Amani Thani: Mzalendo mpigania uhuru wa Zanzibar

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,857
30,205
vlcsnap-2016-01-03-20h35m32s576.jpg


Aman Thani



‘’….inataka ifahamike kuwa Ufalme wa Zanzibar ulikuwa ni Ufalme wa Katiba na Mfalme mwenyewe naye alikuwa Mfalme wa Katiba. Ni maarufu kua chama cha Afro Shirazi hakimtaki Mfalme. Basi ingekuwa na serikali ya kina Ali Muhsin nayo haimpendi Mfalme nini cha kuzuia Baraza yaTaifa isipasishe kwa pamoja kumuondoa Mfalme kwa kura. Ama hao wasemao kuwa Karume alimpa Ali Muhsin uwaziri katika Serikali yake yenye kuitwa ya"Mapinduzi", hao tena pahala pao pa kufaa kuishi ni katika hospitali ya wendawazimu, (Kidongo Chekundu kwa Zanzibar). Ikiwa kupewa cheo cha uwaziri ni tunza ya kushirikiana na Karume katika mauwaji ya wananchi na kumuondowa Mfalme, kisha kuyaita mauwaji hayo "mapinduzi", basi vyema, natuikubali, fikra hiyo.


Kwa hivyo basi, ni Babu na wenziwe ndiye aliyeshirikiana na Karume katika kumuondoa Mfalme sio Ali Muhsin, kwani ni yeye Babu ambaye baada ya kufuzu hayo 'mavamizi' alifanywa Waziri wa Mambo ya Nje! Mambo sio hayo tu, wapo vilevile wenye kusema kuwa Ali Muhsin aliambiwa Afro Shirazi na Makomredi wanapanga kuipindua Serikali lakini Ali Muhsin amedharau na amejibu, "Kwani Serikali ni kisahani cha chai?" Ukiuliza ni nani huyo aliyekwenda kwa Ali Muhsin kumwambiya maneno hayo na akajibiwa hivyo, kila aulizwae, jawabu ni hilo hilo kuwa, "Mimi nimewasikia watu wakisema." Na katika suala hili, wengine utawasikia wanasema aliyekuwa amesema hivyo, Ali Muhsin, na wengine husema Juma Aley na wengine, Dr. Idarus Baalawy, mradi kila apendaye kuvurumisha uwongo wake, huuvurumisha bila ya kiwewe chochote! Sheikh Ali Muhsin alikuwa ni mwongozi wa chama na uwongozi wenyewe sio kuwa ulikuwa kwa kuchaguliwa kuwa awe mwongozi, laa, uwongozi wake ulitokana na mapenzi tu ya umma wa Hizbu wenyewe mpaka kufika kumwita "Zaim", yaani kwa Kiswahili, Mwongozi.


Hata hivyo, Ali Muhsin hakuwa mwongozi wa Serikali, bali alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje. Mwongozi wa Serikali alikuwa Sheikh Mohammed Shamte Hamad. Usalama na Ulinzi ulikuwa chini ya Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo yaNdani, Sheikh Salim Kombo. Waziri Msaidizi wa Mambo ya Ndani ni Sheikh Rashid Hamad. Kwa hivyo, Ali Muhsin hakukhusika na kazi ya Ulinzi na Usalama wa nchi wakati huo. Waziri Mkuu Sheikh Mohammed Shamte mara tu baada ya kupata khabari za kuwa ma Afro na maKomredi wanajitayarisha kufanya michafuko kama yaliyofanywa Juni, 1961 hapo hapo alichukuwa khatua za kiserikali. Aliwaita wakuu wa Polisi na wakuu wa Idara ya Usalama ambao ndiwo waliyokuwa wamekhusika na usalma na ulinzi wa nchi na kuzungumza nao khabari zilizokuwepo nchini. Wakuu hao walimuhakikishia Waziri Mkuu kuwa wanazo khabari hizo, nao wameshajitayarisha kukabiliana na michafuko ya namna yoyote ikiwa itatokea maadamu haitokuwa yenye kutoka nje ya nchi. Kwa mwenendo wa Serikali za kidemokrasi, Waziri Mkuu kwa khatuwa hiyo aliyochukuwa amekuwa ametekeleza wajibu wake, yaliyobakia ni juu ya waliyokhusika na utekelezaji.


