Amuua babu yake akimtuhumu kumuibia solar panel

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Jeshi la Polisi mkoani Pwani linamshikilia mkulima na mkazi wa kijiji cha Mafumbi, kata ya Chole, wilayani Kisarawe, Gale Salaho, kwa tuhuma ya kumuua babu yake Haima Nasri.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa, alidai mtuhumiwa huyo alitekeleza mauaji hayo kwa kutumia sime.

Alidai tukio hilo lilitokea Agosti 24, mwaka huu, majira ya saa 11:00 jioni katika kijiji cha Mafumbi.

"Chanzo cha mauji hayo ni kumtuhumu marehemu babu yake kumuibia solar panel," alisema.

Kamanda Nyigesa alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Kituo cha Afya Chole kwa ajili ya uchunguzi zaidi na mtuhumiwa anashikiliwa kwa mahojiano na kwamba upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.

Chanzo: Habari Leo
 
Marehemu wengine wanavitafutaga vifo wao wenyewe.

Hapana vifo vingine Ni kwa sababu maisha yamekaza hivyo mtu akizinguliwa kidogo anamalizia machungu yote aliyonayo....

Vifo vya mauaji siku hizi Ni visa vinavyoweza kuvumilika....
 
Back
Top Bottom