Wengi humu hamuelewi historia ya sherehe za ndoa.
====NI HIVI====
Hufika wakati katikati ya sherehe ya harusi bwana harusi hutakiwa kuwaonyesha hadhira "chuma alichopatiwa hati miliki" Na mambo hufanywa kama desturi isemavyo kwamba bwana harusi humfunua shella bibi arusi kwa kutokea mbele na kumfunika nalo kichwani hivyo kuuacha mwili wa bibi harusi ukiwa mtupu toka tumboni hadi miguuni.
Ni wakati huu ndio hadhira hulipuka kwa shangwe na vigelegele na sherehe kupamba moto ikihanikizwa na mirindimo ya ngoma, zumari, matari, vinubi, mazeze na pembe (tarumbeta)
Hii taratibu Inayo falsafa murua kabisa iliyowanya wamama kujiheshimu sana na kuiheshimu zaidi jamii inayowazunguka.