Anaedaiwa kuiibia PBZ Aachiwa Huru. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Anaedaiwa kuiibia PBZ Aachiwa Huru.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Junius, Jul 26, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Jul 26, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mwane Mashungu.
  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imemfutia mashitaka mfanyabiashara maarufu Zanzibar, Said Nasir Bopar aliyekuwa akikabiliwa na tuhuma za kuiba dola 880,000 za Marekani kabla ya kesi yake kuanza kusikilizwa.
  Uamuzi wa kufutiwa mashitaka yaliyokuwa yakimkabili, ulitolewa na Mkurugenzi wa Mashitaka wa SMZ (DPP), Othman Masoud Othman kutokana na uwezo aliopewa na sheria namba 7 kifungu 95 (1) ya mwenendo wa makosa ya jinai ya mwaka 2004.
  Mfanyabiashara huyo alikamatwa na kufunguliwa mashitaka ya wizi wa fedha hizo Julai 17, mwaka huu, pamoja na wafanyabiashara wengine na wafanyakazi wawili wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ).
  Bopar na wenzake walifunguliwa mashitaka ya kula njama za kuiba fedha viwango tafauti katika Benki ya Watu wa Zanzibar, ambayo hutumika kuhifadhi fedha za wananchi wa Zanzibar wakiwemo wakulima na wavuvi.
  Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Aziza Suwedi, akiwasilisha uamuzi wa Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Mkoa Vuga, Mkusa Isack Sepetu, alisema Mkurugenzi wa Mashitaka ameamua kumfutia mashitaka mfanyabiashara huyo kutokana na uwezo aliopewa kisheria.
  Alisema kulingana na barua ya mkurugenzi huyo wa mashitaka kwenda kwa Mrajis Mkuu wa Mahakama Kuu Zanzibar, amefikia uamuzi huo Julai 22 kuwa mfanyabiashara huyo afutiwe shitaka lililokuwa limefikishwa mbele ya mahakama hiyo.
  “Mheshimiwa hakimu niko hapa kumuwakilisha DPP kwa kuwasilisha uamuzi wake wa kumuondoshea mashiataka mshitakiwa aliyepo mbele yako kutokana na uwezo aliopewa kisheria,” alisema mwendesha mashitaka huyo.
  Hakimu Mkusa Sepetu alitaka kufahamu alipo wakili wa mshitakiwa huyo kabla ya kutoa uamuzi wake, lakini kwa wakati huo hakuwepo mahakamani hapo.
  Hata hivyo, Hakimu Mkusa alisema mahakama haina pingamizi na uamuzi wa mkurugenzi wa mashitaka kwa vile sheria inampa uwezo, na kumueleza mshitakiwa aliyekuwa kwenye kizimba wakati huo kuwa yuko huru baada ya mashitaka yaliyokuwa yakimkabili kuwa yamefutwa.
  Mfanyabiashara huyo na wenzake walifikishwa mahakamni kwa mara ya kwanza Julai 17 na kusomewa mashitaka yao na Mwendesha Mashitaka Juma Msafiri na Khamis Suwedi ya kula njama na kuiba zaidi ya shilingi bilioni tatu.
  Kabla ya kuanza kusikilizwa kesi hiyo, mtafaruku mkubwa ulijitokeza baada ya mwangalizi wa ofisi wa mahakama kuu, Haji Pandu kutoa tangazo kuwa waandishi wa habari hawaruhusiwi kumpiga picha mfanyabiashara huyo.
  Aidha, tangazo hilo lilisisitiza mbali na kutoruhusiwa kupiga picha, waandishi hao hawaruhusiwi kutumia vinasa sauti mahakamani hapo muda wote kesi hiyo itakapokuwa ikiendelea.
  Kutokana na kujitokeza hali hiyo, baadhi ya waandishi walilazimika kumuuliza Mrajis wa Mahakama Kuu, Essaya Kayange juu ya uhalali wa kuzuiliwa kutekeleza majukumu yao.
  Kayange alisema kwamba waandishi wa habari wanaruhusiwa kupiga picha ndani ya mahakama kabla ya mahakama kuanza kusikiliza kesi.
  Akiwa amezungukwa na watu wanaosadikiwa kuwa wapambe wake na baadhi ya askari polisi, mfanyabiashara huyo aliondoka mahakamani hapo na kupanda katika gari la kisasa aina ya Toyota Land Cruiser.
  Alipomsomea shitaka lake kwa mara ya kwanza Julai 17 mwaka huu, Mwendesha Mashitaka, Juma Msafiri alidai mahakamani hapo kuwa mfanyabiashara huyo alikula njama na kuiba dola za Marekani 880,000 Machi 11, mwaka huu.
  Hata hivyo, mfanyabiashara huyo mwenye asili ya Kiasia alinyimwa dhamana baada ya upande wa mashitaka kudai kima cha fedha alizoiba na wenzake ni kikubwa na kuwepo kwao nje kunaweza kuathiri upelelezi wa kesi hiyo.
  Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ambao bado wanasota katika gereza la Kiinua Miguu mjini Zanzibar ni Meneja wa Operesheni wa BPZ, Ramadhan Mussa Jecha (47) na Juma Abbas ambaye ni Mshika Fedha Mkuu wa benki hiyo.
  Ramadhan Mussa, ilidaiwa mahakamni hapo kuwa aliiiba dola za Marekani 379,240, 000, ambapo Abas anatuhumiwa kuchota dola 341,220, 000.
  Watuhumiwa wengine ni Zahor Mbaraka Salum anayedaiwa kuiba dola za Marekani 340,000 na Suleyum Mbaraka Salum dola 1,220, 000.
  Taarifa za mfanyabiashara huyo kufutiwa mashitaka zilianza kuenea juzi mchana kufuatia mchakato uliokuwa ukiendelea nje ya taratibu za kisheria.
  Bopar ni kiungo muhimu katika soko la biashara Zanzibar, ambaye hivi karibuni alikumbwa na msukosuko wa tuhuma za kuingiza mchele tani 2,900 kutoka Pakistan ambao haufai kwa matumizi ya binadamu. Sakata hilo ambalo lilisababisha Waziri Kiongozi Shamsi Vuai Nahodha kuunda tume ya uchunguzi lilisababisha aliyekuwa Mkemia Mkuu wa SMZ, Haji Bonde na aliyekuwa Mkurugenzi wa Biashara Zanzibar, Salma kupoteza nyadhifa zao. Hata hivyo, mchele huo baadaye ulipotezwa Zanzibar na kudaiwa kupelekwa mkoani Tanga na chimbuko la kuundwa tume hiyo lilitokana na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutaka suala hilo lichunguzwe ili ukweli wake ufahamike.

