Anaandika Dotto Bulendu kuhusu bunge la JMT

Viongozi wetu wengi wanafiki na vigeugeu, wanajali zaidi vyama vyao kuliko maslahi ya Taifa.

Ndio maana wanachokizungumza leo sicho watakachokitetea Mwakani.
acha kupepesa macho,waliopitisha ni ccm lakini unaogopa kuwa specific na kuwalaani,instead unaleta generalization eti "vyama"..hapa wa kulaumiwa ni ccm wasema ndioooooo
 
kiukweli bunge hili lina wabunge wengi wasiojielewa. kwa mtazamo wangu bunge hili limechangia kulifikisha taifa letu hapa lilipo. kazi yao ni kutetea vyama vyao na si taifa letu na watu wake. kwao huungana pamoja bila kujali vyama pale linapo kuja suala la posho tu. kwa sasa wanajifanya kumpongeza rais kwa kuzuia mchanga badala ya kuitaka serikali kupeleka mswada wa kurekebisha sheria mbovu za madini. wengine ni kumponda tu rais bila kuonyesha njia.
 
Wanajifany wana uchungu sana na nchi hii
Hili bunge hili nalo linataka tuliamini kwenye sakata la madini nchini kwetu? liaminiwe kwa lipi ?

1.Ni mhimili huu huu mwaka 1997,ulipitisha kwa dharura sheria mbili,ile ya kodi na ya uwekezaji,sheria zilizohalalisha wawekezaji kukwapu madini yetu,sheria ambazo zilifuta kodi nyingi kwenye sekta ya madini,mhimili huu huu ukiitika ndiyooo,kuhalalisha wawekezaji kusamehewa na kufutiwa kodi!.

2.Ni hawa hawa mwaka 2007,walimfukuza bungeni Zitto Kabwe baada ya kutaka ufanyike uchunguzi kwenye mkataba kati serikali na huyuhuyu Acacia wakati huo akiitwa Barrick,hawahawa walitetea huo mkataba uliowaruhusu Barrick kusafirisha haya Makinikia,hawahawa walikataa waziri aliyesaini mkataba huo asijadiliwe bungeni na kumuadhibu aliyeibua hoja kuhusu Mkataba huo ulioidhinisha wana Kahama wafukuzwe kwenye maeneo yao kuwapisha hawa Acacia!.

Tena waliotetea mkataba huu uliovuja mpaka kwenye vyombo vya habari,baadhi yao bado wamo bungeni,wengine ni viongozi bungeni!.

3.Ni hawa hawa,na wengine wamo bungeni tena ni viongozi,mwaka 2010 waliitetea sheria ya madini na kupiga kura za ndiyooo sheria hii inayowapunja wazawa kwenye malipo ya fidia baada ya kuhamishwa kupisha wawekezaji wakiwemo Acacia!.

Hii sheria ya ajabu inayosema eti mtanzania yeye anamiliki sehemu ya juu ya ardhi ,huko chini siyo mali yake,ni mhimili huu huu ndiyo mwaka 2010 ulitunga sheria ya kuwafanya watu wanaoishi pembezoni mwa migodi wawe masikini wa kutupwa pamoja na kuishi sehemu yenye utajiri!

4.Ni mhimili huu huu,mwaka 2009,ukifumbua macho unyama wa Barrick pale wananchi wa Nyamongo walipotiririshiwa sumu,baadhi wakababuka,wengine wakapoteza maisha,mifugo ikafa,ardhi ikachafuliwa na sumu,mhimili huu huu uliunda kamati mwaka 2009,kamati ambayo mwisho wa siku iliwakumbatia wawekezaji na kuwaita waathirika wa sumu kuwa ni wavamizi/wizi,kinachonidikitisha baadhi ya wajumbe wa kamati ile bado wamo bungeni,waliwasaliti wana wa wanyongo kwa kuwaambia wamejitakia kwa kuwavania wawekezaji,leo wanaidai kuongea kwa hasira wakati mwaka 2009 waliwasaliti watanzania na kuwatetea wawekesaji,leo wanataka tuwaone vinara wa kwenye wizi huu wa madini!.

