TUJITEGEMEE
Platinum Member
- Nov 6, 2010
- 27,583
- 28,628
.....mwakalebela leo kasema kuwa serikali imewaambia waitishe mkutano ili wajadili katiba mpya au wafanye uchaguzi kwa katiba ya zamani .....
#MauozoYaTFF
Kwamba Amos Makala ni waziri Tanzania is enough reason ya kutufungia...
Kama wamekataa ushauri huu basi akina Tenga ni wakorofi.
wewe ni ***, unaamini fifa wameskia kupitia vyombo vyetu ya habari?
Sio mbaya tukifungiwa hata miaka 5 mbele,tukifunguliwa hawa wanaong'ang'ania watu wao watakuwa washachoka,na nchi itakuwa ishajipanga kisoka,tutasonga kivingine,wakati huo huo ligi yetu ya ndani inaendelea
... Katiba mpya ya TFF ilipitishwa by resolution ya wajumbe wote husika sasa serikali inataka ijadiliwe upya kwa lengo gani?
........
Nasikia anataka kutumia mambo ya siasa pia ili kuishawishi serikali nzima ikubaliane na matakwa yake kisa TENGA ni mwanachama muanzilishi na muandamizi wa chadema!
Angalizo:Tusichanganye mpira na siasa kwa mtego wa Amos Makala,jk mmulike huyu jamaa yako.
Kusajili katiba haitoi fulsa kwa serikali kuingilia uendeshaji wa vyombo vilivyosajiliwa kwa namna serikali inavyoingilia TFF kuamrisha wala sio kushauri
Ingewashauri walalamikaji kuchukua hatua zinazostahili na wala sio kutuo amri na altimatums. Ziko associations nyingi zinaanza kufuata katiba zao baada ya kupitishwa na vikao halali za vyama husika na baadae kusajili. Kwa nini TFF tu ndio iingiliwe jikoni.Maswali ya kujiuliza ni haya
1.je FIFA wanaruhusu katiba zao zisajiliwe na serikali ili zianze kutumika?
2. Katiba mpya ya TFF ilianza kutumika kabla haijasajiliwa kwa sababu ya kukimbizana na muda je TFF wamewaambia fifa kuhusu hicho?
3. Serikali kama wamegundua kuwa tff wamefanya makosa ya kisheria za nchi na kuwaambia wafuate sheria za nchi huko ni kuwaingilia?.
Eti bwana!!!.. Kwa kuwa mfanyabiashara Malinzi hakupitishwa kugombea?TFF hawana ulazima wa kufuata ushauri wa serikali kwani mambo ya mpira wa miguu yana miiko yake iliyoasisiwa na FIFA na TFF ni signatory!! Katiba mpya ya TFF ilipitishwa by resolution ya wajumbe wote husika sasa serikali inataka ijadiliwe upya kwa lengo gani?
TFF kufuatana na FIFA hairuhusu mambo yake kupelekwa mahakamani ila kusuluhishwa na kamati za usuluhishi za ndani. Sasa wakitupwa nje kugombea kwa kukiuka kanuni wanakimbilia serikalini.Pia tukumbuke kuwa pamoja na Serikali kutoa maelekezo kwa TFF, kuna kesi mahakamani za kuzuia uchaguzi baada ya wadau kutoridhishwa na mchakato wa uchaguzi.
kama ni hivyo basi waonyeshe muhitasari/minutes za kikao kilichohusisha wajumbe wote na kupitisha hiyo katiba....ili tuone kama kweli serikali ndiyo korofi
Mkuu nadhani huna uelewa wa maana ya kupitsha maamuzi kwa njia ya RESOLUTION; wahusika wanapotoa uamuzi kwa njia hiyo, huwa hakuna kikao bali makabrasha husika hupelekwa kwa wajumbe na wao huafiki au hukataa kufuatana na ajenda husika!! Kuhusiana na na katiba ya TFF, wajumbe wahusika waliipitisha kwa mtindo huo na hivyo ndivyo maamuzi mengi duniani hufanywa bila ya wahusika kukutana!!