Amos Makalla kaa chonjo, wamachinga ni jeshi kubwa

Elitwege

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
5,154
10,809
Mkuu wa mkoa mpya wa Dares Salaam bwana Amos Makala mara alipoapishwa tu alitoka mbiombio kwenda kufanya kazi na kero ya kwanza aliyoiona kwenye jiji la Dar es Salaam ni wamachinga kufanya biashara katikati ya jiji!

Licha ya kwamba Makalla alishangiliwa sana na Chadema kwa uamuzi wake huo wa kufukuza machinga, lakini sisi tunaona mbali tulimuonya kuwa wamachinga ni jeshi kubwa hutaliweza.

Leo bwana Makalla amepata salamu kutoka Morogoro baada ya mkuu wa wilaya na Mkurugenzi kufukuzwa kazi kwa kosa la kutuma mgambo kwenda kupiga machinga.

Tukupe ushauri tu bwana Makala kuwa Chadema wanakushindilia uwafukuze machinga wakiwa na malengo yao.
1. Ili wamkomoe mwendazake kwa sababu alijipambanua kama machinga namba moja wa Tanzania.
2. Ili machinga wakikosa kazi basi chadema wataanza kuwanywesha viroba na kuwaandamanisha mitaani.

Makala kama unataka kudumu na u RC wa Dar basi pambana na wauza madawa ya kulevya, wezi wa mafuta bandarini na mafisadi wote ila achana kabisa usiguse wamachinga.

Haiwezekani uajili mgambo uwalipe kwa kodi za wanachi alafu kazi yao iwe kupiga watu wanaojipatia kipato chao halali kabisa bila kuibia mtu yoyote.

Samia = Magufuli.

Mtaelewa tu.

.
20210615_143705.jpg
 
Chadema imeingiaje humu kwenye inshu ya wamachinga!?

Kwa taarifa yako hakuna chama ambacho ni mtetezi wa machinga kama Chadema tangu mwanzo. Wewe inshu ya wamachinga uliidandia tu kama yule mwenzio mwendazake nae aliidandia tu kwa sababu za kisiasa.

Wamachinga ni ajenda ya Chadema tangu enzi na ndio waliowapigania kuwepo mpaka leo.
 
Mkuu wa mkoa mpya wa Dares salaam bwana Amos Makala mara alipoapishwa tu alitoka mbiombio kwenda kufanya kazi na kero ya kwanza aliyoiona kwenye jiji la Dares salaam ni wamachinga kufanya biashara katikati ya jiji...
Kwanini unashindwa kuleta hoja yako hapa Bila kuzitajataja taasisi zilizo kuwa bora, ama una kuwa na hofu nguvu ya hoja zako.
 
Yani wengi watavunjika moyo kushughulikia tatizo la machinga.

Imeshakuwa nongwa!

Sijui hatima ya Dar itakuwaje?!
 
Lakini ni chadema hao hao wanataka wafukuzwe
Ila uzuri nyie ni vigeugeu na wanafiki Sana, punde mlikuwa mnashabibia ubabe na uonevu leo hii mna jidai kuhamia upande wa haki, na kuwaona watetezi wa kweli wa haki ndio wabaya. Acha unafiki huo wa kiwango cha sgr .
 
Ndio wanefukuzwa kazi, Je rais kama rais yeye anaamua nini kuhusu machinga?

Machinga ndio mtaji wake kupata ushindi ama kuonekana anajali wanyonge..

Hilo ni onyo kwa viongozi. Maana yake ukimgasi mmachinga mama anakufukuza kazi.

Maana ameshasema ni wanae.. kasema wanangu wamachinga wa moro.. wamepigwa na mgambo
 
Back
Top Bottom