Ana mtoto wa miezi minne na wiki 3. Anahisi amepata ujauzito ananiuliza afanyeje nasita nimshauri lipi hasa kwa afya yake

Hebu upandishe huo Uzi wake hapa niuone mkuu
 
Mkuu punguza hasira kidogo. Haya ni makosa ya kiufundi na kama utatafakari vizuri nimakosa yakawaida na yapo tuu. Hapa ndio ishakuwa ivo maana binafs mim natumia kondom pekee kama njia ya kuzuia mimba na hayo mengine yakumharibu mtoto binafsi siya amini maana hayajawahi kuthibitishwa kisayansi zaidi ya kuongelewa tuu. Nilipo kuwa mdogo niliamini hayo lakini sasa nimekua naona watu wanazaa na wake za watu na mtoto anaishi na baba asiye kuwa wakwake na anakuwa na afya tele
 
Asante mkuu.
 
Kiswahili tuu mkuu. Tulipeana mapenzi mubashara na si ngono zembe
 
Jumapili ya aina yake. Tumekubali makosa tutalea mimba na mungu akijaalia mtoto wa kike itakua furaha zaidi na akija wa kiume tena basi yote ni heri nitampokea kwa shangwe zote
 
Kweli... Kweli nakubali mkuu.. Hata mimi ilibidi nitolewe miaka 25+ iliyopita huko.. Maza alikaza sana... Kwa sasa anajivunia mimi
 
Sasa mkuu utatumia mipira mingapi..
 
Nimeumia sana kusoma uzi huu na majibu mengi uliyopewa. Sidhani hata itaweza kuyachambua yote kujua mema na mabaya. Kwa kukusoma tu, nadhani weye utakuwa mkristu. Sasa unaijua amri ya 7 ya Mungu inasemaje? "Usiue". Wewe wataka kuua?? Jiulize, nadhani wakati wazazi wako wanakupata Labda kulikuwa hakuna JF kwa hivyo babako hakupata mahali pa kuulizia ushauri. Je, angeliamua kukuua ka weye unavyotamani kumuua huyo mzaliwa wako leo ungekuwepo??
Ushauri wangu; Lea kijacho huyo. Hujui atakuja kuwa nani. Aweza kujakuwa ndiye msaada wako baada ya hao wengine kutoweka. Watoto 2 tu sio mtaji
 
Kweli... Kweli nakubali mkuu.. Hata mimi ilibidi nitolewe miaka 25+ iliyopita huko.. Maza alikaza sana... Kwa sasa anajivunia mimi
Naomba Mungu anijaalie maisha marefu nije nimsimulie haya mwanangu
 
Mkuu nilishafanya maamuzi na nimeshakutana na daktari amesema mtoto anaweza kuendelea kunyonya hadi miezi mitatu kabla mdogowake hajazaliwa hivyo hatuna mpango wa kuua
 
Mkuu nilishafanya maamuzi na nimeshakutana na daktari amesema mtoto anaweza kuendelea kunyonya hadi miezi mitatu kabla mdogowake hajazaliwa hivyo hatuna mpango wa kuua
Ubarikiwe saana kwa uamuzi muruwa kabisa. Tena huyo ndiye rais ajaye. Jambo la pili, huyo dakitari amekufundisha mambo ya kitabuni tu. Tuulize sisi tunaolea vitukuu. Mtoto anaweza kunyonya hadi wiki 2 tu mamake aende kujifungua. Umlishe mamake vizuri ili apate nguvu ya kulea kijacho na kumnyonyesha mtoto.
Pia, hata akimwachisha kwa kitambo kidogo, akiisha kujifungua na kijacho akapata maziwa ya kwanza "Colostrum" ambayo ni muhimu sana kwa kijacho basi mwenzake akipenda kuendelea kunyonya mpeni maziwa. Wapo wamama ambao wana uwezo mkubwa kutoa maziwa tosha na ziada. Kama huyo mama ana uwezo huo, mlishe vizuri anyonyeshe wawili.
Faida ya maziwa ya mama ni kuwatolea ma genius.
 
Nimeongea na Bi mkubwa aliniambia kitu hicho kuwa mtoto aliyepo ata punzika kunyonya miezi mwili kabla ya mdogo wake na baada ya miezi mwezi atakapo jifungua ataendelea na mdogo wake ake
 
Kawaida mwanamke akijifungua salama anaweza anza kushiriki tendo baada ya muda gani ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…