Elections 2010 Amkeni wanachama wa CCM- Kura zenu za maoni hazina nafasi kwenye kuamua nani agombee.

Shadow

JF-Expert Member
May 19, 2008
2,897
671
Amkeni wanachama wa CCM- Mfumo wa Kupiga Kura umekaa kitapeli

Kwanza natoa shukrani kwa MM kwa kuleta hoja ya msingi na sasa ni Wakati wa kuwaamsha makada,wanachama wa CCM kwamba huo mfumo wa kupendekeza wanachama wanaowapenda ni upotezaji wa muda, rasilimali na kuchezeana akili. Mfumo asilia wa upitishaji wa wagombea bado hupo pale pale ni bora siku hiyo mtumie muda huo kwenda kujenga taifa au kutembelea mayatima au wagonjwa mahospitalini au ata kushiriki kwenye harambee za ujenzi wa taifa. It is a shady process…ni mchakato wa kitapeli….mwisho wa siku mtavunjwa mioyo yenu kwani wapiganaji wa kweli watapigwa panga kwenye vikao vya 'kujadili na kutangaza matokeo'

Wakatabahu,

Shadow.

EBU SOMA HAPA KISHA TAFAKARI KAMA MUDA WAKO , KURA YAKO INA NAFASI YOYOTE NDANI YA VIKAO VYA 'NDANI' VYA CHAMA CHENU!



MCHAKATO WA UTEUZI WA WAGOMBEA UBUNGE NA UWAKILISHI WA MAJIMBO:

(i) Tarehe za Kuchukua na Kurudisha Fomu ndani ya Chama
NAFASI YA UONGOZI
KUCHUKUA FOMU
KURUDISHA FOMU
Ubunge
19/07/2010
21/7/2010

Uwakilishi
19/07/2010
21/7/2010




(ii) Mchakato wa Uteuzi wa wagombea Wabunge/Wawakilishi (Majimbo) – ndani ya Chama


TAREHE
TUKIO
21/7/2010
Mara baada ya muda wa kurudisha fomu kumalizika saa 10 jioni, Kamati za Siasa za Wilaya zitafanya mikutano ya pamoja na wagombea wao wa nafasi za Udiwani, Ubunge au Uwakilishi, waliorudisha fomu; kwa madhumuni ya kujadili na kuafikiana juu ya ratiba na vituo vya mikutano hiyo; michango ya usafiri wa pamoja wakati wa mikutano ya kampeni; na kukumbushana juu ya umuhimu wa kila mgombea kuzingatia maadili ya Chama Cha Mapinduzi na miiko ya uchaguzi wa ndani ya Chama chetu.

22 - 31/7/2010
Kipindi cha Mikutano ya kampeni ya wagombea
Ubunge/Uwakilishi na Udiwani.

1/8/2010
Siku ya Upigaji Kura za maoni kwa wagombea wote katika Matawi.

2-3/8/2010
Kuandaa matokeo kwa ajili ya vikao.

5-6/8/2010
Kamati za Siasa za Wilaya kuwajadili wagombea Ubunge/Uwakilishi na Udiwani.


Kabla ya kuanza agenda ya kuwajadili wagombea, Kamati za Siasa za Wilaya zitafanya mikutano ya pamoja na wagombea wao waliopigiwa kura za maoni, kwa madhumuni ya kukubaliana juu ya suala la kuvunja makundi ya wagombea hao ili kuimarisha umoja na mshikamano ndani ya Chama chetu.

7/8/2010
Kamati za Siasa za Mikoa kujadili na kutoa mapendekezo kwa Kamati Kuu kuhusu wagombea wote.




Ngazi ya Taifa

TAREHE
TUKIO
9/8/2010
Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa Zanzibar, kuwajadili wagombea Ubunge/Uwakilishi wa Majimbo na Viti Maalum Wanawake.

10-11/8/2010
Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa.

12-13/8/2010
Kamati Kuu kupendekeza wagombea Ubunge/Uwakilishi.

14/8/2010
Halmashauri Kuu ya Taifa kufanya uteuzi wa mwisho wa wagombea Ubunge/Uwakilishi wa Majimbo na wa viti maalum.

