Uandikishaji wa BVR umekuwa ukiendelea katika hali ya kulegalega na kuna uwezekano kuna watu wengi hawataandikishwa.Je ambao watakosa haki ya kuandikishwa kutokana na makosa ya tume ya uchaguzi wanaweza kudai haki yao mahakamani?
Binafsi Naona kusubiri mpaka zoezi likamilike tutakuwa tumechelewa na baadhi ya raia wema kukosa haki yao ya msingi. Nilitarajia mpaka sasa wanaharakati, viongozi wa dini na wanasiasa wawe tayari na majina ya walioshindwa kujiandikisha kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo uzembe wa time, nilitarajia kuwa nimesikia tamko la tume juu ya watu hao. Haiingii akilini kujaza waangalizi wasaidizi wakati wa kupiga kura na kushindwa kuwa na waangalizi wakati wa uandikishaji ili kubaini kasoro na kuishauri tume!