Anafikiri alipotea njia

Anafikiri alipotea njia

Elpaul

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2018
Posts
984
Reaction score
757
Pole na hekaheka za hapa na pale za kujitafutia riziki, nisiwachoshe sana ngoja niende kwenye mada. Ni mwaka wa kumi na tatu tangia jamaa yangu aoane na mwenzie wana watoto 4 mpaka sasa kwa mtoto wa kwanza maisha yao ya kimahusiano yalikuwa mazuri ktk familia, kukurukakala zilianzia baada ya kumzaa mtoto wa 3, mke alianza kwenda nyumbani kwao Mara kwa Mara kwa wiki ilikuwa Mara mbili au tatu mume kuona tabia imekolea akaamua kuhoji, mke akajibu tabu iko wapi si ninaenda nyumbani?? Mume akamezea kwanza. Lakini baada ya kuona mke haachi kwenda kwao siku moja akaamua kufuatilia kuona nini huwa kinajiri?? Alipofika kwa wazee akakaribishwa kwa bashasha baada ya kuongea mawili matatu akaamua kufunguka kilichokuwa kimempeleka pale majibu aliyopewa mpaka leo hatamani kwani aliambiwa mkewe ana miezi minne hajawahi kanyaga nyumbani, Mme akapigwa na bumbuwazi akaeleza namna mkewe anavyoaga kwa kudai kuwa anakwenda nyumbani na namna alivyoona tabia hiyo imekithiri akaamua kufuata nyuma siku hiyo baada ya mke kuaga kuwa anaenda nyumban ili kama kuna ya kuongea wayamalize, basi jamaa baada ya kuwa amepewa majibu Yale akarudi nyumbani akiwa mnyonge, mke baada ya kurudi Mme akahoji huwa unaenda Wapi mbona nyumbani hawajakuona siku nyingi?? Mke akasema huwa anaenda kwenye business ambayo huwa anaifanyia mtaan kwao, Mme akahisi kunyang'anywa make akakomaa amwambie ukweli kuhusu kinachoendelea akamnasa vibao viwili vitatu ili akae Sawa mke akaamua kufunguka ukweli wake kuwa yeye hakumpenda alimlazimisha kumuoa lkn aliweka nadhiri ktk nafsi yake kuwa one day atamuacha na kama haitoshi alimlazimisha kubadili dini kutka ktk ukristo na kuingia kwenye uislam, basi mume ikabidi ashuke akamuomba make aseme chochote Mme atatoa ili mradi wayaweke Sawa mke akataka ya kutaka Mme akagharamikia mke akasema yameisha lkn akaomba ombi moja tu kwa mmewe kwamba kila mmoja aendelee na dini yake Mme akaridhia maisha yakasonga baada ya miezi kadhaa tabia ya mke imerudi kuliko hata mwanzoni anaweza kutoka nyumban siku mbili mfululizo Mme hajui yuko wapi, Mme amepeleka malalamiko nyumbani, ameomba ushauri sehemu mbalimbali lakini mke haoneshi kubadirika anadai anampenda sana mke wake na hataki watoto wake walelewe na mama mwingine tofauti na mkewe. Sasa anahisi kulemewa na Tabia hii anahisineno ningejua limekuja mwisho was safari. Ushauri wenu wazoefu was mambo haya....... Nawasilisha
 
kumuacha huyo mke ni bora kwake, huwezi kuvumilia tabia mbovu za mke kwa kisingizio cha watoto, hakuna jema watoto wanalojifunza hapo, aache utegemezi wa kuamini hawezi pata mke bora kuliko huyo, ataishia kwenye presha na ugonjwa wa moyo
 
Labda wanaume tumetofautiana sana,mm hata kama tuna wajukuu siku akileta ujinga ataondoka na wajukuu ataamua yeye eidha aende nao au awaache maana pote watakuwa kwa mzazi wao,huo ni ubwege siyo upendo.
 
Wanaume wanaokaliwa sikuizi wamekuja na excuse ya watoto.

MWANAUME NI MISIMAMO NA SHERIA

Siku atakavyoanza kuleta wanaume ndani akili zitamrudi.
Mkuu Luna mambo mengine ukisimuliwa tu Alam ya jambo Fulani inalia kichwani
 
Duuh. Pole yake ila huyo mume alishindwa kusimama kama mwanaume tangia mwanzo sababu lait ingekuwa hizo tabia za kusafiri safiri amezipiga marufuku tangia mwanzo wala hayo yasingetokea na pia anatakiwa ajue huyo mwanamke hana lolote sababu mtu mpaka kamzalia watoto bado anasema hakumpenda. Mmh.

Hicho asichokitaka ndio sahihi sasa sababu ikiwa hali imeshafikia huko halafu anasema hataki watoto walelewe na mtu mwingine huko sijui anataka nini kingine.

Sababu huyo mwanamke hawezi kugeuka nyuma mpaka yakamkute huko kunakompa jeuri hivyo asipoteze muda wake kutwanga maji kwenye kinu.
 
Labda wanaume tumetofautiana sana,mm hata kama tuna wajukuu siku akileta ujinga ataondoka na wajukuu ataamua yeye eidha aende nao au awaache maana pote watakuwa kwa mzazi wao,huo ni ubwege siyo upendo.
Mkuu Meru nakuona huna mchezo kabisa lkn wanaume tumeumbwa mteso kweli
 
Duuh. Pole yake ila huyo mume alishindwa kusimama kama mwanaume tangia mwanzo sababu lait ingekuwa hizo tabia za kusafiri safiri amezipiga marufuku tangia mwanzo wala hayo yasingetokea na pia anatakiwa ajue huyo mwanamke hana lolote sababu mtu mpaka kamzalia watoto bado anasema hakumpenda. Mmh.

