AN OLD FOX IS NOT EASILY SNARED; Bilal kuzindua vitabu vya Mzee Makamba! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

AN OLD FOX IS NOT EASILY SNARED; Bilal kuzindua vitabu vya Mzee Makamba!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiganyi, May 21, 2012.

 1. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  [​IMG]Yusuph Makamba
  Makamu wa Rais Dokta MOHAMMED GHARIB BILAL Jumapili ijayo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Uzinduzi wa Vitabu Viwili vilivyotungwa na Katibu Mkuu Mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi-CCM Mzee YUSUF MAKAMBA. Uzinduzi wa Vitabu hivyo ambavyo ni Binadamu na Kazi pamoja na Ukweli utafanyika katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa pia na wananchi, viongozi mbalimbali wakiwemo wa Chama, Dini na serikali.


  Akizungumza na mtandao huu wa Francis Godwin Mzee Wa Matukio Daima Mtunzi wa Vitabu hivyo Mzee MAKAMBA amesema tayari Kitabu chake cha Kwanza kinachoitwa Makatazo ya Rushwa kilichozinduliwa na Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa FREDIRICK SUMAYE, serikali imetoa ruhusa kitumike kufundishia shule za msingi kuanzia Darasa la Tano hadi la Saba.


  Pamoja na mambo mengine Mzee MAKAMBA amesisitiza kuwa katika Vitabu hivyo viwili kuna maudhui pia ya Masuala ya Dini ambayo yanahimiza nidhamu ya kazi kwa wananchi kwa kufanya kazi kwa bidii.


  Kuhusu uwajibikaji wa kazi, amewaomba wananchi kutokubali kurubiniwa na baadhi ya wanasiasa kwa kufanya mandamano barabarani na badala yake amewataka kufanya kazi kwa bidii ili kuisaidia serikali kufikia malengo iliyojiwekea.

  sosi; Fransis Godwin!
   
 2. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,015
  Likes Received: 2,666
  Trophy Points: 280
  Hiyo ndio kazi ya makamo wa rais yeye na sherehe/uzinduzi baaaasi ndio kazi anazoweza.
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Ningeshukuru kama viongozi au wafanyakazi ngazi za juu serikali mara wanapoondoka kazini wanaandika vitabu vinavyoeleza mambo yalikuwaje. Kwa mfano ningetaka kusikia toka kwa Mzee Makamba process ya election ilikuwaje, how they made it, critical moments during the campaign period, walifanyaje, walitarajia nini, na matekeo yalikuwa kama walivyotajia? na nini mtazamo wake juu ya future ya CCM na siasa kwa ujumla.

  Haya mambo mengine ya kusema watu wasiandamane ni kuturadharau sisi watanzania. Watu wazima wanatoka majumbani mwao, wanaancha shughuli na kwenda kwenye maandamano kwa sababu kuna jambo linawasumbua. Kusema wanapata msukumo toka kwa wanasiasa ni sawa na kusema kuwa watanzania hawana utashi wa kufanya maamuzi jambo ambalo si sahihi.

  Bado Mzee Makamba ni kijana hivyo nategemea atutapa inside thinking ya CCM wakati akiwa katibu.
   
Loading...