Ambani,mwalala wafulia china | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ambani,mwalala wafulia china

Discussion in 'Sports' started by Pdidy, Jul 28, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,107
  Likes Received: 5,563
  Trophy Points: 280
  Boniface Ambani asikitika kuikosa Ligi Kuu[​IMG]Na Jessca Nangawe

  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Kenya, Boniface Ambani huenda akakosa baadhi ya mechi za ufunguzi za Ligi kuu baada ya kupewa mapumziko ya mwezi mmoja kutokana na kusumbuliwa na nyonga kwa muda mrefu.

  Ambani aliyewasili juzi akitokea China alikokwenda kwenye majaribio katika klabu ya Xian, ametakiwa kupumzika zaidi ya mwezi mmoja kwa ajili ya matibabu.

  Akizungumza na Mwananchi jana, Ambani alisema kilichomfanya ashindwe majaribio yake nchini China ni kusumbuliwa na nyonga na ameambiwa na daktari wake apumzike kwa muda wa mwezi mmoja kwa ajili ya matibabu.

  Alisema bado anapata maumivu makali na hataweza kujinga na wenzake ambao tayari wameanza mazoezi kwa ajili ya maandsalizi ya msimu ujao wa ligi na kulazimika kupata matibabu kama livyoshauriwa na daktari wake.

  ''Nimerejea jana (juzi) kuitoka China lakini nasikitika sitaweza kujiunga na wenzangu mpaka nitakapomaliza matibabu kwani mpaka sasa bado nina mamumivu sehemu za nyonga na ndio chanzo kikubwa kilichopelekea mimi kushindwa katika majaribio yangu,'' alisema Ambani.

  Ambani alisema ingawa kuna uwezekano mkubwa wa yeye kukosa baadhi ya mechi za mwanzoni lakini ana imani nafasi yake itazibwa na wachezaji wengine ambao wamesajiliwa katika klabu ya Yanga na atakapopata nafuu atarudi katika nafasi yake. Kikosi cha Yanga tayari kimeanza mazoezi ya ufukweni ingawa baadhi ya wachezaji wao wa kimataifa ambao hawajawasili kuwasili wakati wowote na kitapiga kambi katika klabu yao iliyopo mtaa wa Jangwani ambayo tayari imekamilika.
   
Loading...