America na Ulaya watu weusi bado wapo, Je uarabuni walitoweka vipi baada ya kukoma kwa Slave Trade?

themagnificient

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
988
3,318
Katika historia yetu wazungu pamoja na waarabu katika vipindi tofauti walipokuja Africa waliwachukua watu kutoka Africa na kuwapeleka katika nchi zao kwa ajili ya kufanyishwa kazi na mambo mengine

Lakini baada ya biashara ya utumwa kukoma wazungu hawakuwafukuza waafrica bali waliwatengea maeneo yao maalum na maisha yakaendelea pamoja na ubaguzi na mateso yalikuwa ya hali ya juu lakini hadi leo Amrica na Bara la ulaya kuna watu weusi wengi sana hadi leo hii.

Lakini tukija kwa ndugu zetu waarabu pamoja na wao kuwa na historia ya kuwachukua waafrica wengi zaidi kipindi cha biashara ya utumwa na kuwapeleka kwao uarabuni lakini leo hii 2018, ukizunguka nchi za kiarabu huwezi kukuta wazawa wa kiafrica yaani waarabu weusi ambao bado wanaishi kule na ukiwakuta jua wametoka nchi nyingine either wapo kikazi au wana mambo yao mengine

Maswali yanayokuja je

1)Watu hawa walienda wapi?

2)Waliuawa au walitoweka?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maybe waliwauzia wazungu

sent using samsung galaxy s8
 
Back
Top Bottom