5.Mwaka 2004,watanzania waliokuwa wanaishi kijiji cha Mtakuja,wakihamishwa kinyama,usiku wa manane,kamati ya mhimili huu ilikwenda Geita,ikashuhudia watanzania wakiishi kwenye jengo chakavu la mahakama eneo la Sofia town,baadhi yao mpaka leo wamo bungeni,walifumbia macho unyama huu,waliwaita watu wa mtakuja wavamizi,leo wanataka tuwaamini kuwa wana uchungu na wizi huu!.

6.Hivi hawa wabunge hawajui chochote kinachoendelea Geita?hawajui kinachoendelea Nyamongo ,hawajui kinachoendelea Mererani?.Wanasubiri nani aseme kinachoendelea huko?je wao wanachojua ni makinikia tu?

7.Huu mhimili huu umekaa kimya miaka yote,kamati ya Bomani,kamati ya Lau,kamati ziliundwa zaidi ya tatu kabla ya hii,ripoti mbali mbali zimetoka zikithibitisha uporwaji wa mali zetu,huu mhimili ulikuwa unatazama tu,nakumbuka baada ya mto Tigithe kumwagiwa sumu,kamati ya viongozi wa dini iliinda timu ya wataalam kuchunguza kama kweli mto tigithe ulichafuliwa na sumu kutoka Barrick,ripoti ilitoka,ikathibitisha kuwa mto ulichafuliwa na sumu,huu mhimili kimyaaaaa,haukuwahi hata itumia tafiti hiyo kusaka haki ya waathirika wa sumu za Tigithe!.

8.Ni mhimili huu huu ndiyo ulitunga sheria ya sisi kupata mrahaba/mrabaha wa asilimi 4 tu,ni hawa hawa walipitisha sheria hii,sasa wanataka tuwaamini kwa lipi?

Mhimili huu ujitafakari unapojadili mambo mazito ya nchi hii,ujipime uzalendo wake,ujipime uwezo wake kuisimamia serikali,ujipime uwezo wake kuwawakilisha watanzania!.

Huu mhimili huu?any way!usiku mwema!.

Dotto Bullendu.
 
Mara zote huwa napata shida sana kuhukumu watu kwa jumla.

Kuna wabunge ndio kwanza wameingia ubunge 2015. Je, ni haki kuwalaumu haokwa maamuzi waliokuwepo kuanzia 1995 ambao wengine washafariki?

Kuna wabunge walipinga hayo yaliyolalamikiwa, lakini kwa kuwa hawakuwa na majority wakashindwa, na hao nao tuwalaumu?

Kitu cha muhimu ni kushurutisha bunge lipitishe hoja zote kwa kura ya wazi na kila mbunge ajulikane rekodi yake alivyopiga kura katika kila hoja.

Hapo tutajua nani ni nani na hata tukienda kupiga kura, tutapiga kura kwa data.

Sio sasa hivi kila kitu ni kificho na uzushi tu.

Kuanzia mikataba ya madini mpaka wabunge wanavyopiga kura.
 
Usisahau kificho hadi bunge lenyewe ili tusijue nani kasema nini maana tukijua tunaweza tusimchague au tukamchagua kutokana na hoja zake. Hii ni kuzidi kuwafanya watu wawe gizani.
 
Uvyama ni jambo baya sana. Hawa wafuasi wa kijani hasa wabunge ambao ni wakongwe kwenye hii kadhia ya mikataba ya madini kimsingi walipaswa kukaa kimya,hawana uhalali wa kutia neno. Wanakula matapishi yao wenyewe ambapo walikua hodari kugonga meza kwa furaha za kiushabiki. Mambo yote yalifanyika kwa baraka zao. Leo bila aibu wanatia neno.
Hakuna kitu kilichostaajabisha kama kuyasigina maoni ya wananchi ambayo yalikua na mambo mazuri,uvyama ukatutoa ufahamu,leo tumekwama. Hata leo akitokea kiongozi mkuu akasema anaamua kwa dhati yake kubatilisha Katiba pendekezwa na akasema ni bora kuriview Maoni ya Rasimu,wale wale walioipinga watagonga meza tena kwa kufaraha. Hii yote ni kwa sababu ya uvyama. Tatizo ni kubwa sana na litatusumbua mno, haya mambo ya itikadi za vyama
 
Hili bunge hili nalo linataka tuliamini kwenye sakata la madini nchini kwetu? liaminiwe kwa lipi ?

