Hii ndiyo kali yao nimeitoa "readers digest"
Wakati mwingine mapacha wana hadithi za kushangaza ila hawa ni kali yao. Wavulana wadogo walijitenga baada kuchukuliwa na wazazi wengine. Wazazi wapya wa wavulana hawajawahi kufahamiana na hawajawahi kukutana. Ila kila mmoja aliambiwa alikuwa na ndugu.
Miaka arobaini baadaye mmoja, James aliamua kufuatilia ndugu yake ajue alipo. Baada ya kumtafuta muda mrefu, akamkuta ndugu yake, na alikutana na haya:-
--- pacha mwenzie naye aliitwa James! Ingawa hawajawahi kukutana.
--- wote wawili walikwenda kusoma "law enforcement"
---Wote wawili walikuwa na ujuzi bora ufundi seremala na kuchora.
---Wote wawili walioa wanawake walioitwa Linda.
---Wote wawili walikuwa na watoto, mmoja alitwa James Allan wa mwingine aliitwa James Alan.
---Baadae kila mmoja alitengana na mkewe na kuoa tena wanawake walioitwa Betty!
--pia wote wawili walimiliki mbwa na kila mmoja alimpa jina la Toy!