Amani ni kila kitu itunze isipotee ndani yako

Amani ni kila kitu itunze isipotee ndani yako

Nimepoteza hii kitu ,inner peace ,ni mateso makubwa sana
Pole mkuu, jitahidi kujipa furaha, jiepushe na mawazo mabaya, ugumu wa maisha n.k, kikubwa zaidi epuka kukaa pekeako huleta msongo wa mawazo zaidi, jitahidi kujichanganya na watu wa karibu yako wenye mitazamo chanya.
 
Katika ukimya nafsi hupata majibu ambayo kelele za ulimwengu huficha. Jipe muda wa kukaa kimya kila siku. Sikiliza sauti ya ndani yako, inayo hekima kubwa. Amani haipatikani kwa kubadilisha mazingira yako, bali kwa kubadilisha moyo wako. Amani ni kazi ya ndani. Usiitafute nje, itengeneze ndani. Wasiwasi hauondoi matatizo ya kesho, bali unaondoa amani ya leo. Ishi katika sasa. Yote yatakuwa sawa. Kuwa kama mti mkubwa kando ya mto. Maji ya maishani (matatizo\ yapite, lakini wewe baki na mizizi yako imara katika utulivu... Mjusi sina baya.
Dogo kumbe unakuwaga na madini.

Nyau ww
 
Back
Top Bottom