Mbeya: Amuua mwanafunzi mwenzie kwa shoka baada ya kushindwa kumbaka

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
1662524128978.png

Mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Sinde jijini Mbeya, Faraja Kasole (16), ameuawa kwa kukatwa na shoka shingoni na mwanafunzi mwenzie aitwaye Humphrey Ngogo (17) mwanafunzi wa kidato cha tano shule ya sekondari Iduda, baada ya kushindwa kumbaka.

Chanzo cha mauaji hayo kimedaiwa kuwa ni tamaa za kimwili ambapo mtuhumiwa Ngogo alifanya jaribio la kumbaka marehemu, lakini baada ya kuzidiwa nguvu akachukua shoka na kumpiga nalo kichwani.

East Africa Radio

============

MWANAFUNZI wa kidato cha nne katika shule ya Sekondari Sinde jijini Mbeya, Faraja Kasole ( 16) ameuawa kwa kukatwa na shoka shingoni na mwanafunzi mwenzie aitwaye Humphrey Ngogo ( 17) mwanafunzi wa kidato cha tano Shule ya Sekondari Iduda.

Chanzo cha mauaji hayo kimedaiwa kuwa ni tamaa za kimwili ambapo mtuhumiwa Ngogo alifanya jaribio la kumbaka marehemu lakini baada ya kuzidiwa nguvu akachukua shoka na kumpiga nalo kichwani.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi, Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Ulrich Matei, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba kabla ya tukio hilo, mtuhumiwa alifika nyumbani kwa marehemu ambaye kwa muda huo alikuwa peke yake na kisha kumvamia chumbani kwake kwa nia ya kumbaka na alipozidiwa nguvu ndipo alimua kuchukua shoka na kumpiga nalo.

Kamanda Matei alisema baada ya upelelezi wa jarada hilo unaendelea na mara baada ya kukamilika atafikishwa mahakamani kwa ajili ya hatua nyingine za kisheria ikiwamo mtuhumiwa kuchukuliwa hatua.

“ Jeshi la Polisi linalaani tukio hili kikatili na linatoa pole kwa wazazi na familia ya marehemu, hata hivyo tunatoa rai kwa wazazi au walezi kujenga tabia ya kuzungumza na watoto wao kuhusu masuala ya makuzi huku wakisisitiza kujikitiza zaidi kwenye masomo na kuachana na tama za kimapenzi wangali masomoni ili kujiepusha na matukio kama hayo,” alisema Kamanda Matei.

Katika hatua nyingine Kamanda Matei alisema wanamshikilia, mfanyabiashara Mabula Mabhembe (35) mkazi wa kijiji cha Ifumbo wilayani Chunya kwa tuhuma za kuuza dawa za kulevya aina ya bangi katika duka lake la kuuza bidhaa za nyumbani.

Alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa Septemba 5 mwaka huu majira ya saa 11 jioni akiwa na magunia matatu yenye ujazo wa kilogramu 20 , misokoto 3500 pamoja rizla boksi mbili ndani ya duka lake.

Aliongeza kuwa mtuhumiwa alikiri kufanya biashara ya kuuza dawa hizo za kulevya kwa kushirikiana na mtuhumiwa mwingine aitwaye Hamis Shauritanga ambaye anaendelea kutafutwa na Jeshi la Polisi.

“Tayari tumemkamata mtuhumiwa mmoja kuhusiana na tukio hilo bado mwingine ambaye tunamtaka popote alipo ajisalimishe kituo cha Polisi, lakini natoa rai kwa wananchi kwa yeyote mwenye taarifa za mahali alipo asisite kuzitoa ili akamatwe na kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria,”

Kwa mujibu wa maelezo ya Mjomba wa marehemu, Sauli Mwaisenye alisema maziko yalifanyika Septemba 4 mwaka huu katika makaburi ya Iyela jijini Mbeya na kwamba familia inaomba vyombo vya maamuzi kutenda haki.
 
So sad, masterbation Ni suruhisho kwa vijana wa kiume waliokatika umri huo,huo umri kumpata binti Ni kazi sana ,Tena inahitaji kijana mwenye uwezo wa kujenga hoja kwa binti Hadi amuelewe,ona Sasa kamwaga damu isiyo na hatia kwa Jambo la sekunde 5 baada ya hapo unaanza kujutia.
 
Kuna watu watkuja kusema balehe inawasumbua lakini kwa nia njema kabisa Serikali ipunguze umri wa mtu kutambulika Kama mtoto kisheria kutoka miaka 18 mpaka miaka 14 kwa Sababu kijana wa miaka 14 ana uelewa na utimamu wa kutosha kabisa kujua anachofanya ni kosa au si kosa?

Yaani jitu la miaka 17 kabisa linaenda kutambulika kama mtoto na atastakiwa kama mtoto...this is insane. Ifike mahali tuwe na huruma na hao watendewa. Furaha yangu ni kuona mtu huyo anafungwa maisha na kazi ngumu za mateso makali
 
Mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Sinde jijini Mbeya, Faraja Kasole (16), ameuawa kwa kukatwa na shoka shingoni na mwanafunzi mwenzie aitwaye Humphrey Ngogo (17) mwanafunzi wa kidato cha tano shule ya sekondari Iduda, baada ya kushindwa kumbaka.

Chanzo cha mauaji hayo kimedaiwa kuwa ni tamaa za kimwili ambapo mtuhumiwa Ngogo alifanya jaribio la kumbaka marehemu, lakini baada ya kuzidiwa nguvu akachukua shoka na kumpiga nalo kichwani.

East Africa Radio
Madogo ngono inawatesa
 
Akikaa rumande mbona itafika tu hiyo miaka 18
 
Kushutakiwa kama mtoto hakutapunguza adhabu yake sema akihukumiwa hatachanganuwa na watu wazima jela mpaka afikishe umri wa miaka 18.
 
Mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Sinde jijini Mbeya, Faraja Kasole (16), ameuawa kwa kukatwa na shoka shingoni na mwanafunzi mwenzie aitwaye Humphrey Ngogo (17) mwanafunzi wa kidato cha tano shule ya sekondari Iduda, baada ya kushindwa kumbaka.

Chanzo cha mauaji hayo kimedaiwa kuwa ni tamaa za kimwili ambapo mtuhumiwa Ngogo alifanya jaribio la kumbaka marehemu, lakini baada ya kuzidiwa nguvu akachukua shoka na kumpiga nalo kichwani.

East Africa Radio
Ugwaduuuu ugwaduuu ni balaa
 
Back
Top Bottom