Amos Makalla awataka majambazi kusalimisha silaha zao mara moja

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,208
4,705
Wadau wa JF

Nawasalimu kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Amos Makalla ameanza kazi kwa kishindo kwa kutuma salaam kwa Majambazi

Mkuu huyo wa Mkoa ambaye amerithi mikoba ya Aboubakar Kunenge aliyehamishiwa Pwani ameagiza kuwa Majambazi wote Mkoani Dat es salaam kusalimisha Silaha zao mara moja

====

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ameliagiza Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam kuhakikisha linawashughulikia kikamilifu Majambazi na Vibaka Jijini humo huku akiwataka kujisalimisha na kukabidhi Silaha zao kwa hiyari.

RC Makalla ameagiza kuanza kwa Operesheni ya kufagia watu wote wanaofanya Vitendo vya uhalifu Jijini humo ambapo amesema ni vyema pia Wazazi wakaanza kuwaonya watoto wao pindi wanapoona Wana mienendo isiyoeleweka.

Aidha RC Makalla amesema kwakuwa uzoefu unaonyesha wahalifu hao hutumia Silaha kujerui na kusababisha vifo, ni vyema Jeshi la Polisi likawawahi kuwashughulikia kikamilifu Majambazi kabla hawajatumia Silaha hizo kujerui na kusababisha vifo kwa Wananchi.

Hata hivyo RC Makalla amewahikikishia Wananchi Usalama na kuwataka kuendelea na majukumu yao Kama kawaida kwakuwa Vyombo vya usalama vimejidhatiti kulinda usalama wao na mali zao.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Camilius Wambura amesema Katika msako ulioanza May 21 adi May 25 wamefanikiwa kuwakamata Majambazi na Vitu mbalimbali ikiwemo magari Manne, Pikipiki moja, Bunduki Moja, Laptop na vifaa vinginevyo.

Aidha Kamanda Wambura amemuhakikishia RC Makalla kuwa maagizo aliyoyatoa wameyapokea kwa mikono miwili na watayafanyia kazi kwa ufanisi mkubwa.
1621948164364.png
1621948216335.png
1621948243008.png
1621948280142.png
1621948312026.png
 
Hii amri haitatekelezwa. Makalla aje na gia nyingine.

Majambazi ya miaka hii yana nguvu kuliko maDC, maRC na mawaziri.
 
No hajachemka,bali kawapa taa nyekundu, watubu warudishe surahs vinginevyo moto utawaka ,ni nafasi nzuri katoa maana jambazi ni binadam anaweza jisahisha,ataki acha moto umuwakie
Jambazi? labda atumie neno wanaomiliki silaha kinyume na sheria anaweza kuwapa mwanya baadhi yao kubadiri mawazo na kuacha uhalifu. Lakini kutamka tu kuwa majambazi wasalimishe silaha amechemka Wasomi wetu wanakwama wapi?
 
Waache utani, kuna viashilia huko tuendako hali ya usalama itadorola. Jana wakati nikifanya mazoezi uwanjani majira ya saa moja jioni nimeona vijana kama sita hivi wakiwa vifua wazi na mapanga wakitukana na kuyaburuza chini, sasa sielewi walikokuwa wanakwenda.
 
Hii amri haitatekelezwa. Makalla aje na gia nyingine.

Majambazi ya miaka hii yana nguvu kuliko maDC, maRC na mawaziri.
MaDC na RC wa wapi?
Hapo ana maana moja tu, wakinashwa hakuna kesi ni pipe kuwatanguliza mbele za haki.

Goo, go Makalla goooo
 
Yaani ni kama kumwambia mkulima asalimishe jembe, atakula wapi ?🤣🤸🐒
 
majambazi hawawezi jisalimisha kwa maneno tu, wafanye operation ya kuwasaka mtaa kwa mtaa wanaotuhumiwa kufanya kazi hiyo
 
Waache utani, kuna viashilia huko tuendako hali ya usalama itadorola. Jana wakati nikifanya mazoezi uwanjani majira ya saa moja jioni nimeona vijana kama sita hivi wakiwa vifua wazi na mapanga wakitukana na kuyaburuza chini, sasa sielewi walikokuwa wanakwenda.
Elewa kwamba si huyu RC wa kwanza fanya Jambo Kama hili ,yapo majambazi yamepigika na yanatafuta jinsi ya kujisalimisha ila yanashindwa, hata hivyo ukipata majambazi sugu wawili wa kujisalimisha na kuwapa ushirikiano wenda mtandao mkubwa utaupata VIZURI ,so RC kwa kifupi yuko VIZURI Sana ,uongozi ni kipaji mkuu,
 
Back
Top Bottom