Ana mchumba wake lakini anataka nimpe mimba

Ana mchumba wake lakini anataka nimpe mimba

mzee wa kasumba

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
1,440
Reaction score
2,963
Habari zenu / Shikamooni / Assalaam alaykum / Bwana asifiwe

Poleni na changamoto za kupambana na CORONA, lakini maisha yanatakiwa yaendelee kwa jitihada tofauti na nawausia msisahau kuchukua tahadhari ikiwemo KUPIGA NYUNGU walau kutwa mara tatu.

AMA BAADA YA SALAMU:-

Najua kwa haraka haraka unaweza ukasema kuwa mimi ni boya kwa sababu ya kuleta mada hii. lakini ifahamike kuwa suala hili limenibidi kutafakari mara mbili na hatimaye kuomba ushauri kabla ya maamuzi.

Huyu bint sikuwa najua kama ana mchumba na alinambia kuwa hana mtu, mzee baba nikawa najipigia mambo. Lakini tangu mwaka huu umeingia kuna jambo moja nilimfanyia kumbe kwake lilikuwa la thamani sana. (Sikuwa najua hili)

Leo akanitafuta na akaomba nikiwa na utulivu tuongee kwa kina. Basi nikalazimisha kupata utulivu ili kujua nini kinamsibu. Kiukweli nikwamba alinambia kuwa ana mchumba na anataka kufunga naye ndoa. Na aliomba msamaha kwa kutonijulisha lakini kwakuwa sikumuweka sana moyoni sikuwaza.

Lakini aliomba nimtie mimba na iwe kama kumbu kumbu kwake, alisema kuwa tukutane siku chache kabla ya harusi yake na akishajihakikishia kuwa ana mimba yangu ndio afunge ndoa na huyo bwana. Mshkaji inasemekana kuwa pesa ipo....

Suala hili sikumjibu moja kwa moja kwanza sijui ni kutokana na ufinyu wa akili yangu lakini nikaona ni bora nije kwa ma GREAT THINKER angalau naweza kupata mwangaza walau kidogo.

Maana kila nikiaa nawaza haya.

1. Kwanini alinificha na hakusema kuwa ana mchummba?
2. Kama ananipenda kwanini asiseme nimuoe mimi?
3. Nikimfikiria mwwanaume mwenzangu naona sitomtendea haki katika ndoa yake pale atakapomshkuru Mungu kwa kupata mtoto.

Swali kwenu wakubwa ni upi uamuzi wa busara hapa?
 
VITA DHIDI YA UKIMWI NI NGUMU MNOOOOO AFU MKUU TURAHISISHIE UPATIKANAJI WA VIPIMO VYA DNA HALI NI MBAYA WATU WANALEA WATOTO SIO WAO
 
Nikaandika humu, ukikutana na Ukaoa mwanamke BIKRA , unakua na uhakika kua "Mtoto wa kwanza ni wako"




Sasa nyinyi wanawake ,ivi kweli hata kama umefanyiwa uzuri wa aina gani.. Ndo udiriki kabisa kumfanyia ubaya wa aina hii mwanaume unayeenda kuzeeka naye?.




Jamaa wee piga tu kwa maana Mwanamke mpumbavu ndio abomoaye nyumba yake.... Piga sababu hajaolewa kwaiyo ule msemo wa ndoa iheshimiwe na watu wote haukuhusu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesoma kwa makini sana uzi wako ushauri wangu kwako; kwa kuwa ashakutamkia kuwa ana mchumba na soon anafunga nae ndoa basi muone kama mke wa mtu vile heshimu ndoa ya jamaa ,utendee haki pia moyo wako, chakujifariji hakuna kipya kwa huyo mwanamke so funga hesabu kwa faida sio hasara

Inauma sana kuwa sperm donor mwsho wa siku mtoto akizaliwa atakuwa c wako utaumia sana cku moja usoni ukiamua kumtia mimba huyo mwanamke.

My take: move on na maisha yako mapya kabsa bila touch na huyo mwanamke.

Asante
 
mmmmmmhhh kaa mbali kaka..mimi ni kama mjuvi na muhanga wa hayo mambo..hakutakuwa na mwisho mzuri...mwishowe wasije kuku rarua marinda bureee kijana wa watu
 
[QUOTE="Pennstatepro, post: 35251636, member: 575663"
Nimesoma kwa makini sana uzi wako ushauri wangu kwako; kwa kuwa ashakutamkia kuwa ana mchumba na soon anafunga nae ndoa basi muone kama mke wa mtu vile heshimu ndoa ya jamaa ,utendee haki pia moyo wako, chakujifariji hakuna kipya kwa huyo mwanamke so funga hesabu kwa faida sio hasara

Inauma sana kuwa sperm donor mwsho wa siku mtoto akizaliwa atakuwa c wako utaumia sana cku moja usoni ukiamua kumtia mimba huyo mwanamke.

My take: move on na maisha yako mapya kabsa bila touch na huyo mwanamke.

Asante
[/QUOTE]

Nimekulewa Sana . Shukran
 
Back
Top Bottom