Ameniganda eti lazima nimuoe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ameniganda eti lazima nimuoe

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by HAZOLE, Oct 27, 2011.

 1. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,332
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Habari ndugu zangu wana jf,
  nina rafiki yangu wa kike tumekuwa wapenzi miezi 8 sasa, kiumri tupo sawa.ana watoto wawili mapacha alizaa akiwa na miaka 19. Mimi sijawahi panga kumuoa huyu binti, sasa kuanzia mwezi uliopita nikaamua rasmi kutengana naye. Nilikaa nae kuzungumza kwamba uhusiano wetu si wa milele(pia sijawahi kumwambia kwamba nitamuoa) so, kuachana kupo njenje.daaaahhhh kama nilichokoza nyuki vile, kaamua kuniganda, anataka awe anakuja home kwangu kila siku na simu haziishi.nimeongeza msimamo wangu kwamba sasa ndo basi maana imekuwa fujo sasa.
  Jana kanipigia simu ananiambia "piga ua lazima unioe"
  duh nikasema hapa kazi ninayo, jamani ushauri wenu maana ngoja werevu mseme huyu anang'ang'ania nini?
  By any means siwezi muoa hata aje na jeshi la nato.
  Thanks
   
 2. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Mkuu mbona unauliza majibu,jibu liko mbele yako unaliona kabisa bana kisha unauliza?
   
 3. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kijana ndoa hailazimishwi, kama ulikuwa unapunguza uchovu kwake mwambie wazi.
   
 4. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #4
  Oct 27, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Hiyo bunduki haijakusaidia?...
   
 5. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,332
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  bunduki ipi mkuu??
   
 6. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,332
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  good idea. Very simple, haolewi mtu kifalfala
   
 7. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,332
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  teh teh teh bishanga acha visa, nipe mbinu mjukuu wako. Vipi mwanao yule last born ameacha utukutu wa kutofanya assignment?
   
 8. v

  valid statement JF-Expert Member

  #8
  Oct 27, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,737
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  mwambie moja kwa moja mi sikuoi bana. Nna mtu tayari.
   
 9. L

  Luluka JF-Expert Member

  #9
  Oct 27, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Afu na wewe ulichotaka kwake ni nini?uache um-l-y- kuchezea watoto wa watu!huyo dada aendelee kukung'ang'ania tu!stupid!
   
 10. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #10
  Oct 27, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Alafu Hazole unaanza kunipa wasi na topic zako... Kwanza ilikua ni barmaind ambae anakung'ang'ania umuoe... Pili ilikua kutupa taarifa kua umepata mchumba (ambae nakumbuka hukunijibu kama ni yule barmaid ama lah!) Kupitia topic yako ya "ulazima wa kuoa" Hii topic has you on the hooks eeeh??

  Habari yako Hazole (Sema mkuu kama kweli serious, ili kweli tutoe ushauri...)
   
 11. h

  hayaka JF-Expert Member

  #11
  Oct 27, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mpige chini fasta, kwani ulimbaka si alikubali kwa hiari, sasa anakuganda nini, mvalie sura ya kazi.
   
 12. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #12
  Oct 27, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Unajua mambo ya kulazimisha ndoa madhara yake makubwa sana.
  Mwisho wa siku atasema anaenda kumsalimia mzazi mwenzie sijui utakataa?
   
 13. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #13
  Oct 27, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,006
  Likes Received: 2,660
  Trophy Points: 280
  Mtoto wapi wakati ni mmama mtu mzima mwenye watoto.
   
 14. ghumpi

  ghumpi Senior Member

  #14
  Oct 27, 2011
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 187
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Kijana umelikoroga. Sasa linywe basi
   
 15. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #15
  Oct 27, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mweleze ukweli kua safari yenu imeishia hapo.
   
 16. kashengo

  kashengo JF-Expert Member

  #16
  Oct 27, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 2,649
  Likes Received: 466
  Trophy Points: 180
  We kijana ni FATAKI utawa*** wangap? Unajua ipo siku nawe yatakukuta umzalishe alafu umkimbie? Alafu eti ushauriwe? Koma akun'gan'ganie tu..safi sana mnapenda kudo lakini outcomez hamzitaki kwanin?
   
 17. Bhbm

  Bhbm JF-Expert Member

  #17
  Oct 27, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 716
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kama yeye kweli ni bingwa wa kung'ang'ania watu, kwa nini asimng'ang'anie jamaa alomzalisha mapacha?
   
 18. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #18
  Oct 27, 2011
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Na wanawake wa kisasa eti ukipenda boga penda na ua lake. Hapo kijana akioa tu matunzo kwako hao watoto
   
 19. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #19
  Oct 27, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,332
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  ashadii haya bwana......
  this is true mkuu, ni jana tu nimetoka kumpigia simu na kumwambia hakunaga ndoa hapa. kuhusu barmaid ni kweli huwa naenda bar moja kuna kula chakula kizuri na drinks na zaidi week end na huwa natazama soka, sasa huyo maid yupo pale na alikuwa ananikubali sana,nilishasovu na kanizoea kawaida kwa sasa.
  naomba ushauri ndugu yangu maana akiendelea kujakuja home wengine hatunaga aibu, ntamfukuza hovyo aalllaaaah.
   
 20. m

  mzabzab JF-Expert Member

  #20
  Oct 27, 2011
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 6,981
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  hahahahahah
  unajua hapa mie kwanza nakulaumu wewe...wewe unaingia kwa mwanamke ambaye tayari kashazaa unadhani ayakuachia kirahisi tuu....huyo market yake kwisha haribika sasa wewe ulivyojiingiza tuu akaona mdio hapa hapa lol

  sasa kusema kweli hawezi kukulazamisha unuoe ila sassa huwezi jua reaction yake itakuwaje....maana watu tunatofautiana .....brace urself for a long baattle!!!
  sasa mara nyingi binadamu anaonaga mlanngo wakuingilia ila wakutokea haoni na anadhani itajipa tuu.....so lesson hapa.ni kama unataka kumkojolea demu be careful katika selection yako maana kweli hawezi kukulazimisha umuoe ila chamoto utakiona!!!!!!
   
Loading...