1.Ni mhimili huu huu mwaka 1997,ulipitisha kwa dharura sheria mbili,ile ya kodi na ya uwekezaji,sheria zilizohalalisha wawekezaji kukwapu madini yetu,sheria ambazo zilifuta kodi nyingi kwenye sekta ya madini,mhimili huu huu ukiitika ndiyooo,kuhalalisha wawekezaji kusamehewa na kufutiwa kodi!.

2.Ni hawa hawa mwaka 2007,walimfukuza bungeni Zitto Kabwe baada ya kutaka ufanyike uchunguzi kwenye mkataba kati serikali na huyuhuyu Acacia wakati huo akiitwa Barrick,hawahawa walitetea huo mkataba uliowaruhusu Barrick kusafirisha haya Makinikia,hawahawa walikataa waziri aliyesaini mkataba huo asijadiliwe bungeni na kumuadhibu aliyeibua hoja kuhusu Mkataba huo ulioidhinisha wana Kahama wafukuzwe kwenye maeneo yao kuwapisha hawa Acacia!.

Tena waliotetea mkataba huu uliovuja mpaka kwenye vyombo vya habari,baadhi yao bado wamo bungeni,wengine ni viongozi bungeni!.

3.Ni hawa hawa,na wengine wamo bungeni tena ni viongozi,mwaka 2010 waliitetea sheria ya madini na kupiga kura za ndiyooo sheria hii inayowapunja wazawa kwenye malipo ya fidia baada ya kuhamishwa kupisha wawekezaji wakiwemo Acacia!.

Hii sheria ya ajabu inayosema eti mtanzania yeye anamiliki sehemu ya juu ya ardhi ,huko chini siyo mali yake,ni mhimili huu huu ndiyo mwaka 2010 ulitunga sheria ya kuwafanya watu wanaoishi pembezoni mwa migodi wawe masikini wa kutupwa pamoja na kuishi sehemu yenye utajiri!

4.Ni mhimili huu huu,mwaka 2009,ukifumbua macho unyama wa Barrick pale wananchi wa Nyamongo walipotiririshiwa sumu,baadhi wakababuka,wengine wakapoteza maisha,mifugo ikafa,ardhi ikachafuliwa na sumu,mhimili huu huu uliunda kamati mwaka 2009,kamati ambayo mwisho wa siku iliwakumbatia wawekezaji na kuwaita waathirika wa sumu kuwa ni wavamizi/wizi,kinachonidikitisha baadhi ya wajumbe wa kamati ile bado wamo bungeni,waliwasaliti wana wa wanyongo kwa kuwaambia wamejitakia kwa kuwavania wawekezaji,leo wanaidai kuongea kwa hasira wakati mwaka 2009 waliwasaliti watanzania na kuwatetea wawekesaji,leo wanataka tuwaone vinara wa kwenye wizi huu wa madini!.

5.Mwaka 2004,watanzania waliokuwa wanaishi kijiji cha Mtakuja,wakihamishwa kinyama,usiku wa manane,kamati ya mhimili huu ilikwenda Geita,ikashuhudia watanzania wakiishi kwenye jengo chakavu la mahakama eneo la Sofia town,baadhi yao mpaka leo wamo bungeni,walifumbia macho unyama huu,waliwaita watu wa mtakuja wavamizi,leo wanataka tuwaamini kuwa wana uchungu na wizi huu!.

6.Hivi hawa wabunge hawajui chochote kinachoendelea Geita?hawajui kinachoendelea Nyamongo ,hawajui kinachoendelea Mererani?.Wanasubiri nani aseme kinachoendelea huko?je wao wanachojua ni makinikia tu?

