Angalizo kwa ambao bado hatujasajili line kwa alama za vidole

Kona4

Senior Member
Nov 1, 2019
145
242
Habari wapendwa?
Poleni na abc za hapa na pale!

Bado siku chache sana kuelekea kufungiwa huduma kwa ambao hatujasajili line za simu kwa alama za vidole.

Mimi ni muhanga wa hili zoezi, nimefuatilia sana huko NIDA lakini wamenipanga tena kurudi January 15 mwakani ..

Sasa nawaza endapo nitafungiwa, hii miamala niliyonayo humu kwenye line nitaitoaje?

Je nikiambiwa tena kurudi February 30? Maana NIDA hawaeleweki!!

Wadau nashauri tuanze kuangalia njia mbadala za kutunza pesa zetu na sio M-pesa, tigo wala Airtel Money mpaka pale tutakaposajili line zetu upya.

Nimetoa angalizo tu sina maana ya kuharibia watu biashara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wadau nashauri tuanze kuangalia njia mbadala za kutunza pesa zetu na sio M-pesa, tigo wala Airtel Money mpaka pale tutakaposajili line zetu upya.
Swali jingine linajitokeza kuhusu haya maswala ya fedha.

Je itakuwaje kwa mkopaji/wakopaji wa MPAWA iwapo laini zao zitafungiwa? wakiwa na madeni, kwa kutosajiriwa kwa wakati!
 
Back
Top Bottom