Wakuuu hbr za usiku huu polen na uchovu wa majukumu ya kila siku ya kujitafutia riziki.Moja kwa moja pasipo kupoteza muda nijikite katika mada husika.
Ni kwamba nina mdogo wangu jinsia KE mtoto wa ndugu yangu.Huyu binti baada ya kuhitimu masomo yake ya O level mwaka 2016 na kufanikiwa kupata division two ya 20 alijiunga na masomo ya A level mwaka 2017 combination CBG.
Baada ya kusoma kwa takriban miaka 2 hatimaye mwaka huu amefanikiwa kuhitimu salama masomo yake ya elimu ya juu na sasa yupo nyumbani akisubiri matokeo kwa ajili ya kujiunga na chuo.
Kilichonifanya niandike Uzi huu ni kwamba huyu binti ameniomba msaada wa kimawazo baada ya kuingia mgogoro kati yake na wazazi wake juu ya kozi gani asome endapo atajiunga na elimu ya chuo.Kwa upande wa binti yeye anapenda sanaaaa kusoma kozi ya biashara na ndio lengo lake hilo.Kwa upande wa wazazi wake wanataka binti aende akasomee nursing kwani wao wanaamini nursing itamsaidia kupata ajira.
Kutokana na kuwepo kwa mitazamo hiyo miwili kinzani ndipo binti akaamua kuniomba ushauri juu ya kitu gani akasomee chuoni.Naomba msaada wa mawazo ni kitu gani nimshauri huyu mdogo wangu.
Ni hayo tuu ndugu zangu.