7.Huu mhimili huu umekaa kimya miaka yote,kamati ya Bomani,kamati ya Lau,kamati ziliundwa zaidi ya tatu kabla ya hii,ripoti mbali mbali zimetoka zikithibitisha uporwaji wa mali zetu,huu mhimili ulikuwa unatazama tu,nakumbuka baada ya mto Tigithe kumwagiwa sumu,kamati ya viongozi wa dini iliinda timu ya wataalam kuchunguza kama kweli mto tigithe ulichafuliwa na sumu kutoka Barrick,ripoti ilitoka,ikathibitisha kuwa mto ulichafuliwa na sumu,huu mhimili kimyaaaaa,haukuwahi hata itumia tafiti hiyo kusaka haki ya waathirika wa sumu za Tigithe!.

8.Ni mhimili huu huu ndiyo ulitunga sheria ya sisi kupata mrahaba/mrabaha wa asilimi 4 tu,ni hawa hawa walipitisha sheria hii,sasa wanataka tuwaamini kwa lipi?

Mhimili huu ujitafakari unapojadili mambo mazito ya nchi hii,ujipime uzalendo wake,ujipime uwezo wake kuisimamia serikali,ujipime uwezo wake kuwawakilisha watanzania!.

Huu mhimili huu?any way!usiku mwema!.

Dotto Bullendu.
.

Hoja nzuri tatizo unaishia njiani na wagombea wa chama chetu pendwa Chagadema kikawatanguliza nani ili kusahihisha makosa ya CCM? JPM ananyosha wahuni wote kwa manufaa ya nchi hangalii Chama.Tulikosea hamtaki tusahihishe,leo mnawatetea mliosema wezi halafu kuna mpuuzi anataka wananchi wawaunge mkono watuhumiwa.Hatujawa wazembe kiasi hicho.
 
Watanzania tujitahidi kuachana na udhaifu wa kushadadia mambo tusiyoyajua.
Sakata la ore concentrate, watu wengi hamjui kinachafanyika pale. Cha ajabu tumeishia kupayuka na kutoa kauli ambazo watu wanaojua ukweli wa kinachoendelea, wanatuona sisi wapumbavu.
Mzungu ni mwizi, lakini mara nyingi hawezi kufanya wizi wa kitoto, kama akili zenu za kitoto zinavyowafanya muamini.
Ni kweli tunapigwa na hawa wakoloni, lakini sio kweli kwamba tunapigwa kwa style mnayoaminishwa na wanasiasa wenu. Sitapenda kuingia kiundani kwa sasa kuhusu hili.
I assure you, kwa jinsi sampling inavyofanyika ya kujua contents za mchanga, majibu yanayotoka ni sahihi. Mzungu hawezi ku-plan wizi kwa style mnayodhani anatumia kutuibia.
Hebu angalia structure ya group ya acacia na role ya kila subsidiary, kwa wale wenye akili timamu mtajua ni wapi tunapigwa, sio kwenye sample na uzito wa makinikia
 
.

Hoja nzuri tatizo unaishia njiani na wagombea wa chama chetu pendwa Chagadema kikawatanguliza nani ili kusahihisha makosa ya CCM? JPM ananyosha wahuni wote kwa manufaa ya nchi hangalii Chama.Tulikosea hamtaki tusahihishe,leo mnawatetea mliosema wezi halafu kuna mpuuzi anataka wananchi wawaunge mkono watuhumiwa.Hatujawa wazembe kiasi hicho.

Hebu tuacheni unafiki hebu onyesha mahali ambapo kuna mtu anatetea wezi, kila ninapofuatilia suala hili ninaona watu wana uchungu wa jinsi baadhi ya wenzetu waliotufikisha hapa. Watu wanashauri njia muafaka ya kujinasua na kadhia hii bila kuongeza maumivu zaidi matokeo yake ninona upotoshaji wa hali yajuu. Ninajiuliza hivi watanzania wote bado ni wajinga hawaelewi waliotufikisha hapa kweli! Hebu tusemeni ukweli tuiponye nchi yetu!
 
