Amemuachisha kazi mumewe kawa baba wa nyumbani

cosa nostra

JF-Expert Member
Sep 17, 2010
1,773
1,804
Hii inakera sana.

Kuna dada mmoja rafiki yangu ameolewa miaka mitatu iliyopita ni msomi na anafanya kazi kama Muhasibu katika kampuni kubwa hapa nchini, wote wanaumri si zaidi ya miaka 30.

Mara kwa mara huwa anahamishwa kikazi kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine. Anachokifanya huwa anasafiri na mumuwe kwa kuwa yeye anakipato kikubwa basi ameshamuachisha kazi mumewe na mumewe amekubali kua baba wa nyumbani.

Yani kazi za huyo mumewe ni kama za mama wa nyumbani, mkewe akiwa kazini anamuuliza vipi salama hapo nyumbani, mtoto anaendeleaje, anamtuma sokoni na kufanya shughuli zote kama mwanamke.

Kinachoniudhi kwake jamaa hajiongezi kabisa kufanya mishe mishe kama wanaume wengine katika hiyo miji anayohamia yeye ni kudrive gari ya wife na kusubiri kuhudumiwa kama mwanamke.

Natamani nimshauri lakini naogopa nitakua naingilia maisha yao
ila hili jamaa limekua kama fala yani halina aibu kabisa.
 
Fanya yako ... ishi maisha yako yangoswe mwachie ngoswe
nimeyaacha ndio maana nimefunguka huku ili tabia hii isiwepo coz ni mfano mbaya hata kwa mtoto wake,akikua atakua anajua baba kukaa home poa tu
 
Yeye kakwambia hapendi hiyo hali? Kwann umlazimishe apende unachopenda wewe na si alichoridhika mwenyewe?

We achana na ya wengine bana
 
Achana na nyumba za watu...wanawake wengi wanapenda wawe na pesa ili watu-control wanaume tatizo ni kuwa hiyo kitu ni ngumu sana
 
Ni aibu sana mtoto wa kiume kuwa mmbea kiasi hki nakushauri tu fanya yako achana na lifestyle za watu
 
Unataka kutia sumu kwenye love la watu. Kama jamaa mwenyewe kakubali na karidhika mwache waendelee. Sasa ukisema unaudhika wewe nashindwa kukuelewa.
 
Jamani mapenzi ni makubaliano kati ya wawili kama mume ameridhika kuacha kazi na kulea familia tatizo letu sisi wengine liko wapi wakti muhusika ameridhika?
 
Acha mfumo dume wewe , mama anamlea dume lake wewe unataka kutia kokoro, Fanya yako na wao waache waendelee na yao, kwanza akipika msosi na kukuna Nazi wewe kinakuuma nini

Acha umbea
 
Back
Top Bottom