Anachokifanya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ni kuuza ramani kwa adui, maana huwezi kuwatangazia wauza madawa ya kulevya kwamba leo usiku utaenda kuwakamata halafu uwakute na kidhibiti, sijui ni kwanini huyu jamaa ameamua kuharibu vita hii ya kupambana na madawa ya kulevya kwa kuwa alert wauzaji kabla ya kuwakamata, ilitakiwa kabla ya kwenda kwenye media kututangazia mbinu na maeneo ya wauzaji na wasambazaji wa madawa ya kulevya wawe wamekamatwa na sio kututangazia halafu uende kuwakamata hutakuta ushahidi.
Makonda amesahau kuwa anaopambana wengi ni watu wazito wenye ukwasi na wako smart na hata hiyo sheria ya madawa ya kulevya anayoisema wanaijua vyema, kitendo cha kwenda kwenye vyombo vya habari na kutangaza namna utakavyo washughulikia unawapa nafasi na wao kujipanga namna watavyovicha ushahidi na kubadili mbinu ya kusambaza mzigo wao.
Hili suala la kuuza ramani kwa hawa watu linaweza kuwa limefanyika makusudi ili kuwasaidia hawa wauzaji na wasambazaji wa madawa ya kulevya, hivi ni nani leo atamsubiri makonda atakapoenda kuwasha moto kwenye mahoteli aliyoyasema, nani leo atatumia bandari bubu kuingiza mzigo wakati anajua kwamba zinajulikana. Hivi kulikuwa na haja gani ya kuliongelea suala hili kwenye vyombo vya habari baadala ya kulifanya kimya kimya.
Ni dhahiri shahiri kuwa makonda anafanya yote haya sio kwa nia ya dhati bali kutafuta sifa Minardi na kuwachafulia jina kundi fulani la watu.