Hili bunge hili nalo linataka tuliamini kwenye sakata la madini nchini kwetu? liaminiwe kwa lipi ?

1.Ni mhimili huu huu mwaka 1997,ulipitisha kwa dharura sheria mbili,ile ya kodi na ya uwekezaji,sheria zilizohalalisha wawekezaji kukwapu madini yetu,sheria ambazo zilifuta kodi nyingi kwenye sekta ya madini,mhimili huu huu ukiitika ndiyooo,kuhalalisha wawekezaji kusamehewa na kufutiwa kodi!.

2.Ni hawa hawa mwaka 2007,walimfukuza bungeni Zitto Kabwe baada ya kutaka ufanyike uchunguzi kwenye mkataba kati serikali na huyuhuyu Acacia wakati huo akiitwa Barrick,hawahawa walitetea huo mkataba uliowaruhusu Barrick kusafirisha haya Makinikia,hawahawa walikataa waziri aliyesaini mkataba huo asijadiliwe bungeni na kumuadhibu aliyeibua hoja kuhusu Mkataba huo ulioidhinisha wana Kahama wafukuzwe kwenye maeneo yao kuwapisha hawa Acacia!.

Tena waliotetea mkataba huu uliovuja mpaka kwenye vyombo vya habari,baadhi yao bado wamo bungeni,wengine ni viongozi bungeni!.

3.Ni hawa hawa,na wengine wamo bungeni tena ni viongozi,mwaka 2010 waliitetea sheria ya madini na kupiga kura za ndiyooo sheria hii inayowapunja wazawa kwenye malipo ya fidia baada ya kuhamishwa kupisha wawekezaji wakiwemo Acacia!.

Hii sheria ya ajabu inayosema eti mtanzania yeye anamiliki sehemu ya juu ya ardhi ,huko chini siyo mali yake,ni mhimili huu huu ndiyo mwaka 2010 ulitunga sheria ya kuwafanya watu wanaoishi pembezoni mwa migodi wawe masikini wa kutupwa pamoja na kuishi sehemu yenye utajiri!

4.Ni mhimili huu huu,mwaka 2009,ukifumbua macho unyama wa Barrick pale wananchi wa Nyamongo walipotiririshiwa sumu,baadhi wakababuka,wengine wakapoteza maisha,mifugo ikafa,ardhi ikachafuliwa na sumu,mhimili huu huu uliunda kamati mwaka 2009,kamati ambayo mwisho wa siku iliwakumbatia wawekezaji na kuwaita waathirika wa sumu kuwa ni wavamizi/wizi,kinachonidikitisha baadhi ya wajumbe wa kamati ile bado wamo bungeni,waliwasaliti wana wa wanyongo kwa kuwaambia wamejitakia kwa kuwavania wawekezaji,leo wanaidai kuongea kwa hasira wakati mwaka 2009 waliwasaliti watanzania na kuwatetea wawekesaji,leo wanataka tuwaone vinara wa kwenye wizi huu wa madini!.

5.Mwaka 2004,watanzania waliokuwa wanaishi kijiji cha Mtakuja,wakihamishwa kinyama,usiku wa manane,kamati ya mhimili huu ilikwenda Geita,ikashuhudia watanzania wakiishi kwenye jengo chakavu la mahakama eneo la Sofia town,baadhi yao mpaka leo wamo bungeni,walifumbia macho unyama huu,waliwaita watu wa mtakuja wavamizi,leo wanataka tuwaamini kuwa wana uchungu na wizi huu!.

6.Hivi hawa wabunge hawajui chochote kinachoendelea Geita?hawajui kinachoendelea Nyamongo ,hawajui kinachoendelea Mererani?.Wanasubiri nani aseme kinachoendelea huko?je wao wanachojua ni makinikia tu?