Tarehe za kuchukua fomu za Serikali zitatangazwa na Tume za Uchaguzi.





(3) MCHAKATO WA UTEUZI WA WAGOMBEA UBUNGE NA UWAKILISHI WA VITI MAALUM WANAWAKE

(i) Tarehe za Kuchukua na kurudisha Fomu

NAFASI YA UONGOZI
KUCHUKUA FOMU
KURUDISHA FOMU
Ubunge Viti Maalum Wanawake

19/07/2010
21/7/2010

Uwakilishi Viti Maalum Wanawake

19/07/2010
21/7/2010




(ii) Mchakato wa uteuzi wa Wagombea Ubunge/Uwakilishi wa Viti Maalum vya Wanawake


TAREHE
TUKIO

28/7/2010
Mikutano Mikuu ya UWT ya Mikoa kupiga kura za maoni kwa wagombea watano (5) kwa kila Mkoa na Makundi mengine, isipokuwa kundi la Vijana.

29/7/2010
Mikutano Mikuu ya UVCCM ya Mikoa kuwapigia kura za maoni wagombea wa Viti Maalum wa kundi la VIJANA.

30/7/2010
Kamati za Utekelezaji za UVCCM na UWT za Mikoa kutoa mapendekezo Kamati za Siasa za Mikoa.

2/8/2010
Kamati za Siasa za Mikoa kuandaa mapendekezo yatakayowasilishwa kwa Mabaraza ya UVCCM na UWT Taifa.











Ngazi ya Taifa

TAREHE
TUKIO
3/8/2010
Baraza Kuu la UVCCM Taifa, kufanya uchaguzi kwa wagombea wa kundi lao na kuwasilisha matokeo yake kwa Baraza Kuu la UWT Taifa.

4/8/2010
Baraza Kuu la UWT Taifa kuandaa mapendekezo yatakayowasilishwa kwa Halmashauri Kuu ya Taifa.

7/8/2010
Kamati za Siasa za Mkoa kujadili na kutoa mapendekezo kuhusu wagombea Ubunge/Uwakilishi na Udiwani katika Majimbo, Kata/Wadi.

9/8/2010
Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa Zanzibar kuwajadili.

10-11/8/2010
Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa kuwajadili.

12-13/8/2010
Kamati Kuu kupendekeza wagombea Ubunge/Uwakilishi.

14/8/2010
Halmashauri Kuu ya Taifa kufanya uteuzi wa mwisho wa wagombea Ubunge/Uwakilishi wa Majimbo na Viti Maalum

15/8/201
Siku ya kutangaza majina yote yaliyoteuliwa ya Udiwani wa Kata/Wadi, Uwakilishi na Ubunge.

Tarehe za kuchukua fomu za Serikali zitatangazwa na Tume za Uchaguzi.





(4) MCHAKATO WA UTEUZI WA WAGOMBEA UDIWANI WA KATA/WADI:


(i) Tarehe za Kuchukua na Kurudisha Fomu


NAFASI YA UONGOZI
KUCHUKUA FOMU
KURUDISHA FOMU

Udiwani wa Kata/Wadi
19/07/2010
21/7/2010



(ii) Mchakato wa Uteuzi wa wagombea Udiwani wa
Kata/Wadi


TAREHE
TUKIO
21/7/2010
Mara baada ya muda wa kurudisha fomu kumalizika saa 10 jioni, Kamati za Siasa za Wilaya zitafanya mikutano ya pamoja na wagombea wao waliorudisha fomu; kwa madhumuni yaliyokwisha kuelezwa.

22 - 31/7/2010
Mikutano ya kampeni ya wagombea Udiwani.

1 Agosti, 2010
Upigaji kura za maoni katika Matawi.

2-3 Agosti, 2010
Kukusanya matokeo ya matawi na kufanya maandalizi ya vikao vinavyohusika.

