ARUSHA: Amuua kaka yake na kumjeruhi mama yake kwa kisu, akikataliwa kupika

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Kijana, Adael Willbad (21) Mkazi wa kitongoji cha Upendo katika kijiji cha Manyire wilaya ya Arumeru ,Mkoani Arusha amemuua kaka yake kwa kisu na kisha kumjeruhi mama yake mzazi,Editha Vavoiyo kwa kisu katika ugomvi wa kugombea jiko la kupikia baada ya kukatazwa.

Tukio hilo la aina yake limetokea jana majira ya saa 1.30 jioni nyumbani kwa familia hiyo mara baada ya kuzuka mzozo baina ya marehemu ,aliyefahamika kwa majina ya Ezekiel Willbard (24) na mdogo wake(Mtuhumiwa)wakigombea jiko la kupikia.

Akithibitisha tukio hilo mwenyekiti wa kijiji cha Manyire,Evarest Mallya ,alisema kuwa chanzo cha mzozo huo ulitokana na wanandugu hao kugombea sehemu ya kupikia ambapo mama yao mzazi aliwakataza na kuwaambia wakatafute sehemu nyingine ya kupikia kwa sababu jiko hilo ni mali yake.

"Baada ya kuona mzozo unazidi kuwa mkubwa mama yao aliamua kuchukua uamuzi wa kumwagia maji katika jiko hilo ili wote wakose"alisema

Alisema kitendo hicho kilimkera mtuhumiwa ambaye alichukua kisu na kumjeruhi mama yake tumboni ambaye alianguka chini,tukio ambalo lilishuhudiwa na kaka yake (marehemu)

Mwenyekiti alieleza kwamba baada ya marehemu kushuhudia mama yake amechomwa kisu na kudondoka chini aliingia ndani na kuchukua chuma ili kumpiga mdogo wake ,lakini wakati akitoka nje hakumwona kwa kuwa alikuwa amejificha.

"Marehemu aliamua kumfuata mama yake na kujaribu kumwinua lakini wakati akielekea eneo hilo ghafla mtuhumiwa alitokea ghafla mafichoni na kumchoma kisu cha ubavuni kushoto na kuanguka chini "alisema

Mwenyekiti alisema kuwa mtuhumiwa alimburuta na kumficha marehemu kwenye shamba la mahindi kando ya nyumba yao hadi kesho yake watoto wadogo waliokuwepo nyumbani walipouona mwili wa kaka yao ukiwa shambani akiwa amepoteza maisha.

Alisema mtuhumiwa huyo alijaribu kutoroka lakini wananchi walifanikiwa kumkamata katika eneo la Gomba alikokuwa amekimbilia kujificha.

"Baada ya kufanikiwa kutoroka alienda katika kituo cha polisi Chekereni na kutoa taarifa kwamba kaka yake amemchoma kisu mama yake na sisi baada ya kupata taarifa tulianza msako wa kumtafuta na kufanikiwa kumkamata akiwa eneo la Gomba wilayani Arumeru amejificha na tulimpeleka katika kituo cha polisi ambako hadi sasa anashikiliwa "alisema

Mama alikombizwa katika hospital ya Mt Meru ambako amelazwa akipatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa na kisu tumboni, na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha maiti katika hospitali ya Nkoaranga wilayani humo.

Kamanda wa polisi Mkoani hapa ,Justine Masejo hakuweza kupatikana kuzungumzia tukio hilo licha ya simu yake ya mkononi kuita kwa muda mrefu bila kupokelewa.
 
Mhh! Mambo mengine ni mapepo tu, haziwezi kuwa akili za kawaida.

Na hao watu ni either wamasai au wameru… wamasai ni wagomvi wagomvi tu, tena kama hana elimu ndio tafrani.

Niliishi nyumba / boma ya kimasai hapo zamani za kale aisee, mtoto alimzingua mama yake mzazi ni noma’
Guts za kumfokea/ kumpiga mama mzazi unatoa wapi?!!
 
Nimesoma hyo habari adi mwili umesisimka.
Kweli sio mzima huyo dogo
 
Mhh! Mambo mengine ni mapepo tu, haziwezi kuwa akili za kawaida.

Na hao watu ni either wamasai au wameru… wamasai ni wagomvi wagomvi tu, tena kama hana elimu ndio tafrani.

Niliishi nyumba / boma ya kimasai hapo zamani za kale aisee, mtoto alimzingua mama yake mzazi ni noma’
Guts za kumfokea/ kumpiga mama mzazi unatoa wapi?!!
Wameru hao bhna
 
Ukisoma hiyo stori ni kwamba mama nae ni janga... halafu hata marehemu angemkuta mwenzie bado ilikua ni kumuua kwa hicho chuma alichokuwa amefuata.
 
Back
Top Bottom