Habari za kazi wakuu,
kwanza napenda kutoa uzi huu nikiwa na majonzi makubwa kweli, kwani mahusiano yangu yamevunjika kizembe sana japo kuna wakati najipa moyo kuwa ni ujasiri... Mpenzi wangu aliaamua kuondoka kwao baada ya kukuta Kondomu iliyotumika chumbani kwangu. Huwa anasafiri mara kwa mara ndipo nipo shetani aliponivuta mkono nikaomba game kwa dada mmoja ambaye ni mpangaji mwenzetu na hii ndio chanzo baada ya kuisahau kuitupa, Lakini bado najiuliza kwanini asingenisamehe na kunipongeza kwamba nimetumia kinga? itakuwaje akipata mchepukaji ambae hatumii kinga?
Wito wangu ni kwamba bado nampenda na ndio maana nilikumbuka kinga hivyo kama ananisikia arudi nyumbani nipo tayari kuhama ile nyumba.