipenda mnapigwa na upofu kabisa!
 
Mimi naitwa Halima ni msichana wa miaka 19 Nasoma kidato cha tatu (form 3) hapa Arusha.... nimejitokeza kwenu kuomba ushauri
Mimi nina mpenzi wangu ambae yupo chuo kikuu, ana miaka 25... kutokana na upendo anaonionyesha sitamani tena kuendelea na shule... kwani nikiwa darasani muda wote namuwaza yeye tu
Nilicho penda kutoka kwa huyu BOYFRIEND wangu ni kua ananijali sana na ana pesa kwan kwao wanajiweza kifedha... ananionga sana PESA kwani nikitaka hela ya CHIPS KUKU hua ananipa, hela ya lotion, pafyumu na saloon hua ananipa kila mwezi kwahiyo sina shida na shule wala sioni umuhimu wa shule.
NAOMBENI ushauri wenu jamani.. niwaambie nini WAZAZI wangu ili wanikubalie niache SHULE ili niolewe na huyu MWANAUME nifaidi pesa zake na mali za nyumbani kwao

recycled and not funny
 
Kuwa makini inawezekana mpo wengi hiyo pesa chambo na wewe unajiingiza mzima mzima
 
Back
Top Bottom