  source: Tanzania Daima.[​IMG]
   
 2. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  One sided story
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Jul 26, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  unnecessarily looong story!
   
 4. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Jamaa wa UK watafurahi sasa
   
 5. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #5
  Jul 27, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Hivi huo mchele wa Pakistani wanaosema haufai kwa matumizi ya wanadamu Visiwani: ni kweli umepelekwa Tanga??
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Jul 27, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Can you give us the other side of the story?
   
 7. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #7
  Jul 27, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Kumbe si madogo!!!!!!
   
 8. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #8
  Jul 27, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Biashara ya pesa na bandari iliingia kigugumizi baada ya jamaa kushikwa...!
   
 9. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #9
  Jul 27, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  No PakaJimmy, we are under spam attack!!!!!
   
 10. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #10
  Jul 27, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Kuna mtu "nyumba kubwa" kanitonya umbea kuwa hata shughuli zilisimama na ingia toka kutwa nzima kama mzinga wa nyuki, mwisho Othmani Masoud akapokea ujumbe kutoka kwa "Bwana Mkubwa", nayeye bila kinyongo akaandika "Nollei Prosequi" kwa mkono wake na kaichapa mwenyewe, na Mh. Mkusa akapewa habari kabisa kuwa hakuna masuala wala kuhoji, futa kesi watu waendelee na biashara na wale wengne "mbuzi kavimba" wakaachwa wanatafunwa na mbu kiinua miguu.
   
 11. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #11
  Jul 27, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Ndio mambo na vijimambo vya Zenj!
   
 12. M

  MLEKWA Senior Member

  #12
  Jul 29, 2009
  Joined: Aug 18, 2007
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukweli ya yote wakubwa wa SMZ na ndani ya SMZ wanahusika na wizi huu benki inaendesha kama kampuni ya baba mdogo haina dicipline unaweza kumhonga mtu ndan i ya benki hii na kukupa mamilioni bila ya kuwa collateral yotote as long hiyo biashara unayofanya faida mugawane na watu wa Benki ?
  Zanzibar inaiggopa technology kwani wizi utakua haupo na hii ndio njia ya pekee kutumia techonology kuondoa uoza wa Benki hii.
   
 13. Mopao Josee

  Mopao Josee JF-Expert Member

  #13
  Jul 29, 2009
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  chini ya kapeti but do not qoute
  WAKO SHARE HA HAA HAAAAAAAAAAAAAAH
   
 14. C

  Chakarota Member

  #14
  Jul 29, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Znz hakuna wizi kama unavyotangazia, bali watu huchukua chao na wakagawana kama wanavyofanya kwenye matukio ya uchafuzi na kugawana madaraka. Sasa hapo liliotokea ni mkubwa mmoja hakupewa chake ndiyo maana siri ikavuja na mmoja au kundi wakawekwa ndani. jee kuna kesi yoyote inaendelea kwenye ishuu hii ? Hivi ndivyo ipigwavyo huko pwani, lazima uelewe ichezwavyo la si hivyo unakwenda na maji.
   
Loading...