4 Agosti, 2010
Kamati za Siasa za Jimbo (Zanzibar) kujadili Wagombea Udiwani.

5 – 6 Agosti, 2010
Kamati za Siasa za Wilaya zitafanya mambo yafuatayo:

a) Kabla ya kuanza agenda ya kuwajadili wagombea, Kamati za Siasa za Wilaya zitafanya mikutano ya pamoja na wagombea wao waliopigiwa kura za maoni, kwa madhumuni ya kukubaliana juu ya suala la kuvunja makundi ya wagombea hao ili kuimarisha umoja na mshikamano ndani ya Chma chetu.
b) Kuwajadili na kutoa mapendekezo kuhusu
wagombea Udiwani wa Kata/Wadi.


c) Kuandaa orodha ya Majina ya wagombea wa
Viti Maalumu Wanawake kwa kuzingatia idadi
inayotakiwa kwa mujibu wa sheria.


7 Agosti, 2010
Kamati za Siasa za Mikoa kuwajadili na kutoa mapendekezo kuhusu wagombea udiwani wa Kata/Wadi katika Mikoa.

8 Agosti, 2010
Halmashauri Kuu za Mikoa kufanya uteuzi wa mwisho wa wagombea udiwani wa Kata/Wadi na kuwasilisha orodha ya walioteuliwa kwa Katibu Mkuu wa CCM.

15 Agosti, 2010
Siku ya kutangaza majina yote ya wagombea udiwani wa Kata/Wadi, Uwakilishi na Ubunge kwa tiketi ya CCM.

Tarehe za kuchukua fomu za Serikali zitatangazwa na Tume za Uchaguzi.






(5) UTEUZI KWA WAGOMBEA WA UDIWANI VITI MAALUM WANAWAKE


(i) Tarehe za Kuchukua, Kurudisha Fomu ndani ya Chama.


NAFASI YA UONGOZI
KUCHUKUA FOMU
KURUDISHA FOMU
Udiwani Viti Maalum Wanawake (Kata)
19/07/2010
21/7/2010

Udiwani Viti Maalum Wanawake (Wadi)

19/07/2010
21/7/2010



(ii) Mchakato wa uteuzi wa Wagombea ndani ya Chama

TAREHE
TUKIO
22/7/2010
Mikutano Mikuu ya UWT ya Wilaya kuwapigia kura za maoni wagombea wa nafasi za Udiwani Viti Maalum Wanawake.

23/7/2010
Kamati za Utekelezaji za Mabaraza Kuu ya Wilaya kuwajadili.

25/7/2010
Kamati za Siasa za Wilaya kutoa mapendekezo kwa wagombea wa nafasi za Udiwani Viti Maalum Wanawake.

30/7/2010
Kamati za Siasa za Mkoa kuwajadili na kutoa mapendekezo yao.

8/8/2010
Halmashauri Kuu za Mikoa kufanya uteuzi wa mwisho wa wagombea Udiwani wa viti maalum vya Wanawake, na kuwasilisha orodha ya walioteuliwa kwa Katibu Mkuu wa CCM.

Tarehe za kuchukua fomu za Serikali zitatangazwa na Tume za Uchaguzi.





“RUSHWA NI ADUI WA HAKI, SITAPOKEA WALA KUTOA RUSHWA”
[FONT=Tahoma, sans-serif]
[/FONT][FONT=Tahoma, sans-serif]
[/FONT]Ahadi za Mwanachama wa CCM
(Katiba ya CCM – 1977)





Imetayarishwa...
14:47:33 24.05.2010
 
Dah ccm ni noma kama walikua wanataka watu wapya wagombee wangeruhusu hao wagombea wafanye kampeni kama ilivyokuwa kwa Hilary clinton na Obama kule USA sasa hao wanafanya sirisiri hapo si ndio rushwa zitatembea hawa jamaa ni wasanii hakuna lolote bora hizo hela wangefanyia kazi nyingine hata kutoa msaada kwa watu wasiojiweza.Hapo ndipo utakapoona ccm hakuna kitu.
 
Dah ccm ni noma kama walikua wanataka watu wapya wagombee wangeruhusu hao wagombea wafanye kampeni kama ilivyokuwa kwa Hilary clinton na Obama kule USA sasa hao wanafanya sirisiri hapo si ndio rushwa zitatembea hawa jamaa ni wasanii hakuna lolote bora hizo hela wangefanyia kazi nyingine hata kutoa msaada kwa watu wasiojiweza.Hapo ndipo utakapoona ccm hakuna kitu.

Ngoja Makamba aje na majibu yake!
 
Back
Top Bottom