Ikiwa palifanywa dharau zozote katika masala haya hata yakatokea yaliotokea, na ikiwa kunastahiki lawama, na iwapo kulaumu kuna faida, basi lawama hizo ni kwa waliyokuwa wamekhusika na utekelezaji juu ya ulinzi wa nchi, si kwa Waziri Mkuu, wala kwa Mawaziri wake. Wao, walikuwa ni watungaji na wapangaji wa sheria na siasa ya nchi, kwa kufuatana na misingi na katiba ya nchi,hawakuwa watekelezaji, watekelezaji walikuwa wengine. Demokrasi hairuhusu "kuvaa kofia mbili" katika uendeshaji wa mambo ya nchi, yaani kofia ya utungaji wa sheria na kofia ya utekelezaji washeria. Ikiwa lawama ni kuwa kina Ali Muhsin walihishimu demokrasi, basi hilo ni suala la kuzingatiwa na kudurusiwa kwa namna yake…’’


Kutoka kitabu ‘’Ukweli ni Huu,’’ na Aman Thani
 
Inamaana hawa viongozi hawaoni riwaya zako au ni kiburi

Uyui Kwetu
,
Hayo maneno niliyoweka hapo si riwaya kwa maana ya hadith za kubuni.
Wala mimi sifahamiki kama mwandishi wa riwaya.

Inaelekea wewe ni mgeni hapa Majlis.

Soma tena na angalia chini utaona ni maneno kutoka kalamu ya Aman Thani
kutoka kitabu chake, ''Ukweli ni Huu.''

Aman Than ni Mzanzibari na alikuwa Katibu Mkuu wa Zanzibar Nationalist Party
(ZNP) baada ya Abdulrahman Babu kujitoa ZNP mwaka wa 1963.

Aman Thani ni hazina kwa mwanafunzi yeyote wa historia ya Zanzibar na Afrika.

Ameyaona yote yaliyopita katika siasa za Zanzibar kuanzia 1957 wakati wa kupigania
uhuru hadi yalipotokea mapinduzi mwaka wa 1964.

Baada ya mapinduzi Aman Thani aliwekwa kizuizini na baadae kuhukumiwa kifungo
cha miaka10 jela kazi ngumu Zanzibar kama mfungwa wa siasa.

Nimejifunza mengi katika nyaraka zake na kumbukumbu nilizoziona na namshukuru
kwa kunipa ilm ambayo sikupatapo kuwa nayo kabla.

Sidhani kama viongozi wetu wanakataza watu kufanya utafiti, kujifunza mapya na
kuandika kwa faida ya jamii.
 

Uyui Kwetu
,
Hayo maneno niliyoweka hapo si riwaya kwa maana ya hadith za kubuni.
Wala mimi sifahamiki kama mwandishi wa riwaya.

Inaelekea wewe ni mgeni hapa Majlis.

Soma tena na angalia chini utaona ni maneno kutoka kalamu ya Aman Thani
kutoka kitabu chake, ''Ukweli ni Huu.''

Aman Than ni Mzanzibari na alikuwa Katibu Mkuu wa Zanzibar Nationalist Party
(ZNP) baada ya Abdulrahman Babu kujitoa ZNP mwaka wa 1963.

Aman Thani ni hazina kwa mwanafunzi yeyote wa historia ya Zanzibar na Afrika.

Ameyaona yote yaliyopita katika siasa za Zanzibar kuanzia 1957 wakati wa kupigania
uhuru hadi yalipotokea mapinduzi mwaka wa 1964.

Baada ya mapinduzi Aman Thani aliwekwa kizuizini na baadae kuhukumiwa kifungo
cha miaka10 jela kazi ngumu Zanzibar kama mfungwa wa siasa.

Nimejifunza mengi katika nyaraka zake na kumbukumbu nilizoziona na namshukuru
kwa kunipa ilm ambayo sikupatapo kuwa nayo kabla.

Sidhani kama viongozi wetu wanakataza watu kufanya utafiti, kujifunza mapya na
kuandika kwa faida ya jamii.
Sorry kwa hilo Mohamedsaid najiuliza hawa viongozi wetu hawaoni historia hii
 
Sorry kwa hilo Mohamedsaid najiuliza hawa viongozi wetu hawaoni historia hii

Uyui Kwetu,
Viongozi wetu wanaziogopa historia za kweli zitakazoleta fikra kinzani.
Msikilize Aman Thani akizungumza kuhusu uhuru wa Zanzibar:

''…ikiwa uhuru wa tarehe 10 Disemba 1963 ulikuwa ‘’uhuru bandia’’ nao
ukaweza kubalika katika Umoja wa Mataifa, ukapata na kiti chake katika
Ukumbi wa Umoja wa Mataifa na ukapandisha na Bendera ya Zanzibar
huru katika Kiwanja cha Umoja wa Mataifa na Waziri Mkuu wa serikali
huru ya Zanzibar Sheikh Muhammad Shamte Hamad akaukhutubia
Ukumbi wa Umoja wa Mataifa na Wajumbe wengine kama wa Japan
akaukhutubia Ukumbi kwa kuipongeza Zanzibar, Ikiwa yote haya
yalikuwa bandia, basi tupeni hayo yenu ya binadamu ya tarehe 12
Januari1964 mnao yaita mapinduzi ambayo mnayajua kwa hakika kuwa
si ‘’mapinduzi,’’ bali ni mavamizi… ''
 
Mavamizi?nimeupenda sana huu msemo unaowakilisha ukweli wa kilichotokea Zanzibar
 
Back
Top Bottom