PreGE2025 Amos Makalla: Wananchi wa Buchosa msimhukumu mbunge wenu kisa ubovu wa barabara

PreGE2025 Amos Makalla: Wananchi wa Buchosa msimhukumu mbunge wenu kisa ubovu wa barabara

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Wakuu,
Kwakweli hatutakiwi kuwachekea na kuwaonea huruma hawa wabunge, wasiotimiza tunachohitaji wananchi, wanataka tusiwahukumu, ili tuendelee kuteseka huku wao wanateleza na matumbo yao.

====
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM, CPA Amos Makalla, amewataka wananchi wa Buchosa wasimhukumu mbunge wao, Erick Shigongo, kutokana na kutokamilika kwa barabara ya Sengerema- Buchosa, iliyoko Halmashauri ya Buchosa, wilayani Sengerema, mkoani Mwanza.

Makalla ametaja sababu ya kutokukamilika kwa barabara hiyo yenye urefu wa takribani kilomita 53 inayojengwa kwa kiwango cha lami ni kutokana na kazi ya mkandarasi aliyekabidhiwa awali haikuridhisha ndipo alipoondolewa, lakini taratibu za kumpata mwingine zimekamilika.

Akizungumza Mei 21, 2025, na wananchi Halmashauri ya Buchosa, wilayani humo, Makalla aliyeko katika ziara ya kikazi ya siku saba, katika mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza Simiyu na Shinyanga anasema anaifahamu barabara hiyo tangu akiwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

“Barabara Sengerema-Buchosa naomba Erick asihukumiwe nayo ninaijua vizuri, nilikuwa Mkuu wa Mkoa huu nimeshiriki baada ya mkandarasi kuzingua nilisema mkandarasi afutwe kazi ili wizara tupate mwingine.

“Ninajua ni mambo ya kisheria hatimaye ameondoka ninajua Waziri Mkuu alikuwa hapa na Waziri baada ya kupatikana mkandarasi barabara itamalizika,” amesema.

Makalla amesema ameamua kulisema hilo ili isiwe fimbo kwa wanasiasa wengine.

“Tulifanya uamuzi mgumu kwa maslahi ya wananchi wa Buchosa ili barabara isilipuliwe,” amesema.


Chanzo Nipashe
 
Basi wawahukumu halmashauri na Tanroads wanaowapa kazi wakandarasi wabovu.
 
Makala usiwapangie wanaccm nini cha kufanya, wao ndio wanajuwa wanamtaka nanj wa kuwasaidia shida zao.
 
Back
Top Bottom