Pole na hekaheka za hapa na pale za kujitafutia riziki, nisiwachoshe sana ngoja niende kwenye mada. Ni mwaka wa kumi na tatu tangia jamaa yangu aoane na mwenzie wana watoto 4 mpaka sasa kwa mtoto wa kwanza maisha yao ya kimahusiano yalikuwa mazuri ktk familia, kukurukakala zilianzia baada ya kumzaa mtoto wa 3, mke alianza kwenda nyumbani kwao Mara kwa Mara kwa wiki ilikuwa Mara mbili au tatu mume kuona tabia imekolea akaamua kuhoji, mke akajibu tabu iko wapi si ninaenda nyumbani?? Mume akamezea kwanza. Lakini baada ya kuona mke haachi kwenda kwao siku moja akaamua kufuatilia kuona nini huwa kinajiri?? Alipofika kwa wazee akakaribishwa kwa bashasha baada ya kuongea mawili matatu akaamua kufunguka kilichokuwa kimempeleka pale majibu aliyopewa mpaka leo hatamani kwani aliambiwa mkewe ana miezi minne hajawahi kanyaga nyumbani, Mme akapigwa na bumbuwazi akaeleza namna mkewe anavyoaga kwa kudai kuwa anakwenda nyumbani na namna alivyoona tabia hiyo imekithiri akaamua kufuata nyuma siku hiyo baada ya mke kuaga kuwa anaenda nyumban ili kama kuna ya kuongea wayamalize, basi jamaa baada ya kuwa amepewa majibu Yale akarudi nyumbani akiwa mnyonge, mke baada ya kurudi Mme akahoji huwa unaenda Wapi mbona nyumbani hawajakuona siku nyingi?? Mke akasema huwa anaenda kwenye business ambayo huwa anaifanyia mtaan kwao, Mme akahisi kunyang'anywa make akakomaa amwambie ukweli kuhusu kinachoendelea akamnasa vibao viwili vitatu ili akae Sawa mke akaamua kufunguka ukweli wake kuwa yeye hakumpenda alimlazimisha kumuoa lkn aliweka nadhiri ktk nafsi yake kuwa one day atamuacha na kama haitoshi alimlazimisha kubadili dini kutka ktk ukristo na kuingia kwenye uislam, basi mume ikabidi ashuke akamuomba make aseme chochote Mme atatoa ili mradi wayaweke Sawa mke akataka ya kutaka Mme akagharamikia mke akasema yameisha lkn akaomba ombi moja tu kwa mmewe kwamba kila mmoja aendelee na dini yake Mme akaridhia maisha yakasonga baada ya miezi kadhaa tabia ya mke imerudi kuliko hata mwanzoni anaweza kutoka nyumban siku mbili mfululizo Mme hajui yuko wapi, Mme amepeleka malalamiko nyumbani, ameomba ushauri sehemu mbalimbali lakini mke haoneshi kubadirika anadai anampenda sana mke wake na hataki watoto wake walelewe na mama mwingine tofauti na mkewe. Sasa anahisi kulemewa na Tabia hii anahisineno ningejua limekuja mwisho was safari. Ushauri wenu wazoefu was mambo haya....... Nawasilisha