Ilikuwa hivi:
Jirani na ninapoishi kuna eneo limetengwa na Manispaa kwa ajili ya kuhifadhi takataka kwa muda kabla gari la Manispaa halijaja kubeba taka hizo.
Wakazi wengi wa mtaa wetu huona uvivu kwenda kumwaga taka ktk chemba hiyo iliyotengwa, badala yake husubiri usiku mwingi kuja kumwaga taka zao jirani kabisa na nyumba yangu.
Asubuhi ilipofika, nikaamka na kukuta furushi la taka jirani na kwangu.
Nikaghadhibika sana
Nikaamua kulibeba furushi hilo na kulipeleka dampo (chemba). Wakati nalikokota, furushi lile likanaswa na kipande cha mti, likapasuka na uchafu ukasambaa.
Hamadi!!!!
Nilichokiona, sikuamini. Nilipigwa butwaa. Baada ya akili kuwa Sawa, nikainama na kuokota na kukimbilia nyumbani, tena chumbani kwangu.
Nimezihesabu. Zipo Tsh 6,000,000 (milioni 6).