Ambao hatujasajili ‘laini’ kwa alama za vidole tukutane hapa, tatizo ni lipi au tunachukuliaje hili zoezi?

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
15,024
28,200
Heshima zenu wakuu,

Ni kama juzi tu ila siku zimeyoyoma, ilikuwa mwezi Juni kama sijasahau ikawa agizo la kukamilisha usajili ni hadi Disemba 31 mwaka huu watu wewee utasema tumeshinda bingo.

Siku hazigandi na sasa spidi imeongezeka, na kadri siku zinavyosonga naona ‘vitisho’ vinazidi. Hivi ni kweli hawa jamaa wako ‘siriazi’ au tusubiri kuona watatufanya nini?

Onyo: Laini yako itafungwa baada ya 31/12/2019 ikiwa haikusajiliwa kwa alama za vidole. Tembelea duka la Tigo au wakala ukiwa na namba ya nida au kitambulisho.

Na wengine mnaopata ujumbe kama huu, sababu ipi imekukwamisha au jeuri?
 
jana nmeingia website ya nida nkakuta wamejiongeza kwani unaweza jaza details zako wakakuletea namba yako, sasa tangu jana mpk leo sijaona wale wanaosajili mitaani wakipita tena wakati kabla sijapata namba kila siku walikua wanapita, mi nasubiri wapite ndo nisajili sitaki kupoteza nauli kwenda kwe maduka yao
 
imekua deal kwa wenye mamlaka ya kutoa affidavit . yaani ni gharama sana ukizingatia watu wengi wazima hawana supporting document kama cheti cha kuzaliwa
 
jana nmeingia website ya nida nkakuta wamejiongeza kwani unaweza jaza details zako wakakuletea namba yako, sasa tangu jana mpk leo sijaona wale wanaosajili mitaani wakipita tena wakati kabla sijapata namba kila siku walikua wanapita, mi nasubiri wapite ndo nisajili sitaki kupoteza nauli kwenda kwe maduka yao
Naomba link ya Website yao nijaribu
 
Back
Top Bottom