Amri ya kufanya mazoezi siku ya mapumziko (J'mosi), nisipohudhuria ni kosa kisheria?

Bornventure

JF-Expert Member
Jan 29, 2017
529
523
Naomba kufahamu kuhusu agizo la makamu wa raisi kutaka watumishi wa umma kufanya mazoezi kila jmosi inakuaje iwapo mi ni mtumishi na sitaki kufanya mazoezi hayo ya amri Na kwa muda huo wa serikali? Ni kosa nsipohudhuria??
 
Naomba kufahamu kuhusu agizo la makamu wa raisi kutaka watumishi wa umma kufanya mazoezi kila jmosi inakuaje iwapo mi ni mtumishi na sitaki kufanya mazoezi hayo ya amri Na kwa muda huo wa serikali? Ni kosa nsipohudhuria??
 
Hajatoa ufafanuzi, Ila kuishi serikali ya matamko kila unachofanya hata kama ni halali kinakuwa kama magendo!
 
Tena hayo mazoezi yatakua na push ups kwa wingi sana na yanafanyika kwa pamoja nje ya jengo la kituo chako cha kazi mapema sana asubuhi.
 
Mungu nipe nguvu

Mungu nipe uwezo nione mengi kwa kweli kila siku mapya

msijekuta Tanzania kuna mdudu kaingia ndani ya vichwa vya ................. hatujui ee
 
Sijapata nafasi ya kumsikiliza wala kufuatilia hii habari kwa kina. Ametoa amri au ushauri?

Kama nna utaratibu wangu wa kufanya mazoezi inakuaje? Wanataka kuleta mambo ya miaka ile mkicheza mpira Kama Una Viatu unaambiwa uvivue. Shule za private wanazishurutisha kubadili mfumo zifanane na za umma japo za private ndio zinaongoza kufanya vizuri.

Serikali itambue mambo mengine binafsi iwaachie wahusika ilimradi sheria na taratibu zisivunjwe.

Mwisho tutapangiwa hadi tule nini..
 
Sio amri. Kuna ufafanuzi ulishatolewa na utumishi kuwa ni hiari kwa mtumishi kufanya mazoezi. Kilichopo wakuu wa vitengo kwa kutaka sifa km kondakta watafanya vikao na kuchakachua mihutasari ionekane idara au kitengo wafanyakazi kwa umoja wao wameridhia mazoezi ni lazima kumuenzi makamu wa Rais.
 
Mazoezi ni kwa faida yako mwenyewe unayo hiari ya kufanya au kutofanya. My advice- fanya mazoezi.
 
Ni amri mkuu. Mkuu wetu Wa idara kapigiwa simu kwamba watumishi wote tunatakiwa kufika ofisi za mkuu wa mkoa saa moja kamili asubuhi siku ya jumamosi kwajili ya mazoezi.

What were they smocking, seriously? Very unacceptable..
 
Kuna mkoa fulani waliambiwa waandike barua za kujieleza kwa nini hawakuhudhuria hayo mazoezi
 
Back
Top Bottom