Frank Wanjiru
JF-Expert Member
- Apr 12, 2012
- 21,838
- 38,730
Pichani ni Amina Narcis Ndunguru (39) - Mkazi wa Makoka, Dar es Salaam amenusurika kifo baada ya kujeruhiwa vibaya kichwani hususani sehemu ya jicho la kushoto, kutokana kipigo kinachodaiwa kufanywa na Mume wake, Charles Jacob Kulemba.
Amina maarufu kwa jina la Mama Vai, Mama wa watoto wanne amelazwa katika Hospitali ya Bochi iliyopo Mbezi kwa Msuguri, Ubungo jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Amina alikutana na kipigo hicho mara baada ya kuonesha furaha ya ushindi wa mabao 5-1 ambao Yanga iliupata kwa kumwadhibu mtani wake wa jadi - Simba katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliofanyika Jumapili Novemba 5, 2023 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Amina ni shabiki wa Yanga na Mume wake ni shabiki wa Simba. "Ndugu mwandishi, kilichoniponza mimi ni Yanga, tuliwapiga Makolo 5-1," anasema Amina kwa shida akiwa Wodi ya Wanawake - ghorofa ya pili, Jengo namba mbili hospitalini hapo.