Amani katika jamii huwa hailindwi bali inazalishwa au ni matokeo ya tunu iitwayo haki

Gwappo Mwakatobe

JF-Expert Member
Nov 22, 2019
1,494
1,874
Amani katika jamii huwa hailindwi bali inazalishwa au ni matokeo ya tunu iitwayo haki. Amini na/au usiamini, amani kwa hakika, kwa uhalisia na kwa ukweli, ni tunda au zao la haki.

Ukitamani tunda la amani katika jamii huna budi kutunza mti unaoitwa haki, ndiposa amani inazaliwa, inatamalaki na kwa hakika inapatikana katika kipimo cha kujaa na kumwagika - inakuwa bwerere kila mahali na kwa kila mtu!!

Bila kutenda haki, kujali wengine, kuwaheshimu wengine, kuwalinda na kuwatunza wengine (hata kama wana udhaifu au unyonge), kamwe hatuwezi kuwa na jamii yenye amani.

Tunaweza kuwa na watu watulivu lakini wasio na amani mioyoni mwao. Nafsi zao hujaa visasi, machungu na hasira kali sana - hata kama hawaandamani. Na ndio maana amani si tu kutokuwepo vita, bali pia kutokuwepo dhuluma, udhalilishaji, uonevu na ukandamizaji.

Je, tunataka tunda la amani? Basi tuupalilie, tuutunze na kuuenzi sana mti unaoitwa haki. Only then, and indeed only when, peace becomes an automatic product or fruit of a nourished justice.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom