AMATB - Niulize Chochote Kuhusu Tehama na Biashara

Mtangoo

JF-Expert Member
Oct 25, 2012
6,167
5,602
Habari na Heri ya Mwaka Mpya 2021!

Nimeamua kila nipatapo wasaa kujaribu kusaidia kuelimisha na kushirikisha mawazo wadau mbalimbali juu ya Teknolojia na Biashara, hasa Teknolojia ya Habari na Mawasialiano. Mara ya kwanza na ilikuwa ya mwisho kwa mwaka 2020 ilikuwa ni mwezi Septembe. Tafadhali pitia huko uone kama swali lako halijajibiwa kule kabla ya kuuliza tean!

Mambo muhimu ya kuzingatia kwenye mfululizo huu wa Ask Me Anything Technology and Business (AMATB). ni kama ifuatavyo:
1. Maswali yasiyo na lengo la kujifunza sitayajibu. Sababu ni kuwa lengo ni kushirikishana ufahamu niliopata neema ya Mungu kuwa nao na si vinginevyo.

2. Maswali yasiyohusiana na biashara na teknolojia sitayajibu. Hii ni kutunza focus kwenye mada husika.

3. Maswali yenye mrengo wa kisiasa sitayajibu. Kwa sababu ni nje ya lengo.

4. Maswali kuhusu maisha binafsi sitayajibu. Kwa sababu hii sio Biography. Unless yawe yanahusiana na mada na yatakuwa msaada kwa wasomaji, then nitaangalia namna bora ya kujibu.

5. Sipo hapa 24/7 na wala sina msaidizi wa kusoma hapa. So ukiweka swali lako uwe na uvumilivu.

Best rule: Kama usingependa uulizwe swali hilo ni vyema usiulize...!

Sept 2020 AMATB: September AMATB - Niulize Chochote Kuhusu Tehama na Biashara

Karibu!
 
Ahsante kwa thread hii mkuu,

Picha hii hapa;

TRA wameweka mfumo wa kusajili TIN number online lakini bado mtu anahitaji kwenda office ya TRA kufanyiwa makadilio, sasa basi hii inakuwa ni kama usumbufu flani japo kuwa nafahamu mtu anaweza danganya hasa upande wa mtaji hivyo kupata makadilio yasiyotakiwa lakini labda zipo sababu zingine pia.

Swali hili hapa!

Kwanini tehama na biashara bado havikubaliani katika mazingira kama hayo kwenye maelezo yangu hapo juu?
 
Ahsante kwa thread hii mkuu,
Karibu sana boss!
Picha hii hapa;

TRA wameweka mfumo wa kusajili TIN number online lakini bado mtu anahitaji kwenda office ya TRA kufanyiwa makadilio, sasa basi hii inakuwa ni kama usumbufu flani japo kuwa nafahamu mtu anaweza danganya hasa upande wa mtaji hivyo kupata makadilio yasiyotakiwa lakini labda zipo sababu zingine pia.

Swali hili hapa!

Kwanini tehama na biashara bado havikubaliani katika mazingira kama hayo kwenye maelezo yangu hapo juu?
Kwa maoni yangu sio kwamba Tehama na Biashara havikubaliani. Tehama ni rafiki na mtumishi mzuri sana wa biashara. Tatizo kubwa la Nchi yetu ni sera zetu ambazo zinaifanya Tehama isiwe rafiki au mtumishi mzuri. Nitatumia mfano wako kuelezea hili.

Ili kumkadiria mtu ni lazima ujue kipato chake na faida anayopata. Kwa sasa ni vigumu kwa sababu wengi wa wafanyabiashara, wakubwa kwa wadogo, hawatunzi hesabu kwa namna inavyotakikana na wataalam wa mahesabu. Kwa hiyo kwa utaratibu huu lazima mtu afike afanye mahojiano na Afisa ili kupata uhalisia na kujua anaangukia kundi gani katika kodi. Hili ni tatizo la kubwa!

Lakini Tehama ina suluhu ya suala hili. Kwa sasa kuna mifumo mingi ya mahesabu ambayo wafanyabiashara wanaweza kuitumia, ya bure na ya kununua. Kama mifumo hii ingekuwa imeunganishwa na TRA ina maana kusingekuwa na haja ya TRA kukadiria kwa kuwa wangepata mauzo yote moja kwa moja na kujua stahili yao kwa mwaka huo bila kukadiria.

Kimsingi kiufundi hili linawezekana. TRA wana mfumo tayari ambapo mashine za EFD zinatuma data. Ina maana wanaweza ku extend na kutumia mfumo huo huo kwa special API, kuruhusu mifumo mingine kutuma data za wateja wao kwenda TRA na kuepuka usumbufu. Lakini TRA inaongozwa na sheria na sera. Je sheria na miongozo inawaruhusu TRA kufanya hivyo? Sijui, ila nina mashaka kama zinaruhusu.

Kwa maoni yangu kuna mambo kadhaa yanatakiwa kufanyika ili tufike mahali pa TRA na Wateja wao ambao wanapenda kwenda kidijitali waende sawa bila kokoro:
1. Sheria na Kanuni, kama haziruhusu bado TRA kuwa na mifumo ya wazi (Open API) kwa general Public, basi wapeleke marekebisho Bungeni ili wapewe mamlaka hayo (kupitia wizara husika)

2. TRA watengeneze mifumo ya wazi (Open API) ambapo itakuwa na open sandbox ambapo developers watapatumia kutengeneza systems zao na kuzijaribu. Kisha kuwe na open registration, kwa maana kila mwenye TIN akiomba special key kwa ajili ya mfumo wake kutuma data TRA asiwe na safari ya kwenda ofisini. Aingie na kujisajili. Then TRA watajiridhisha na taarifa zake (ikiwemo kumpigia simu, kumtembelea, kuona demo au watakavyoona inafaa kufanya system Audit) then wana activate ile Key. toka hapo mteja yeyote wa System hiyo atatuma data kupitia API key ya huyo vendor na TIN number yake.

3. Cancellation au editing ya Transaction yoyote ifanyike Online na TRA wafanye approval tu na kui notify system husika on approval au rejection. Kama ikiwa rejected then utaratibu wa barua utafuata.

Tukienda na direction hii, soon or later Compliance karibu zote za TRA zitakuwa Online, tutaondoa Makadirio ambayo muda mwingi hayana uhalisia kwa sababu kundi kubwa linakuwa chini ya makadirio sawa, na serikali itapata haki yake bila wizi wala utapeli.

Tatizo moja ambalo nimeliona linaathiri mifumo mingi pale serikali inapoamua kuwa na vendors kama nilivyoeleza juu ni kuruhusu Monopoly. Unakuta serikali inaamua kuchagua Vendors labda wanne au kumi. Hii ina shida kadhaa. Kwanza inaua ushindani katika huduma. Kwa maana hakutakuwa na innovation ili kuvutia wateja. Lakini Pili inaua ajira. Imagina soko kubwa kama la nchi yetu liwe na Vendors watatu. Vijana wanatoka chuo wana morali wa kufanya mapinduzi ila wanakosa nafasi ya kufanya kwa kuwa tayari kuna wachache tu ndio wanaruhusiwa. Kama wangeruhusiwa, wenye huduma mbovu soko lingewatema na wangekufa kimya kimya na wazuri wangeng'aa.

Kwa hiyo ningependa kuwashauri TRA kama wataamua kwenda na mawazo hayo wafanye juu chini kuhakikisha hawalei monopolism. Wahakikishe wanakuwa na open API na open list ya Matakwa ambayo mhusika akiweza kuyatimiza anapewa Key na kufanya miamala na TRA backend. Hii itawarahisishia sana kupata data hata za wafanyabiashara wa Mbwinde, maana wale ambao hawataweza kushindana mjini wataenda vijijini na kufanya biashara huko, ambako hardly TRA wangeweza kufika effectively. Pia digitization process itakuwa swift and simpler kuliko kulazimisha watu wachache wahodhi kila kitu.

Ningeweza kusema mengi zaidi ya hapo ila nadhani kifupi haya ndio maoni yangu!
 
Ni ipi nafasi ya teknolojia kubadilisha maisha ya vijana wa kitanzania?

Na upi ushauri wako wa kijana km Mimi mwenye miaka 34 anaetaka kuanza kujifunza teknolojia mbalimbali ili aweze kujipatia kipato? Je ni umri sahihi au nilishachelewa tayari?

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Mkuu, Nshukuru kwa Hii mada.
Naomba kujua jambo, Mimi ni freelance na nabahatika kufanya kazi na baadhi ya makampuni hapa tanzania. Mwanzoni kuhusu swala la malipo nilikuwa natumia TIN kwa ajili ya hayo makampuni kukata Withholding Tax, Ila kwa sasa ni ngumu kila ninaoafikiana nao kazi wanahitaji EFD receipt kwa ajili ya malipo na kwangu imeniwia ngumu kununua hiyo machine ikiwa bado hata sijafanikiwa kufungua office.
Wakati Huohuo makampuni hayohayo wakinunua Huduma kama za Matangazo ya Facebook au Google hakuna EFD receipt na biashara wanafanya.

Swali langu ni kwamba Nitawezaje kufanya kazi na haya makampuni nikiwa sina EFD na wao wanasema hawatoi hela bila EFD receipt kwani watu wa auditing wanawaletea shida.
 
Ni ipi nafasi ya teknolojia kubadilisha maisha ya vijana wa kitanzania?
Teknolojia kwa upana wake ina uwezo wa kubadilisha maisha ya vijana wengi wa kitanzania kama itatumika vyema. Kumbuka Teknolojia ni nyenzo tu. Bado akili na ubunifu wako unahitajika ili kubadilisha maisha. Ukiwa na wazo, ukaliweka kwenye vitendo na kwa kutumia teknolojia lazima ubadilishe maisha ya kwako binafsi na wengine. Kwa kuwa teknolojia ni pana, nitaishia hapa. Kama una swali maalum kwa kipande fulani cha teknolojia nitafurahi kuweka maoni yangu

Na upi ushauri wako wa kijana km Mimi mwenye miaka 34 anaetaka kuanza kujifunza teknolojia mbalimbali ili aweze kujipatia kipato? Je ni umri sahihi au nilishachelewa tayari?
Kwanza nikwambie hakuna mtu wa kukwambia umechelewa kwenye miaka 34. Kwa sababu bado u kijana na akili yako ina uwezo mkubwa wa kujifunza na kuelewa na una nguvu za kufanya kile unatamani kufanya. At least ungekuwa 60 au 70 hivi tungeongelea suala la kama umechelewa ama la. Kwa hiyo hujachelewa.

Ila kwenye uhalisia wengi katika umri huu wanakuwa wameanza kuwa na majukumu kama familia au kulea ndugu, na mengineyo, kwa hiyo muda wako, kama uko kundi hili, sio mwingi sana. Bado sio sababu ya kukuzuia. Cha msingi unapaswa kufanya utafiti kujua kile unachotaka kufanya kitahitaji ujue teknolojia ipi kwanza. Hii ni kwa sababu hautakuwa na muda wa kuchezea kujaribu kila kitu. Ukiisha kujua unataka nini na itahitaji teknolojia gani then unahitaji mambo mawili: 1. Ratiba maalum. Mathalani unaweza kuamua kuwa kila siku angalau unapata saa moja la kusoma na saa moja la kufanya mazoezi. Utayagawa kadri unavyoona maana ratiba hutofautiana 2. Unahitaji kuifuata hiyo ratiba bila kukosa. Kila siku. Ukifanya hivyo una uhakika kuwa mwaka unapokwisha wewe ni mtu mwingine kabisa, na hutaamini!

Ushauri wangu ni uanze hatua ya kwanza SASA na usisubiri. Maana utasema kesho na kesho huwa haifiki!
 
Mkuu, Nshukuru kwa Hii mada.
Naomba kujua jambo, Mimi ni freelance na nabahatika kufanya kazi na baadhi ya makampuni hapa tanzania. Mwanzoni kuhusu swala la malipo nilikuwa natumia TIN kwa ajili ya hayo makampuni kukata Withholding Tax, Ila kwa sasa ni ngumu kila ninaoafikiana nao kazi wanahitaji EFD receipt kwa ajili ya malipo na kwangu imeniwia ngumu kununua hiyo machine ikiwa bado hata sijafanikiwa kufungua office.
Wakati Huohuo makampuni hayohayo wakinunua Huduma kama za Matangazo ya Facebook au Google hakuna EFD receipt na biashara wanafanya.

Swali langu ni kwamba Nitawezaje kufanya kazi na haya makampuni nikiwa sina EFD na wao wanasema hawatoi hela bila EFD receipt kwani watu wa auditing wanawaletea shida.
Hili ni swali ambalo limekaa ki sera zaidi na sijajua sera za makampuni uliyofanya nayo kazi ila nitajaribu kuweka mambo mawili matatu yanayoweza kuwa msaada. Nakushauri ukae nao chini kujaribu kujua sababu za kudai EFD.

Ukitoa huduma kwa Biashara au mtu, kuna mawili. Moja inabidi anapokulipa umpe risiti ya EFD. Pili anaweza yeye kukukata kama huduma inaangukia kwenye zile ambazo zinaweza kufanyiwa witholding Tax. Kuna list na maelezo zaidi kwenye website ya TRA Hapa

Nikushauri tu tena, ni vyema ukaongea nao kujua kwa nini wanadai risiti badala ya kuzuia kiasi cha pesa na kukupa certificate yako ya kodi. Sera za kampuni mara nyingi huwa ndio sababu kwa hiyo bila kukaa nao chini huwezi kujua.

Mwisho nikushauri tu kama ni wateja wako wa muda mrefu, ni vyema ukanunua EFD Machine hata kwa kukopa kwani ukiwapoteza wateja, kuja kuwapata tena huwa ni kazi ngumu kuliko kurudisha mkopo wa kununulia mashine!
 
Teknolojia kwa upana wake ina uwezo wa kubadilisha maisha ya vijana wengi wa kitanzania kama itatumika vyema. Kumbuka Teknolojia ni nyenzo tu. Bado akili na ubunifu wako unahitajika ili kubadilisha maisha. Ukiwa na wazo, ukaliweka kwenye vitendo na kwa kutumia teknolojia lazima ubadilishe maisha ya kwako binafsi na wengine. Kwa kuwa teknolojia ni pana, nitaishia hapa. Kama una swali maalum kwa kipande fulani cha teknolojia nitafurahi kuweka maoni yangu

Kwanza nikwambie hakuna mtu wa kukwambia umechelewa kwenye miaka 34. Kwa sababu bado u kijana na akili yako ina uwezo mkubwa wa kujifunza na kuelewa na una nguvu za kufanya kile unatamani kufanya. At least ungekuwa 60 au 70 hivi tungeongelea suala la kama umechelewa ama la. Kwa hiyo hujachelewa.

Ila kwenye uhalisia wengi katika umri huu wanakuwa wameanza kuwa na majukumu kama familia au kulea ndugu, na mengineyo, kwa hiyo muda wako, kama uko kundi hili, sio mwingi sana. Bado sio sababu ya kukuzuia. Cha msingi unapaswa kufanya utafiti kujua kile unachotaka kufanya kitahitaji ujue teknolojia ipi kwanza. Hii ni kwa sababu hautakuwa na muda wa kuchezea kujaribu kila kitu. Ukiisha kujua unataka nini na itahitaji teknolojia gani then unahitaji mambo mawili: 1. Ratiba maalum. Mathalani unaweza kuamua kuwa kila siku angalau unapata saa moja la kusoma na saa moja la kufanya mazoezi. Utayagawa kadri unavyoona maana ratiba hutofautiana 2. Unahitaji kuifuata hiyo ratiba bila kukosa. Kila siku. Ukifanya hivyo una uhakika kuwa mwaka unapokwisha wewe ni mtu mwingine kabisa, na hutaamini!

Ushauri wangu ni uanze hatua ya kwanza SASA na usisubiri. Maana utasema kesho na kesho huwa haifiki!

Ahsante chief kwa majibu yako
 
Another question...… ni kitu gani kifanyike kusaidia sekta ya manunuzi online ikue! Kwa maoni yangu binafsi naona hii sekta ina potential kubwa Sana kubadilisha maisha yetu waafrica
 
Sekta hii ni potential, true! Ila ni ngumu kwa sababu ina pande nyingi sana. Kuna Kuweka mfumo ambao utasimamia kuanzia kununua mpaka kuupokea. Hii ni sehemu ya kwanza. Pili kuna kupata Merchants watakaouza kwenye Platform yako. Tatu kuna Logistics kwa maana ya kufikisha kwa mteja ambao mfumo utakuwa na wakati mgumu kwa sababu ya poor addressing ya nyumba na mitaa.

Ukiweza vyote hivyo uje kuwashawishi watu watumie mfumo wako badala ya kwenda dukani wenyewe.

Kiufupi ni potential sana ndio maana Amazon imemtoa Jeff Bezos. Lakini inahitaji msuli mnene sana kufanikiwa ama sivyo utachukua muda mrefu sana kujenga mfumo ambao unafanya kazi.
 
Programming language zipi zipo highly demanded hapa Tanzania hasa upande wa web
Web Bongo ni PHP kwa backend. Enterprises nyingi bado ni Java na .Net
na ule wA desktop pia

Sent from my TECNO BD2 using JamiiForums mobile app
Desktop Bongo wengi hutumia Microsoft Technologies. Kwa hiyo MS Languages kama C# ni muhimu. Ila kama unatengeneza software kwa ajili ya kuuzia makampuni, tumia language yoyote modern. My suggestion is always C++/wxWidgets au Python/wxPython
 
Ni Payment API gateway zipi kwa hapa bongo na providers wake ambazo unatumia kwenye projects zako na zipo documented vizuri!?
 
Situmii Payment gateways zozote. Inapohitajika ninafanya direct Integration iwe na MNOs au Banks.
 
Bro, Kuna project nafanya ya biometric student attendance system. Nataka iwe desktop application je kwa C# naweza nika implement hii project?
 
Nakushauri uanzie kwenye hardware kufanya decision ya hiyo project. Je wana SDK ya C#? Kama hawana kuna namna ya ku communicate kwa C#? Kama ipo nitafanya majaribio ya kusoma fingerprint just kuwa sure itafanya kazi.

Baada ya hapo swali litakalofuata ni accessibility ya data. Je nani wanazihitaji data. Zinahitajika kuonekana in the same place at same time? Kama Yes then unahitaji data ziee kwenye server na hiyo app yako iwe inapost huko.

Kama ni just ku digitize daftari la mahudhurio no need for a server
 
Lengo ni ku digitize tu daftari la mahudhurio na kufanya zoezi la attendance tracking liwe rahisi na wanafunzi wasiwe na uwezo wa ku manipulate kwa kumsainia mqwenzako ambaye hayupo (by the way ni student final project)
 
Kama ni final year, nakushauri kuwe na Backend ambapo utaweka some analytics kama report ya wanafunzi in general, trend za kuwahi, kuchelewa, na report za mwanafunzi mmoja mmoja. Unaweza pia kutengeneza recommendation report ambayo inatoa list ya wanafunzi ambao ni habitually late comers. Hii itawasaidiwa waalimu kujua waongee na wanafunzi gani kujua wana tatizo gani na kuwasaidia kuwahi.

itakupa more credit than daftari la kidijitali!
 
Habari na Heri ya Mwaka Mpya 2021!

Nimeamua kila nipatapo wasaa kujaribu kusaidia kuelimisha na kushirikisha mawazo wadau mbalimbali juu ya Teknolojia na Biashara, hasa Teknolojia ya Habari na Mawasialiano. Mara ya kwanza na ilikuwa ya mwisho kwa mwaka 2020 ilikuwa ni mwezi Septembe. Tafadhali pitia huko uone kama swali lako halijajibiwa kule kabla ya kuuliza tean!

Mambo muhimu ya kuzingatia kwenye mfululizo huu wa Ask Me Anything Technology and Business (AMATB). ni kama ifuatavyo:
1. Maswali yasiyo na lengo la kujifunza sitayajibu. Sababu ni kuwa lengo ni kushirikishana ufahamu niliopata neema ya Mungu kuwa nao na si vinginevyo.

2. Maswali yasiyohusiana na biashara na teknolojia sitayajibu. Hii ni kutunza focus kwenye mada husika.

3. Maswali yenye mrengo wa kisiasa sitayajibu. Kwa sababu ni nje ya lengo.

4. Maswali kuhusu maisha binafsi sitayajibu. Kwa sababu hii sio Biography. Unless yawe yanahusiana na mada na yatakuwa msaada kwa wasomaji, then nitaangalia namna bora ya kujibu.

5. Sipo hapa 24/7 na wala sina msaidizi wa kusoma hapa. So ukiweka swali lako uwe na uvumilivu.

Best rule: Kama usingependa uulizwe swali hilo ni vyema usiulize...!

Sept 2020 AMATB: September AMATB - Niulize Chochote Kuhusu Tehama na Biashara

Karibu!
Hivi ni namna gani ukijua coding utaweza kupata kazi na kutengeneza Pesa kwa hapa bongo,

Na ni kwa C++ na Python zinatosha kukupa hizo kazi?
 
Back
Top Bottom