Ampeleka mumewe polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ampeleka mumewe polisi

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Saint Ivuga, Mar 21, 2011.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,284
  Likes Received: 19,437
  Trophy Points: 280
  Ampeleka mumewe polisi
  [​IMG]
  Thursday, March 17, 2011 10:41 AM
  KATIKA hali ambayo haijazoeleka katika jamii, Fatma Mussa [50] mkazi wa Gongolamboto amempeleka mumewe polisi kwa kuchoshwa na vipigo, kudhalilishwa na matusi kutoka kwa mumewe huyo.Chanzo cha habari hii kilisema kuwa Fatma aliamua kuchukua uamuzi huo baada kuchoshwa na kadhia hiyo na kupewa ruksa na watoto wake baada ya kuchoshwa na kero hiyo.

  Imedaiwa kuwa mwanamke huyo alikuwa akipata kipigo, matusi ya nguoni mara kwa mara kutoka kwa mumewe huyo hali inayomfanya akose amani pindi tu mumewe anapokuwa akirudi nyumbani.

  Imedaiwa kuwa Jana mume huyo alirudi nyumbani hapo akiwa na hasira tele na kujikuta akimpiga mkewe na kumjeruhi maeneo ya usoni na kupelekea kushonwa nyuzi kumi eneo la jeraha.

  Imedaiwa kutokana na hali hiyo watoto waliamua kuchukua uamuzi wa kumshauri mama yao akaripoti tukio hilo kituo cha polisi kwa kuwa walishachoshwa na hali hiyo.

  Imedaiwa kuwa Khalidi [30] aliongoza wadogo zake kwenda kuripoti tukio hilo kwa kuwa walichoshwa na hali ya kuteswa kwa mama yao huyo.

  Hata hivyo imedaiwa kuwa baba huyo alikuwa akimuamuru mke wake huyo aondoke kwao ili aweze kuoa mke wa pili kwa kuwa mke wake alikuwa haafiki maamuzis yake hayo.
  Imedaiwa kuwa Fatma alipinga maamuzi ya kuletewa mke mwenzake katika nyumba hiyo na kumshauri amtafutie nyumba nyingie awatenganishe na si kukaa mahali pamoja.

  Imedaiwa kuwa mume huyo haafiki mawazo hayo na alikuwa akihitaji amlete ndani humo na kumtaka mkewe huyo aondoke kama hataweza kuishi hapo na mke mwenzake

  Imedaiwa kuwa wanandoa hao walibarikiwa kuwa na watoto watatu na walitoa baraka zote kumpa mama yao kuwa akaripoti tukio hilo ili baba yao huyo aweze kuadabishwe kutokana na kuchoshwa na tabia hiyo.

  Mume huyo aliyetambulika kwa jina moja la Farid [59] ni dereva wa kampuni binafsi wa magari makubwa yasafirishayo mizigo yaendayo nchi jirani.

  Muda wowote kuanzia leo mume huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu shtaka hilo linalomkabili.
   
Loading...