Amuua mwanawe wa kiume kwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja

Poker

JF-Expert Member
Oct 7, 2016
5,305
14,194
Katika hali isiyokuwa ya kawaida kabisa na ya kusikitisha mkazi mmoja wa Ndola huko Zambia amemuua mwanawe wa kiume kwa kumwekea sumu kwenye chakula.

Hiyo ni baada ya mwanawe wa kiume kuja kumtambulisha mpenzi wake wa kiume kwa baba yake, ambaye hakutaka kabisa kukubaliana na ukweli wa mambo hivyo aliagiza waandaliwe chakula cha jioni ndipo alipomuwekea sumu kwenye chakula na kupelekea umauti wa mwanawe huyo wa kiume.

Kwa sasa baba mtoto huyo ametorokea nchini Congo ambako anaishi mafichoni.

Hii si haki kabisa na sisi kama watetezi wa haki za kibinaadamu tunalaani vikali kitendo cha huyo baba kumua mwanawe.

Kila mtu ana haki sawa hapa Duniani na tujifunze kuheshimu maamuzi ya mtu hata kama yanatuumiza.

Na haswa upande wa hisia za watu. Kuua mtu sio suluhisho la kutatua tatizo tuangalie njia bora sisi kama walezi na wazazi.
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida kabisa na ya kusikitisha mkazi mmoja wa ndola huko Zambia amemua mwanawe wa kiume kwa kumwekea sumu kwenye chakula. Hio ni baada ya mwanawe wa kiume kuja kumtambulisha mpenzi wake wa kiume kwa baba yake, ambaye hakutaka kabisa kukubaliana na ukweli wa mambo hivo aliagiza waandaliwe chakula cha jioni ndipo alipomuwekea sumu kwenye chakula na kupelekea umauti wa mwanawe huyo wa kiume. Kwa sasa baba mtoto huyo ametorokea nchini Congo amabako anaishi mafichoni.
Hii si haki kabisa na sisi kama watetezi wa haki za kibanaadamu tunalaani vikali kitendo cha huyo baba kumua mwanawe. Kila mtu ana haki sawa hapa Duniani na tujifunze kuheshimu maamuzi ya mtu hata kama yanatuumiza. Na haswa upande wa hisia za watu.
Sina hata cha kusema
 
Umefirwa mara ngapi?
Mungu aliyekataza ufiraji na ufirwaji ndiye aliyekataza uzinzi, uasherati, usengenyaji, kuhukumu wengine, ulafi, ubinafsi, uchoyo, na kuabudu sanamu.

Hebu niambie kwa nini hao wengine wanaotenda dhambi zilizokatazwa na huyo Mungu mbona hawauawi? Mbona hawatengwi na jamii? Tuache double standard. Kuna njia nyingi za kuwabadilisha wenye shida kama huyo kijana na siyo kumuua.

Kama alichofanya ni halali mbona huyo mzazi kakimbia na sasa anaishi kama digidigi? Nafsi yake inamsuta kwa mauaji aliyofanya
 
Back
Top Bottom