Hicho asichokitaka ndio sahihi sasa sababu ikiwa hali imeshafikia huko halafu anasema hataki watoto walelewe na mtu mwingine huko sijui anataka nini kingine.

Sababu huyo mwanamke hawezi kugeuka nyuma mpaka yakamkute huko kunakompa jeuri hivyo asipoteze muda wake kutwanga maji kwenye kinu.
ahsante mkuu emyta naweza sema penzi ni upofu
 
Mkuu Meru nakuona huna mchezo kabisa lkn wanaume tumeumbwa mteso kweli
Mengine unayaepuka kwa maamzi magumu mkuu,tofauti na hapo utatangulia mbele za haki kwa msongo
 
Kulazimisha penzi ni sawa na kulazimisha fani mwishowe mnaleta utani,ipo siku mwanamke atakuja kumuua,
Mda bado.
 
Pole na hekaheka za hapa na pale za kujitafutia riziki, nisiwachoshe sana ngoja niende kwenye mada. Ni mwaka wa kumi na tatu tangia jamaa yangu aoane na mwenzie wana watoto 4 mpaka sasa kwa mtoto wa kwanza maisha yao ya kimahusiano yalikuwa mazuri ktk familia, kukurukakala zilianzia baada ya kumzaa mtoto wa 3, mke alianza kwenda nyumbani kwao Mara kwa Mara kwa wiki ilikuwa Mara mbili au tatu mume kuona tabia imekolea akaamua kuhoji, mke akajibu tabu iko wapi si ninaenda nyumbani?? Mume akamezea kwanza. Lakini baada ya kuona mke haachi kwenda kwao siku moja akaamua kufuatilia kuona nini huwa kinajiri?? Alipofika kwa wazee akakaribishwa kwa bashasha baada ya kuongea mawili matatu akaamua kufunguka kilichokuwa kimempeleka pale majibu aliyopewa mpaka leo hatamani kwani aliambiwa mkewe ana miezi minne hajawahi kanyaga nyumbani, Mme akapigwa na bumbuwazi akaeleza namna mkewe anavyoaga kwa kudai kuwa anakwenda nyumbani na namna alivyoona tabia hiyo imekithiri akaamua kufuata nyuma siku hiyo baada ya mke kuaga kuwa anaenda nyumban ili kama kuna ya kuongea wayamalize, basi jamaa baada ya kuwa amepewa majibu Yale akarudi nyumbani akiwa mnyonge, mke baada ya kurudi Mme akahoji huwa unaenda Wapi mbona nyumbani hawajakuona siku nyingi?? Mke akasema huwa anaenda kwenye business ambayo huwa anaifanyia mtaan kwao, Mme akahisi kunyang'anywa make akakomaa amwambie ukweli kuhusu kinachoendelea akamnasa vibao viwili vitatu ili akae Sawa mke akaamua kufunguka ukweli wake kuwa yeye hakumpenda alimlazimisha kumuoa lkn aliweka nadhiri ktk nafsi yake kuwa one day atamuacha na kama haitoshi alimlazimisha kubadili dini kutka ktk ukristo na kuingia kwenye uislam, basi mume ikabidi ashuke akamuomba make aseme chochote Mme atatoa ili mradi wayaweke Sawa mke akataka ya kutaka Mme akagharamikia mke akasema yameisha lkn akaomba ombi moja tu kwa mmewe kwamba kila mmoja aendelee na dini yake Mme akaridhia maisha yakasonga baada ya miezi kadhaa tabia ya mke imerudi kuliko hata mwanzoni anaweza kutoka nyumban siku mbili mfululizo Mme hajui yuko wapi, Mme amepeleka malalamiko nyumbani, ameomba ushauri sehemu mbalimbali lakini mke haoneshi kubadirika anadai anampenda sana mke wake na hataki watoto wake walelewe na mama mwingine tofauti na mkewe. Sasa anahisi kulemewa na Tabia hii anahisineno ningejua limekuja mwisho was safari. Ushauri wenu wazoefu was mambo haya....... Nawasilisha

ki ukweli hatuna cha kumshauri-tayari jibu analo mke ashasema hakumpendaa,aende anako pendwa,wanawake bado wapo walio na heshma zao na utuu nyoyoni mwao,usi isihishi kwa mazoe iishi kwa kanuni na sheria zilizo simama na kutekelezwa kama kiongozi wa familia,mwanzo hamna ndoa hapo kwa kua ndoa ilifungwa na misingi ya kidini na dini haipo,pili hakua amempenda huenda ali lazimishwa na ndoa kuswihi ili upendo uwepo na aridhie mtu mwenyewe,atafuta anae endana nae tuu-mbona tuna penda kua kama kupee,
 
Huu upendo wa mke umezidi kipimo, japo ana point kuhusu malezi ya watoto.
Kwa kifupi hana mke bila anaishi na MWANAMKE
 
Pole sana kwa yanayokusibu...

Inasikitisha sana...
Kumbuka kwamba duniani tunaishi mara moja tu, usiruhusu kiumbe yoyote kuchezea maisha yako...

Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom