Ndugu wanajamii mimi ni mwanaume wa miaka 27 na nimekuwa na mahusiano ya kwanza na mwanamke kuanzia 2011.Tangu nibalehe sikuwahi kufanya ngono kutokana na msimamo wangu wa kidini,tarehe 30 may 2012 nilivunja msimamo wangu baada ya kujiridhisha na mwanamke ambaye nilijua nitamwoa na nilifanya baada ya yeye kuwa na wasiwasi kuwa huenda nina mapungufu na alikuwa tayari kuachana nami kama ningemkatalia.Haikuwa shida nilifanya kumthibitishia uwezo wangu na baada ya hapo nilitaka tufunge ndoa maana sikutaka kuzini tena ila alikataa akiomba amalize masomo ya chuo kikuu kwanza pale UDSM.Tuliendelea na ule mchezo na mwaka huu alishika mimba na nikamhakikishia kuitunza hivyo asitoe baada ya miezi miwili aliniambia kuwa alikosea tu kujua mzunguko wa siku zake na hakuwa na mimba,ilinishangaza sana baada ya muda aliniambia kaka yake amegundua kuwa alikuwa na mimba baada ya kuona meseji kwenye simu yake ya dakitari aliyetoa akidai ampelekee pesa yake hivyo aliniomba niseme sijawahi kufanya nae ngono ikiwa babaye au kaka yake angeniuliza.Baba yake hakuniuliza na sasa anadai alikuwa sahihi maana aliogopa baba yake angeacha kumlipia ada maana hana mkopo,kiukweli nampenda sana na ndoa tulitaka kufunga December mwaka huu ila kwa hili nashindwa kuendelea na hata yeye hajutii na hajaniomba msamaha natamani kumwacha lakini moyoni nampenda sana naombeni ushauri wenu maana tayari hata pete ya uchumba nimemvisha home wanamjua na kwao wananijua Kiukweli nimeumia sana na nina msongo wa mawazo sana (Samahani kwa maneno mengi niliyotumia)