7.Huu mhimili huu umekaa kimya miaka yote,kamati ya Bomani,kamati ya Lau,kamati ziliundwa zaidi ya tatu kabla ya hii,ripoti mbali mbali zimetoka zikithibitisha uporwaji wa mali zetu,huu mhimili ulikuwa unatazama tu,nakumbuka baada ya mto Tigithe kumwagiwa sumu,kamati ya viongozi wa dini iliinda timu ya wataalam kuchunguza kama kweli mto tigithe ulichafuliwa na sumu kutoka Barrick,ripoti ilitoka,ikathibitisha kuwa mto ulichafuliwa na sumu,huu mhimili kimyaaaaa,haukuwahi hata itumia tafiti hiyo kusaka haki ya waathirika wa sumu za Tigithe!.

8.Ni mhimili huu huu ndiyo ulitunga sheria ya sisi kupata mrahaba/mrabaha wa asilimi 4 tu,ni hawa hawa walipitisha sheria hii,sasa wanataka tuwaamini kwa lipi?

Mhimili huu ujitafakari unapojadili mambo mazito ya nchi hii,ujipime uzalendo wake,ujipime uwezo wake kuisimamia serikali,ujipime uwezo wake kuwawakilisha watanzania!.

Huu mhimili huu?any way!usiku mwema!.

Dotto Bullendu.
Ndugai ni darasa la saba amefanya kuunga unga elimu, elimu ya kuunga unga!
 
Kuwa na bunge bovu kama hili bora mihimili ibaki miwili tu.
Unamfukuza mnyika wakati sgeria mulitunga nyinyi na muliipitisha kwa "NDIOOOOO" nyinyi,wapinzani kila wanachoshauri munapinga,mahayawani waheed.
 
Kila siku huwa nasema hivi :-

Hatuna bunge, bali tuna "Baby Care Centre" ya kunywa chai ya maziwa ya NIDO na Nescafe.
Baadaye , wanajizungusha Kwenye viti usingizi unawachukua, akishituka toka usingizini, anaangukia kwenye kiitikio cha ndiyooooooooo!

Pia, lile bunge na wabunge wote ni wafanyakazi hewa wa kwanza kabisa hapo Tanzania .

Wajitathimini , waji-assess kisha waachie nafasi zao bila kuchelewa!!

Maana hii , TMAA yote ilijifunza na kuelewa kuwa bunge akili zao zote ni posho tu na mishahara mizuri basi wakawa wanawachomekea vimeo kisha "Baby care Centre' inaitikia kwa kibwagizo cha ndiyooooooooo "

Sasa ukitaka Kufahamu kuwa bunge akili zao zote ni posho tu na mishahara mizuri , hebu gusa hela zao au maslahi yao binafsi, wote ghafula akili zinawarudi wanakuwa timamu.

Ni sawa na watoto, ukiwa unawapa chai, mkate na Blueband, siku ukisema leo mtakunywa uji bila kutiwa sukari , yaani hadi mtoto ambaye hajawahi kuongea neno, siku hiyo utamsikia akipiga kelele. Ndiyo sawa kabisa na hilo mnaloliita bunge hapo Tanzania.

Bunge ili hili, lina watu, wa KKK /RRR , wanaosema wataroga ng'ombe , waziri anainuka anasema, ukiwa na vyerehani vinne (4) hicho tayari ni kiwanda, wanaosema vijana wajiajiri, huku wao wamekuwa wabunge tangu nazaliwa hadi leo mbona hawajaenda kujiajiri!? Awa hawa, wanaopiga wapinzani wao majimboni mwao tena ndani ya chama kimoja, Kama mtu anayeua nyoka!?
Ndiyo hilo mnalolisema eti bunge!,

Bunge, Bunge liwe Tanzania!?
Aiseeeeh, tuache utani kabisa.

Laiti kama ningekuwa, Rais Dr. Magufuli bunge ningelivunjilia mbali nikabakia na mahakama na taasisi ya urais tu.
 
Nchi hii ina safari ndefu sana kwa kuwa na wabunge kama akina msukuma itatuchukua karne kuja kuwa nchi ya viwanda.
 
Back
Top Bottom