VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
UKAWA wanaongoza sehemu mbalimbali za kiutawala hapa Tanzania yakiwemo majiji kama ya Dar es Salaam na Arusha. Watanzania, kupitia uchaguzi mkuu wa 2015, waliwaamini Wabunge na Madiwani wa UKAWA na kuwachagua. UKAWA ni CHADEMA, CUF, NCCR na NLD.
Baada ya ushindi, kikaandaliwa na kuwekwa kibano. Vyanzo vya mapato vilivyokuwa vya Halmashauri vimepokwa na Serikali Kuu. Ndiyo kusema, kodi nyingi sasa zinakusanywa na Serikali Kuu na hivyo kuzibana mbavu Halmashauri kama za Majiji kupanga na kutekeleza mikakati yao. Bajeti zao ni finyu.
Kama hiyo haitoshi wala kutisha, wakuu wa Serikali wa sehemu hizo wamekuwa wakiingilia utendaji wa Halmashauri husika. Imeshakuwa sasa fasheni kwa Mkuu wa Mkoa au Wilaya kufuta au kuzuia hata posho za Madiwani. Ni kinyume na taratibu za Halmashauri ambapo Mkurugenzi huwajibika kwa Madiwani (Wakiwemo Wabunge wa Halmashauri husika).
Wakuu wa kiserikali sasa wanapuuza waziwazi Halmashauri ambapo wapo na kupoka kazi na majukumu ya Mkurugenzi wa Halmashauri. Hata Madiwani, ambao ni kama Bunge kwenye Halmashauri yao, wanaonwa si lolote. Hapo wapo pia Mameya na Manaibu Meya. Kila jambo linaamuliwa na viongozi wa kiserikali sasa.
Katika hali hiyo, amini nawaambia, UKAWA hawatobozi. Hawatafanikiwa katika walivyoviahidi. Wanabanwa kwelikweli na barabara. Lakini, UKAWA wana ngozi ngumu. Wanaendelea kupambana hivyohivyo pamoja na kubezwa, kumezwa na kutwezwa. Wanakukuruka kutimiza walichoahidi mwaka 2015.
Ni mwendo wa kudhibiti ili kuwafilisi UKAWA na wasiwe na cha kusema mwaka 2020!
Bastola ya nini tena jamani!?
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam