Shoctopus
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 3,434
- 1,985
Baada ya kusikia amri ya RC Makala kwamba office zote za serikali za mitaa jijini Dar ziajiri Mgambo kama walinzi ninayo machache yanahitaji ufafanuzi:
Pia soma > RC Makalla: Kuanzia sasa Ofisi zote za Serikali za Mitaa jijini Dar zitalindwa na askari wa kikosi cha Mgambo
Kwanza amri ya RC Makala akiwa MKUU WA MKOA na MWENYEKITI wa kamati ya ulinzi ya mkoa naamini amri yake inatokana na maamuzi ya kamati yake. Na kama hivyo ndivyo inabidi masuala yafuatayo yazingatiwe:
1. Kama ni LAZIMA kila Ofisi ya Serikali ya mtaa iajiri mgambo kama mlinzi wake wa kudumu ni lazima alipwe na Serikali mshahara na posho stahiki.
Kwasababu mgambo ni binadamu anastahili kulipwa kama mwajiriwa yeyote serikalini.
Mwenyekiti na watendaji wengine wa Serikali ya mtaa wote ni watu muhimu wanaofanya kazi kubwa ya kuwahudumia wananchi katika mazingira magumu. Kwamfano wana uhaba wa vitendeakazi, fenicha, gharama za usafiri, umeme nk.
Kama mlinzi hatalipwa na Serikali itakuwa vigumu kwa ofisi ya serikali ya mtaa kumwajiri mgambo kama mlinzi kwa kazi ya kudumu, lakini hata kwa ajira ya muda tu, pia ni vigumu.
Mgambo kama mlinzi lazima alipwe mshahara na posho stahiki na vitendeakazi kama:
i. Sare pea mbili na boots
i. Silaha (bunduki) na vitu vingine muhimu.
Lakini katika mazingira ya serikali za mitaa yanastajili kuwa na ulinzi pote nchini Tanzania, haiwezikani kuwe na ulinzi kwa Dar pekee, kama jambo hilo ni sera ya nchi.
Vile vile kama jambo hilo si sera ya nchi itakuwa vigumu kutekeleza kwa mkoa mmoja tu wa Dar es Salaam.
Suala la ajira kwa Wanamgambo nalo ni suala la kitaifa. Kwasababu wapo mikoa na wilaya zote nchini.
Last but not least! Si lazima kila mgambo awe mwenye vigezo na tabia nzuri kuweza kuajiriwa.
Bila kuwa na mwongozo maalum wa utekelezaji wa jambo hilo huenda likazua matatizo.